Amemfumania mchumba wake aki cheat, afanye nini?

Huyo binti anatakiwa amuombe msamaha mchumba wake. Kwa nini amfanyie ambush saa tano usiku? Jemaa angekuwa na bastola ingekuwaje?

Kama alishindwa kumwambia kwamba amekutana na huyo msichana unategemea amwambie eti leo kuna demu anakuja au alikuja kulala kwangu ni lazima angefanya kicricri. Mi namshauri amwache co unaamua kua nae then unakuja kujutia baadae!
 


Kusamehe inaweza kuwa ni jambo zuri, lakini kuna vitu muhimu ambavyo mfumaniaji anatakiwa kuchunguza na kujiridhisha kuwa vitabaki sawa. Na mbona kamsamehe haraka hivyo? Ana uhakika gani kama alicheat mara moja tu? Ana uhakika gani kama alicheat na msichana mmoja tu? Kuna sababu gani ya kuwa na uchumba wa zaidi ya miaka 4 bila ndoa? Na afya je? Ana uhakika gani kama huyo jamaa alitumia kinga na hajaambikizwa gonjwa lolote na hasa ukizingatia nyie vijana mnatumia kila kitu kwenye mapenzi?

Ushauri binafsi, ni bora angempa muda kidogo na kufuatilia baadhi ya vitu muhimu kuliko kusamehe kwa haraka kiasi hiki! Nalazimika kuhisi kuwa kwa sababu kaambiwa kuna mpango wa ndoa, na yeye anataka ndoa, ndiyo maana kalegea mapema hivyo.
 
Ushauri wangu ni hivi: Kama huyo dada ni mwaminifu asilimia zote kwa mchumba wake basi namshauri amwache huyo mwanaume lkn Kama na yeye amewahi kupita kando hta km hakukamatwa basi amsamehe.
 
AKUMULIKAYE MCHANA, USIKU ATAKUCHOMA... safari ya cheating ikianza mapema hivyo basi binti atarajie makubwa ndani ya ndoa
 
Tukumbuke kwamba WANAWAKE WAKO WENGI SANA LAKINI SIO WOTE WANAOFAA KUITWA "MKE WA MTU"....alichokifanya huyo kaka ni tamaa tu za mwili wake zilimshinda kujizuia akajikuta kamtamani huyo dada....lakini pia tukirudi upande wa dada( mchumba) je kaka alipokuwa anataka " vituz" ulimpa bila tatizo??
Sasa kama dada anajiamini anatakiwa amsamehe kwa kujiamini kwamba yeye ndo "MWANAMKE BORA" NA SIO "BORA MWANAMKE"
Wanawake wa kisasa tunatakiwa kujiamini na hayo yaliyotokea ndo yatawafanya hao wachumba wajifunze kwamba ni wapi walikosea ili wajirekebishe na watakapoingia kwenye ndoa itakuwa ndoa imara sana....Nawatakia kila la kheri kwenye ndoa yao!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…