Asante mlioitabiria Simba kipigo cha 5G

Lihakanga

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2016
Posts
4,810
Reaction score
6,441
Mungu kweli si Athuman,

Baada ya kusoma comments mbalimbali humu kuelekea mechi ngumu ya Simba dhidi ya AS Vita, nilivunjka moyo mno kiasi cha kula chakula cha jioni na baada ya taarifa ya habari nikazima simu na TV na kukimbilia kitandani.

Saa 4.45 usiku nikachungulia YouTube nikaona bado simba haijafungwa halafu mtangazaji anasema Simba wamejitahidi na kwamba mechi ya mwisho katika uwanja ule muda kama huo Simba walikuwa wamekalia 3-0. Nikaona dharau dhidi ya Simba inaendelezwa kiaina.

Nikazima simu japo usingizi hakuna. Nilichungulia tena dakika kumi kabla ya mchezo kumalizika nikaona Simba 1 wenyeji wao 0. Nikajikaza kuangalia dakika zilizobaki hadi mwisho.

Nikiwa alone room kwangu niliamka kuwasha TV kana kwamba mechi ndo inaanza, nikaishia kuangalia hapa na pale kwa furaha ya ushindi wa Simba.

Kuna mchambuzi anajita Jeff, alisema kwamba kwa beki ile iliyocheza siku ya mechi kati ya Simba na Dodoma, Simba hawatafika mbali. Ni maoni yake, lakini tosha tu kusema kwamba asante kwa walioitabiria Simba mabaya kwa kuwa Mungu amewajibu utabiri wenu na roho mbaya haijengi hata siku moja. Isitoshe dua la kuku halimpati mwewe.

Simba imeanza hivi, inshallah mwenye Mungu aendelee kuisimamia hata katika mechi ya marudiano.

This is Simba. Not utopolo.
 
Basi ndugu yangu ulijikosesha Raha bure. Mpira umeanza kila timu ikimsoma mwenzake, Simba ikikamata mpira inapiga pass fupi fupi za kuchunguliana na wakipoteza kila mtu yupo kwenye position yake na washamburiaji wa pembeni kina Nixon wanarudi nyuma kuongeza nguvu kwa kina shabarara. AV VITA walipata free kicks kama mbili hivi ambazo kwa umahili wa Aish Manura zote alizicheza vizuri. Mpira mpaka mapumziko game 0-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Kasi kila team ikiwa ishamsoma mwenzake, Simba walifanya mashambulizi ya uwakika sasa kuonesha kuwa eanahitaji ushindi. Isingekuwa uchoyo wa Chama Simba dakika za mwanzo za kipindi cha pili tu ilikuwa iongoze baada ya kupigwa counter attack na mpira kumfikia Chama na kuambaa ambaa nao akilikimbilia goli la adui.

Ulijikatosha uhondo kuniangalia mechi tamu Kama ile
 
Mkuu nilifanya hivi kulinda afya. Yale yanayomkuta Manara hadi anapoteza network ndiyo hata mimi hunisibu. Simba au Taifa stars wakicheza huwa ninatetemeka na mwili hushikwa ubaridi hata kama jua linawaka.

We acha tu.
 
Mkuu nilifanya hivi kulinda afya. Yale yanayomkuta Manara hadi anapoteza network ndiyo hata mimi hunisibu. Simba au Taifa stars wakicheza huwa ninatetemeka na mwili hushikwa ubaridi hata kama jua linawaka.

We acha tu.
Daaah! Kumbe tunafanana! Ila hapo kwa TAIFA STARS…. mmmmmm.… .upo peke yako!
 
Mkuu nilifanya hivi kulinda afya. Yale yanayomkuta Manara hadi anapoteza network ndiyo hata mimi hunisibu. Simba au Taifa stars wakicheza huwa ninatetemeka na mwili hushikwa ubaridi hata kama jua linawaka.

We acha tu.
Bhasi usiwe unaenda uwanjani maana unaweza ukashikwa na kiharusi cha gafra Simba ikifanya vibaya.
 
Daaah! Kumbe tunafanana! Ila hapo kwa TAIFA STARS…. mmmmmm.… .upo peke yako!
Hata mimi Taifa Stars hii siifagilii, ifungwe ishinde niko normal tu. Taifa Stars ya Maximo kwangu ndio iliiyokuwa bora kipindi chote.
 
We ata ukulipewa kubwa utajibu asante yaan kama wanawake tu wakikojoleshwa
We shoga, usidhani siwezi kutukana. Ni uamuzi tu wa kujibu hivyo. Mbona unawashwa moyo kama unaliwa tigo. Acha ujuaji. Huwezi kuwa na akili kuliko wengine.
 
Utopolo jana walianzisha nyuzi zaidi ya kumi mbaya zaidi wengi walijifanya wakongo wakafikia hadi hatua ya kujichubua mwisho wa siku wameondoka na aibu
 
Dhidi ya Mbabane Dar kabla ya mechi
Leo mnapigwa hapa hapa nyumbani
Baada ya mechi
Simba 4
Mbabane 1
Mnaenda kufa kwao

Marudiano kwao
Mbabane 0
Simba 4
Mmekutana na vibonde hapo ndio mwisho wenu

Dhidi ya Nkana Dar
Mlikufa 2-1 kwao leo mnakufa tena safari ishaisha hiyo
Baada ya mechi
Simba 3
Nkana 1
Kimyaaaaaa [emoji1787]

Makundi
Al Ahly
Simba
As Vita
Js Saoura
Waarabu wawili na m-Congo mmoja hapo Simba anashika mkia na yule jamaa ndio akapigilia msumari kabisa kwa kutuita Under Dog wa kundi

Dar Simba dhidi ya Js Saoura
Waarabu wamekuja kuwapiga hapa hapa nymbn
Baada ya mechi
Simba 3
Saoura 0
Hawa sio waarabu ni wapemba ngoja waje Ahly [emoji1787]

Simba dhidi ya Ahly Dar (kabla)
Sasa leo ndio wamekuja waarabu wenyewe Taifa linaingia ktk aibu nyingine Cairo hamsa na leo hamsa tena
Ramadan Subhi wamemchukua kwa mkopo wa paun billion 10 thamani yake kikosi kizima cha Simba hakifikii thamani hiyo
Baada ya mechi
Simba 1
Ahly 0
Mmebahatisha tu lkn hampiti shughuli mtaiona ktk mechi ya mwisho dhidi ya As Vita hamsa zingine hapa hapa

Simba dhidi ya As Vita Dar
Leo sasa ndio mwisho wa safari mnakufa tena nyingi
Baada ya mechi
Simba 2
As Vita 1
Hamna lolote nyie mnawapulizia dawa wapinzani ndio mnashinda [emoji1787]
Yani kutoa hongera kwao imekua ngumu sana wanageuka vinyonga kila leo kwa kauli zao

Dhidi ya Plateau (Nigeria)
Kabla ya mechi leo Taifa linaingia kwenye aibu kubwa mnaenda kufa nyingi jamaa kila game wanashinda tano tano Enyimba kafa 5 na wengine kibao ni hamsa au 4G
Baada ya mechi
Plateau 0
Simba 1
Wanakuja kupindua matokeo Dar

Leo sasa mnakufa hapa hapa (kabla)
Baada ya mechi Dar
Simba 0
Plateau 0
Mmeshindwa kuwafunga kwenu hata hao wabovu ngoja muone Platinum

Dhidi ya Platinum Bulawayo,Zimbabwe.
Mnakufa nyingi leo
Platinum 1
Simba 0
Chikwende,Chikwende..na kelele kibao na huo ndio mwisho wa safari mnakufa tena Dar

Mechi ya marudiano Dar
Kabla ya mechi
Chikwende leo atakuepo tena
Kwa beki zenu hizo wazee Wawa na Onyango hapo Chikwende na wenzake wanakuja kufanya mauaji tena
Baada ya mechi
Simba 4
Platinum 1
Simba hawashindi mpk mapaka [emoji1787]
Hongera ni ngumu sana kutoa na maneno kila siku yanabadilika

Makundi
Al Ahly
Simba
As Vita
El Merreck
Daaah aibu imerudi tena kwa Taifa zile hamsa hamsa zinarudi tena

As Vita dhidi ya Simba (Congo)
Leo ndio zile hamsa zinajirudia aibu kwa Taifa kila baada ya dkk kadhaa goli,As Vita hatari sana kwao,mara watapakiwa mkongo n.k
Baada ya mechi
As Vita 0
Simba 1
Sasa hivi As Vita hamna timu wameuza sana wachezaji wao [emoji1787]

Hivi ndivyo ambavyo kila siku maneno yanabadilika wanakua vinyonga na wepesi kukana maneno yao ya awali

Simba mnawatesa sana watani mana sio wapinzani,kila wakichagua waume nyie mnaua wanatafuta mwingine mnaua wanapata sana shida hawa wajane

Na nyie wajane fc mjifunze kutoa hongera hata mara moja moja mtabadilisha mabwana mpk lini? mafanikio ya Simba ni mafanikio ya Taifa pia sbb tunawabeba nyie mwende kutembea na kurudi lkn hamna shukrani aibu yenu wenyewe

Tuliwakera sana 2018/19
Msimu huu 2020/21 kero zitaongezeka sbb hatuna nyumbani wala ugenini pagumu kwetu ni Cairo tu na tunauhakika wa kuvuka na kucheza hatua ijayo

Kila siku vitu vizuri tunafanya sisi,wanaume ni sisi,watu wa historia nzuri ni sisi,watu wa ushindi ni sisi,watu wa kulitangaza taifa ni sisi,watu wa kuleta heshima kwa Taifa ni sisi ila watu wa kuharibu ni nyie,watu wa kutia aibu ni nyie,watu wa kushindwa ni nyie,watu wa kuumia (maumivu) kila siku ni nyie,watu wa wivu ni nyinyi yani mnateseka sana..

Poleni sana


Simba Nguvu Moja
 
watu wanakariri
sijui wachambuzi uchwara watasemaje

mwishoni tulipowapa
define the term pira biriani?
tukawapa introduction kiduuchu.
watakapofika mkapa tutawapa notice za kusoma dakika 90 topic ikiwa
Pira biriani
halafu swali tutalowauliza ni
With vivid examples and concrete reasons and by explain in details on why baraka mpenja use the term pira biriani. ( hint use the term Larybwalya to support your answer)
 
Mshikaji yuko vizuri. Nahisi ana notebook kurecord matukio[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] ametisha kwa uchambuzi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…