Amani ni kila kitu itunze isipotee ndani yako

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
7,442
Reaction score
12,710
Katika ukimya nafsi hupata majibu ambayo kelele za ulimwengu huficha. Jipe muda wa kukaa kimya kila siku. Sikiliza sauti ya ndani yako, inayo hekima kubwa.

Amani haipatikani kwa kubadilisha mazingira yako, bali kwa kubadilisha moyo wako. Amani ni kazi ya ndani.

Usiitafute nje, itengeneze ndani. Wasiwasi hauondoi matatizo ya kesho, bali unaondoa amani ya leo. Ishi katika sasa. Yote yatakuwa sawa.

Kuwa kama mti mkubwa kando ya mto. Maji ya maishani (matatizo\ yapite, lakini wewe baki na mizizi yako imara katika utulivu... Mjusi sina baya.
 
Nimepoteza hii kitu ,inner peace ,ni mateso makubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…