Aonywae mara nyingi

lutemi

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
1,750
Reaction score
1,402
Unapoonywa Mungu huruhusu uwe na nafasi ya pili kutafakari mwenendo wako wa mapito.
Lakini unapokaidi na kudharau hii humaanisha kwamba Umekataa sauti ya Mungu kupitia kwa wanadamu ambao Mungu ameamua kuwatumia kutuonya.
Maonyo yapo katika nyanja zote
Uchumi.....economics
Mahusiano.....relationship
Utawala.......administration
Maadili .....code of conduct
Uhuru.......general freedoms

Kuna nyakati huwa kuna kuwa na miluzi miingi sana lakini katika miluzi hiyo kunaweza kuwa na mluzi mmoja tu wenye maana na wenye sauti ya maonyo ndani yake.

Unaweza ukawa mlevi sio ulevi wa kawaida
Ulevi wa madaraka
Ulevi wa utajiri
Ulevi wa kazi
Ulevi wa majivuno na dharau
Kumbuka nyakati zote huwezi tambua kwamba umelewa mpaka yule naekutakia mema atakapo amua kusema yake yatakayo kuumiza.

Ukiona watoto wako kila unaporudi wanakimbilia chumbani Wakikuogopa tambua unatengeneza Janga kubwa sana .
Sio kila anaekupigia kelele anakushangilia
Sio kila anae piga makofi anakushangilia
Sio kila anaetabasamu anakupenda

Tujifunze kuhesabu nyakati zetu.
Nawaza tu
Post hii inataka intelligent persons to know where i’m heading.
 
Na asikie yule ajiitaye jiwe, kichaa, kwani majina hayo ni chukixo machoni pa bwana
 
Na asikie yule ajiitaye jiwe, kichaa, kwani majina hayo ni chukixo machoni pa bwana
 
maadili ni codes of conduct na sio codes of contact
 
Na asikie yule ajiitaye jiwe, kichaa, kwani majina hayo ni chukixo machoni pa bwana

Zamani zile wapo waliokuwa wanasema eee mfalme uishi milele nae mfalme akafikia hatua kutotambua mipaka ya utakatifu wa Mungu na utukufu wa mwanadamu ndipo wakatumia vyombo vya hekaluni.
Baada ya hayo likatokea neno
Mene mene tekel na peres

Mara nyingi tunaonywa majumbani kazini mashambani njiani kwa ndoto kwa njozi kwa viumbe asili inawezekana tusitambue kwamba ni maonyo.
Tiini wenye mamlaka
 
Methali: heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu.
 
Methali: heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu.



Bwana Mungu atusikie sana tunapoomba na atupe macho ya rohoni tutambue.
Lipo tumaini kwa wamwombao Mungu kwa mioyo ya dhati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…