Chama kinachotawala Afrika kusini (ANC) kinakaribia kuanzisha sheria ya kishetani inayohusu kulinda siri za serikali ambayo inapingwa vikali na wanaharakati akiwemo mshindi wa tuzo ya amani ya 'Nobel' Mchungaji Desmond Tutu. Kinachohofiwa na wanaharakati ni kwamba sheria hiyo inaweza kutumika kuficha wizi na ufisadi wa watawala.