Wana JF wenzangu huyu ni mwanangu kamaliza juzi CPA anasubiria matokeo naomba kwa yeyote anayefahamu mahali penye kazi itakayomfaa huyu mwanangu please naomba tusaidiane kwani kazi zimekuwa ngumu sana. Nimeona niwashirikishe najua sitakosa mawazo mazuri hapa. Naomba kwa wazoefu wa kupata kazi na wanaojua nafasi za kazi please tushirikiane tuokoe vijana wetu wasiingie kwenye majanga mabaya.
Nawatakia kazi njema
Ushauri wangu wa haraka Bcom + CPA without any practical experience bado hatoweza kumudu mikikimikiki makazini. Sehemu za kazi wengi wao hawajathubutu kugusa hiyo mitihani ya CPA lakini wanafahamu wanachopaswa kufanya. Anapoajiriwa mtu mwenye CPA wafanyakazi wa zamani wanatabia ya kutokumwelekeza chochote kwa kisingizio si ana CPA afanye basi.
Ushauri wangu sehemu ambayo wako "willing" kufundisha kazi na mtu akaiva ni kampuni za ukaguzi. Mshauri atafute hata kazi za kujitolea kwenye audit firms atatoka haraka sana
Asante sana ndugu huko ameshaomba anasubiri tu amejaribu ndugu yangu asante sana
Mimi niko Arusha kwenye audit firm nina volunteers kama wanne na kama unavyofahami msimu wa kazi ndio uko ukingoni kabisa