Kama kuna mtu ameandika historia mbaya ya uongozi wa soka hapa nchini ni huyu bwana. Katika kipindi chake akiwa kama katibu ameshindwa kuwa thabiti na kusababisha migongano ya hapa na pale kati ya Klabu na TFF au kati ya Klabu na Klabu.
Matatizo aliyosababisha kwa uchache ni kama yafuatayo:
1. Kukosekana kwa waamuzi thabiti wa soka na kupanga waamuzi hasa wa mechi za Yanga kwa upendeleo
2. Kuwepo kwa usimamizi mbaya wa soka na fedha za TFF
3. Kuwa na maandalizi duni kwa timu zetu za Taifa
Na wenzangu ongezeeni hapo chini. Cha msingi kwake ni kujiuzulu ili kuleta imani kwa wapenzi wa soka na kujijengea heshima kabla ya kulazimishwa kufanya hivyo.
Kinachomlinda huyu jamaa ni kufanyakazi na waandishi wa habari kwa kipindi kirefu akiwa ni Mhariri, na ndio maana wanashindwa kumwandika mwenzao. Na hii ndio sababu hasa ya akina Tenga kumweka hapo ili kuzima madudu yao yasitoke magazetini, ila huyu jamaa ni kimeo hasa.
Hebu ona hata tatizo la ucheleweshaji wa ratiba ya ligi kuu, wakati ndio kazi kuu ya TFF ukiondoa maandalizi ya timu ya Taifa, inayoendelea kuporomoka kwenye viwango kila kukicha.
Jambo la muhimu alilofanya tangu aingie madarakani ni yeye kwenda kutibiwa India kutokana na matatizo ya kichwa, lakini mambo mengine yote amekuwa akichemsha tu, na hakuna wa kumkosoa kwani kila mwandishi ni rafiki yake au vijana wake aliokuwa akiwatuma kazi alipokuwa mhariri.
Kama kuna mtu ameandika historia mbaya ya uongozi wa soka hapa nchini ni huyu bwana. Katika kipindi chake akiwa kama katibu ameshindwa kuwa thabiti na kusababisha migongano ya hapa na pale kati ya Klabu na TFF au kati ya Klabu na Klabu.
Matatizo aliyosababisha kwa uchache ni kama yafuatayo:
1. Kukosekana kwa waamuzi thabiti wa soka na kupanga waamuzi hasa wa mechi za Yanga kwa upendeleo
2. Kuwepo kwa usimamizi mbaya wa soka na fedha za TFF
3. Kuwa na maandalizi duni kwa timu zetu za Taifa
Na wenzangu ongezeeni hapo chini. Cha msingi kwake ni kujiuzulu ili kuleta imani kwa wapenzi wa soka na kujijengea heshima kabla ya kulazimishwa kufanya hivyo.
Mimi natofautiana na wengi hapa.Labda tujiulize maswali kwamba Angetile ameshindwa kuongoza TFF kama Entity au ameshindwa kuongoza soka la Tanzania kama sector.Kwa sababu unapoongela failures za TFF huwezi kuacha kuongelea failures kwa soka la Tanzania.Na kwa maoni yangu mimi kushuka(failures) za soka la TZ/TFF ni mfumo zaidi kuliko mtu mmoja na kwa watu ambao tupo kwenye soka la Tanzania tunaweza sema TFF kuna transparency zaidi kuliko kipindi chochote nilichokiona,lakini hii inawezekana kutoka na kipindi tulichopo.
TFF ipo kwa kushirikiana na serikali kuendeleza policy(kama zipo) za kuendeleza na kunyanyua kiwango cha soka letu,vitu kama michezo ya UMITASHUTA,UMISETA ndio ilikuwa chimbuko la wanamichezo wetu sio kwa soka tu hata michezo mingine.
Kwa hiyo nafikiri tusiangalie tu failures za Angetile kama yeye bali TFF kama chombo kwa upande mmoja na serikali kwa uapnde mwingine.Na tuache ugonjwa tulio nao waTanzania wa Usimba na UYanga