Yaani leo asubuhi na mapema nimejitokea hadi masaa ya mchana nikaopoa mdada wa mjini ,ila uzuri wake si wakawaida ,natural hana poda wala mkorogo,mwili namba tatu ,juu akiwa mwembamba kuteremkia chini katanuka ,yani katanuka kifua kidogo kbana mbavu katanuka kushukia kiuno kabana kiwembamba kwenye magoti ,alimuradi hiyo picha nimekupa haitoshi ,sio msomali inawezekana kwa alivyonambia anatokea sehemu za arusha au karatu au karibu ya karatu.
Katika mazungumzo kaonekana kachoka na mahangaiko ya mjini anavyodai alikuwa amekuja kutafuta mashine za kutengenezea juice na pia kafriji kadogo na kafreezer .Andai ni mjasiria mali ,hayo hayakunishughulisha kwani moyo wangu wote ulikuwa umejaa yeye kwa jinsi alivyo ,unajua simba ana njaa halafu kaona nyama si kawaida kuonekana katika anga zake.
Nikamuambia basi anaonaje akapumzike nyumbani ,akanihoji uko na nani ,nikamuambia kwani unaogopa watu ,hapana unajua nyumba zingine bwaaana ! Alinibu.
wewe ni mgeni wangu hata kama kuna watu hawataweza kunihoji na zaidi watakukaribisha ,ah lakini naona nitachelewa ,nikamwambia kwanza usiogope nipo peke yangu na kuchelewa labda iwepo sababu ,akajibu hizo sababu ndizo zinazochelewesha ,nikamjibu usijali ,akakubali huku akihoji kwani sio mbali ,kwa bahati nyumba niishio inaonekana nikamwambia ,ileeeee pale ,tukaelekea ,ushakulah ,nimekunywa soda tu hapa nilipo nilikuwa natafuta seemu nipate chai,kwa bahati nilikuwa na hela ,tukapitia supermarket au dukani tukanunua keki na juice za kutosha.