‘Ambulance’ nusura ichomwe moto

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,077
Reaction score
34,848


Wananchi hao walidai kuwa gari hilo la wagonjwa halina msaada kwani muda mwingi haliko kituoni hapo hivyo kutaka kulichoma moto.



KWA UFUPI

  • Ni baada ya kuchelewa kumchukua mgonjwa, ambaye baadaye alifariki dunia.


Sumbawanga. Wananchi waliotaka kujichukulia sheria mikononi, nusura walichome moto gari la wagonjwa lilitolewa msaada Kituo cha Afya Mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa kutokana na madai ya kuchangia kifo cha mwalimu mmoja aliyekosa msaada wa haraka wakati wa kujifungua.

Wananchi hao wanadaiwa kulishambulia gari hilo kwa mawe na kuvunja moja ya kioo.

Gari hilo linadaiwa kuchelewa kuja kumchukua Mwalimu Leah Mgaya wa Shule ya Msingi Mtowisa ‘A', ambaye alifariki baada ya kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua.

Habari kutoka sehemu ya tukio zilizothibitishwa na Ofisa Tarafa ya Mtowisa, Peter Masindi zinaeleza kuwa, awali mwalimu huyo alipelekwa katika kituo hicho cha afya juzi saa 3 asubuhi akiwa katika hali uchungu wa kujifungua, lakini baadaye ilionekana anahitaji kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa.

Masindi alisema kutokana na hali hiyo ililazimu kupiga simu Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya saa 6 mchana ili kuomba msaada wa gari, lakini gari hiyo ilichelewa kufika kutokana na kudaiwa ilisafiri kwenda wilayani Nkasi, na hata iliporejea jioni ilikwama njiani kutokana na hali ya mvua.

Mmoja ya wananchi waliozungumza na gazeti hili, Mwaipungu alisema kifo cha mwalimu huyo kiliwakera wananchi wa eneo hilo, ambapo walikusanyika kwenye makundi na kuanza kujadiliana.

Wananchi hao walidai kuwa gari hilo la wagonjwa halina msaada kwani muda mwingi haliko kituoni hapo hivyo kutaka kulichoma moto.

Hasira za wananchi hao zilionekana baada ya kufika kwa dereva wa gari hiyo aliyefika, huku akiliza king'ora lakini alipokelewa kwa mabango, kabla ya kumsimamishwa kumtaka kuwapa funguo za gari, jambo lililopingwa na dereva. huyo huku wananchi hao wakilishambulia kwa mawe. ‘Ambulance’ nusura ichomwe moto - Kitaifa - mwananchi.co.tz






 

miundo mbinu mibovu magari machache ya kubebea wagonjwa, ndiyo janga la nchi hii kwa wagonjwa, Mungu ailaze mahala sitahiki mwalimu Amena
 
they have points this people, kwa sababu hiyo ambulence ilitolewa na watu wa AMREF katika kituo hicho kwa ajiri ya emergence zote za akinamama wajawazito ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ila mdada wote hiyo gari ipo mjin haikai kituoni.
 

lilikua ziara ya kichama jamani tuvumiliane tu ni mambo yakawaida tu jamani si unajua akija kiongozi mkubwa kutoka makao makuu lazima tuandamane nalo
 
they have points this people, kwa sababu hiyo ambulence ilitolewa na watu wa AMREF katika kituo hicho kwa ajiri ya emergence zote za akinamama wajawazito ili kupunguza vifo vya mama na mtoto ila mdada wote hiyo gari ipo mjin haikai kituoni.

Kwa mtindo huo walikuwa na haki yakufanya walichokifanya'
 
Wakilichoma linaungua, then....? marehemu atafufuka au?
Litaungua serikali itapata hasara then kodi yao waliochoma itanunua then....|?
Baadhi wanaweza wakasotajela miaka kadhaa kwa kitendo walichofanya cha saa moja then....?
Suluhisho la kuhamisha kivuli sio kukata mti bali ni wewe kukifuata kivuli
 
kwa nini uwe na ambulance isiyokuwa na msaada wakati wa emergence?Tusiwafanye wananchi ni wapuuzi kiasi hiki kwamba hawajui kufanya maamuzi.
This community will be praised for being in line with MDG4&5.....
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…