Are dreams and visions real?

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
2,007
Reaction score
1,898
Nimeuliza swali hili kama vile sijui, lakini kiukweli ninajua. fuatilia mambo haya yaliyonitokea miaka kadhaa.

1. mwkaa fulani, nilikuwa nimelala, usiku nilianza kumtafakari Mungu. niliwasiliana na mke wangu aliyekuwa mbali kabisa (bara lingine na nilikokuwa nimesafiri) kumbe yeye kule naye ananiombea. masaa ya asubuhi ule muda ambao usingizi huwa mnono sana saa kumi hadi saa kumi na moja kabla hakujakucha, nilijikuta AMANI NA FURAHA ipitayo akili zote, its beyond description, ilinitawala ghafla, amani amayo hauwezi kuielezea na kama ni matakwa yako utatamani maisha yako yote uishi vilevile. mara nikaanza kusikia nyimbo nzuriiiiii sana, malaika wakiimba wimbo "YESU BWANA WA MABWANA, YESU MUNGU WA MIUNGU, MFALME WA WAFALME, YEYE ANAWEZA YOTEEE MPENI SIFAAA AAAAA, MPENI SIFAAA AHAAA AHAAA". nilipoamka, siku nzima na wiki zima nilikuwa natafakari na kuimba ule wimbo kimoyomoyo na wimbo ule haujawahi kusahaulika moyoni mwangu miaka 8 iliyopita. moyoni mwangu sikuwa na maswali, kuna kitu moyoni kilinihakikishia kuwa malaika wamenizunguka na vile niliwaona walikuwa wakimsifu Yesu.

2. mwezi huohuo nikiwa nimelala, ilikuja hali moja chafuuu sana, baridi ya ajabu isiyoelezeka, hali ya kuchukiza isiyoelezeka, nikaona kwa macho yangu ghafla ndege, nikapatwa na ganzi, nikaona ndege mkubwa sana, mfano wake ni kama amphibius Dinosaur kama wale wa kwenye mapicha ya holywood, mweusii, ana kucha ndefu na sura mbaya kupita kiasi, akaja akipeperuka akataka kunibeba aende nami. ghafla, nguvu ilitoka moyoni mwangu kwa shida kwasababu alinikaba, nikapaza sauti "KWA JINA LA YESU", yule ndege mwenye nguvu alipaishwa kama na upepo mkali usioelezeka, niliuwa nchi moja ya ulaya, nilihisi ni kama ameenda kudondoka bara la mbali sana na amedhurika kupita kiasi. kitu moyoni kikaniambia "huyo alikuwa adui, kuna kitu Mungu amepanga maishani mwako, adui anataka kukuangamiza kabla haujafanya hicho kitu". ni agent wa shetani alitumwa kuniangamiza, na niliona kwa macho yangu huyo ndege, asabuhi kama saa kumi na mbili nimeshafumbua macho kitandani ile mtu unavyotafakari uamka usiamke.

3. tulikaa miaka kadhaa na mke wangu bila kupata watoto. mke wangu akaota ndoto ana mtoto anayefanana sana na mimi. huyo ndio amekuja kuwa first born wangu.

4. kuna siku mke wangu alienda kanisani akawa anaombewa kupata mtoto, tulizunguka makanisa mengi, hapo hata huyo first born wetu hajazaliwa. mchana kweupe akaona kama maono watoto wawili wameshushwa na anakabidhiwa, kama utani vile, na Mungu alitupatia mapacha kadhaa. na uzao wetu unajirudia mapachamapacha tu.

5. Leo hii asubuhi, nilikuwa nataka kuamka saa 11 asubuhi, mara nikasema ngoja nilale kidogo mida kama ya saa 12, nikaona kama maono si maono au ndoto si ndoto. kuna mdada mmoja amevaa nguo ndefu ya kujisitirii vizuri sana, kama zile nguo za wanawake za zamani, amesimama kwenye njia ya kuelekea kanisani, njia ni nzurii sana, na kanisa linaonekana kwa mbali mlimani, yule dada alikuwa akiiimba wimbo wa kusifu, aliimba kwa kiingereza "YOU ARE THE LORD, YOU ARE THE LORD, YOU ARE THE LORD YOU ARE THE LOOOOOORD!" mwimbo huu tangu asubuhi hadi sasa hautoki moyoni mwangu. yule dada alikuwa anaimbisha, na kuna sauti nzuri sana zilikuwa zinatoka zikiitikia, kuna raha ya utamu moyoni usioelezeka, na nikaambiwa moyoni mwangu kuwa kuna nguvu sana na Mungu huwa anashuka sana watu wakiwa wanamwabudu na kumsifu. nikatafakari jinsi nguvu za Mungu zilivyoshuka paulo na sila walipokuwa gerezani, nikahakikishiwa hata leo hivi watu wakisifu na kumwabudu Mungu anashuka.

ninaposema nilihakikishiwa, watu wengine wanaweza wasielewe, kuna ndogo nyingi na maono mengi, siwezi maliza kuelezea. lakini mambo ya Mungu huwa hayana maswali. yaani jambo la Mungu likikutokea hautakuwa na maswali kichwani kama "atakuwa Mungu au ni njama za shetani"...kuna kuwa na uhakikisho fulani, hautauliza. ila ukiona una wasiwasi hauna uhakika, basi hapo sio Mungu. nina furaha ya ajabu.

nimeandika haya ili kuwapa moyo watu wanaoota ndogo na wana wasiwasi, wanaoona maono na hawaelewi. zaidi sana nimekuja kujifunza kuwa ndani ya Jina la Yesu kuna nguvu ya ajabu isiyoelezeka lakini sisi wanadamu hatujui, pia muda wote mbinguni ni kusifu na kuabudu plus walinzi/malaika wanaotumwa kutuhudumia sisi wanadamu au kufanya maelekezo ya Mungu. Mungu awabariki sana.
 
Amina kwa ushuhuda mzuri
 
ulimwengu wa roho ni bayana!

sent from servant of God
my friend, ulimwengu wa roho ni dhahiri kabisa kabisa, Mungu yupo anaongea na watu hata leo hivi kupitia ndoto na maono. namwomba Mungu anisaidie nimjue zaidi na anionyeshe mengi kuhsu yeye.
 
Hayo ni mambo ya rohoni ambayo hufunuliwa na Roho peke yake. Roho wa Mungu akiwa ndani yako lazima utapata maono kama hayo. Tatizo kwa wengi wetu tunaomjua Yesu ni kwamba adui ibilisi anatuzuia ili macho ya mioyo yetu yasitiwe nuru tuone mambo ya rohoni.
 
thats very right. mambo ya Mungu ni dhahiri na hayana maswali. wakati mwingine shetani anaweza kuleta makapi yake akijifanya malaika wa nuru, lakini mambo ya Mungu ni dhahiri hautauliza maswali, ndio maana hata Roho Mtakatifu akikujaa ukinena kwa kuugua kusikoweza kutamkwa, ile raha ya moyoni na ule udhihirisho hauna maswali..you don't need to ask someone kama hivi huyu ni Mungu au la, kwasababu kuna raha na utamu moyoni usioweza kutamkwa...its beyond description. kuna uhakikisho usioweza kutamkwa. ila yale makapi ya shetani yatakuacha na maswali. vivyohivyo na kwenye ndoto, ndoto za Mungu huwa zinakupa uhakikisho na haziondoki. pia mambo ya Mungu huja na amani ipitayo akili zote, ukiona kitu kimekuja bila amani jua hicho si cha Mungu. hata kama ni ndoto ya kutisha, lakini kuna ufafanuzi wa amani ya ajabu. hii ni kwasababu Yesu Kristo ni Mfalme wa Amani na Mungu mwenye nguvu. hivyo mambo yote huja na amani ya ajabu moyoni. Mungu awabariki sana wapendwa.
 
Niombee nipate wokovu
wokovu waweza kuupata ukiomba mwenyewe. Ukimkiri Bwana Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako na kuamini moyoni kwamba Mungu baba alimtoa afe kwaajili ya ukombozi wetu, utaokoka. Sema, Bwana Yesu Kristo, nakuja mbele zako Kwa JIna lako Yesu Kristo, ninakiri kwamba wewe ndiye mwokozi wangu unaye nipenda, ulikufa kwaajili yangu, ulimwaga damu kwaajili yangu, ninaomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kuwaza kunena na kutenda kwa kujua au kwa kutokujua, unioshe kwa Damu yako, ninamkataa shetani na mambo yake yote na kazi zake zote, ninakukaribisha uwe kiongozi wa maisha yangu. Katika Jina la Yesu Kristo ninaomba, Amin.

ukiomba sala hii kwa kumaanisha, utaokoka. sasa itabidi ujiunge na kanisa linalofundisha wokovu kama wewe ulivyookoka, ili ufundishwe namna ya kuishi maisha mapya ya wokovu. imeandikwa, tazama nasimama mlangoni nabisha mtu akifungua mlango, nitaingia kwake nami nitakula pamoja naye naye pamoja nami.

Isaya 53 yote ukiisoma utagundua kuwa Mungu alimtuma Yesu Kristo kufa kwaajili yetu. alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. sisi sote kama kondoo waliopotea kila mmoja wetu aligeukia njia yake, na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sote. Haleluyah to the Lamb of God!
 
Yesu Bwana wa Mabwana, Yesu Mungu wa miungu, mfalme wa wafalme, yeye anaweza yotee mpeni sifaaaaaaa, mpeni sifaaaaaaaaaaaaaa ahaaaaaaa ahaaaaaaaaaaaaa.

huu wimbo tangu niote ndoto/kama maono niliona malaika wakiuimba, wapo wengiii kwa sauti nzuriiiiiiiiii na zinazogusa moyo, zenye upako wa hali ya juu, haujawahi kunitoka moyoni. siusahau kabisa.

Yesu ni Mungu yuleyule, aliyefanyika mwili ili kwa mwili huu huu wenye madhaifu atukomboe sisi wanadamu. Isaya 53 neno linasema, kwa kupitia yeye makusudi ya Mungu yalitimia, na alizaliwa ili kupitia yeye tusamehewe..Yesu amekuja ili kumwaga damu iwe kafara ya milele kutupatanisha sisi na Mungu katika agano jipya. zamani Mungu aliingia maagano na wanadamu kupitia damu za wanyama, lakini Roho mtakatifu alifanyika mwili ili afanane nasi na afanyike kafara kwa kumwaga damu once and for all..hakuna haja tena kumwaga damu za wanyama kama katika agano la kale.

hapo mwanzo alikuwepo Neno, naye Neno alikuwepo kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu, akafanyika mwili, akakaa kwetu sote tukauona utukufu wake, utukufu wa mwanakondoo............, Yesu alisema mimi na baba u umoja....baba yu ndani yangu na mimi ni ndani yake....hivyo Yesu ni Mungu......

wakati Mungu anaumba mbingu na nchi, alikuwa anadiscuss (..na tufanye mtu kwa mfano wetu....), that means alikuwa anajadili..hapa ndipo panadhihirisha nafsi tatu za Mungu wetu, yeye ni mmoja lakini ana nafsi tatu yaani Mungu Baba, Mungu mwana (Yesu) na Mungu Roho (Roho mtakatifu).....vyote ni kitu kimoja ila utendaji tu.

kwasababu nafsi moja ilishuka duniani ikafanyika mwili na kutoa kafara la dhambi zetu na kututengenezea njia ya uzima.....Mungu mwenyewe ameapa katika Isaha 53 kuwa "for the sake of him (Jesus) i will forgive t heir sins"....Mungu anatupokea sisi kwasababu tu ya Yesu Kristo,...kama sio hivyo, hatuwezi kusogea mbele zake kwasababu tu wenye dhambi na Mungu ni mtakatifu hawezi kuchangamana na dhambi, ukisogea na dhambi zako (bila Yesu Kristo) utateketea, our God is a consuming fire....hivyo ukitaka kusogea mbele zake, lazima uende kwa mgongo wa Yesu. Mungu awabariki.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…