Anawaza Sam Ruhuza kuhusu 4R na Kinachotokea kwenye sakata la Gwajima kuhusu utekaji na hatua za Bunge na Chama Chake kumshambulia mleta habari njema

August

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2007
Posts
10,523
Reaction score
6,462
Na Sam Ruhuza

Ninawaza kwa sauti!!

Hizi siku mbili tatu nimekuwa sijielewi ni kama vile naangalia tamthilia au sijui ni ya kweli yaani sijui tu nabaki nawaza tu!!!
Nilimuona Askofu Josephat Gwajima Mbunge Kawe akiongea ba wanahabari na kulaani utekaji wa watu unaoendelea na kusema hao wanaoteka anaamini ni kikundi cha watu na wala sio vyombo vya usalama wala chama chake cha siasa na kuvitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua kukomesha hili.
Alitolea mfano watoto wa Viongozi wakuu pamoja na wake wakitekwa, je huu ukimya wa utekaji utaendelea??!!
Alitoa pia mawazo ya namna ya kuboresha vyombo vya usalama ili viweze kuwa huru zaidi na hivyo kupambana kiurahisi na watu wasiojulikana ambao sasa ni kero la Taifa maana wana nguvu mno kuliko vyombo vya usalama.

Baada ya kutoa mawazo yake kama Raia na kulaani yaliyowakuta wanaharakati wa Kenya na Uganda, tulitegemea moja kati ya mawili, yaani Serikali kukubali kupokea mawazo yake au kukataa basi na sio zaidi!

Ajabu ambayo imetushangaza wengi...

Kesho yake Wabunge wakaacha kujadili bajeti ya Wizara ya.Ndani kwenye kuimalisha ulinzi na usalama na maslahi ya Askari wetu, wao wakawa bize kupambana na Mbunge mwenzao Gwajima na hata kukitaka chama chao kimtimue uanachama kwasababu tu amemtolea mfano mtoto wa Mkuu akitekwa! Yaani Wabunge ni kama vile waliongea kuwatetea watu wasiojulikana kuteka watu!!

Kwenye mkutano wa chama chao, Mkiti wao akawaomba wajumbe kuwaweka nje wakina Gwajima maana ni wanachama wanaocheza ngoma sio yao!! Yaani sijui kulaani watekaji ndio ngoma isiyo ya chama chao, hivyo labda alitakiwa kuwapongeza watekaji!!

Jana kubwa zaidi, baada ya kutangaza siku 7 za maombi ya Taifa, Kanisa lake linafutwa na Msajili Serikalini sijaielewa sababu vyema maana nilichokisoma kwenye hiyo barua sijaelewa!!

Ukiwaza kauli za viongozi kuhusiana na kumjibu Gwajima, unakosa majibu na kubaki na maswali yako tu!

Nawaza kwa sauti...
  • kosa la Askofu Gwajima ni lipi?!
  • Kanisa linafungiwa kwasababu ipi?!
  • Gwajima alipoingia kwenye Ubunge haikuwa kuchanganya Dini na siasa, ila baada ya kulaani utekaji, Kanisa limekuwa la siasa!!??
  • Kanisa ni la Mtu au Taasisi?! Msajili anaposajili Kanisa anakuwa amejiridhisha vipi, maana kufuta Kanisa ambayo ni Taasisi kwa kosa la kiongozi kunaashiria makosa ya Msajili kwenye usajili!
  • Makanisa mengine makubwa yanatoa mawazo yao tofauti kuhusu kulaani utekaji wa watu, je nayo yatafutwa?! Kwanini Kanisa la Ufufuo??!!
  • Askofu anawataka waumini wafunge siku 7 kuliombea Taifa ili utekaji uishe nchini, siku ya 1 tu mnalifuta Kanisa na Police kulizingira Kanisa, je mnataka Waumini na wananchi waamini nini katika hilo??!
  • waumini waliojenga Kanisa watasali wapi?!
  • kuna kosa la watumishi kutumia madaraka yao vibaya, je hili nalo limo??!

Naendelea kuwaza kwa sauti. ..
Mkiti wa chama amesema muwaweke nje ya chama kina Gwajima maana ngoma ya chama chao sio hiyo wanayoicheza..
  • Je Chama chao ndio watekaji?!
  • Je kikundi alichodai Gwajima ni cha chama chao?!
  • Je hao watu wasiojulikana ni wa chama chao?!
  • Je kuhoji utekaji watu ndio kucheza ngoma isiyo ya chama chao?!
  • Je ninani anapaswa kuhoji kumaliza utekaji?!
  • wanachama nao walishangalia na kupongeza hiyo kauli, je nao wanakubali kukaa kimya kulaani utekaji ili wajitenge na Gwajima??!!
  • Je ni lugha ipi inayotumika kwenye chama chao kuhoji utekaji?!
  • Je wananchi waache kulalamika na kukubali tu watu watekwe na kupotea?!

Katika hili dogo tu, je zile 4Rs zimekimbilia wapi tena??!!
Aagghh! Yaani nimebaki na maswali mengi mno naendelea kuwaza simalizi!!

Nahisi kuna mtu amekanyaga waya huko, arudishe kwenye sehemu yake, dish lisome vizuri!!

Upendo! Tupendane jamani! Maisha haya ni ya kupita tu na kila mmoja ataondoka na sote tutakuwa majivu tu na usimtofautishe majivu!
Tuthamini uhai wa kila mmoja na tutumie vyema nafasi zetu ili tuache historia nzuri.

Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿🤝💪
 
Black shadows behind the darkness.. The ultimate capture.. Being held captive without seen handcuffs.. ! A paw in the bottle🤔
 
Inasikitisha sana ila hatimaye watanganyika wote wenye utimamu wa akili tumeelewa na kuwatambua watekaji na wauaji wa watu wasio na hatia, ila uzuri ni kwamba kila mwanadamu aliyezaliwa na nwanamke atakufa tu, hata wewe Maushungi (Macho kurembua)utalamba mchanga tu.
 
...
 
Maushungi ya uongo to..
Anajifanya binadam kumbe hana utofauti na shetani..
 
Nani atuondolee Askofu msumbufu
 

Attachments

  • Screenshot_20250601_171956_Samsung Internet.jpg
    294.4 KB · Views: 14
Ninapoiwaza Israel inapopigania raia wao wanaotekwa na miili yao waliouliwa na maadui zao. Nalinganisha na serikali yetu inavyowachukulia raia wao waliotekwa kupotezwa na kuuliwa na WASIOJULIKANA nabaki najiuliza upendo wa nchi kwa watu wake umeenda wapi ?!.

Je tatizo ni chama na sera zake !! Je kwao chama ndiyo taifa ?!. Nakumbuka mwenyekiti wa uvccm Bukoba akiwaamuru police kutokumtafuta yeyote watakayempoteza. Kufikia hapo na kauli za kusema Gwajima anacheza ngoma isiyo yao. Unajua WASIOJULIKANA ni mradi wa nani.
 
Huyu jamaa pamoja na Mbatia ndio waliuza mali za NCCR Mageuzi. Dar ina matapeli wengi sana.
 
Mkuu jana kuna kibonzo kiliwekwa na DW kikionesha watu wawili wakiwa na dereva mmoja mwanamke,wale watu wawili mmoja akasema mwambie dereva tumeacha njia,yule aloambiwa amwambie dereva akajibu 'unataka nishushwe njiani?,ko msingi wengi wa hao jamaa wanawaza chakula chao na familia zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…