Aliyekaa chini ya ardhi siku 41 aomba msaada

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,274
Reaction score
25,322
Wambura (51), alitembelewa na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake na kuomba msaada wa Sh. milioni 25 kwa ajili ya matibabu nchini India, baada ya matibabu yake kushindikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili mtoto wa Wambura, Marwa Chacha, alisema hali ya maisha nyumbani inazidi kuwa ngumu, licha ya kuishi maisha ya kimaskini na familia yao wako watoto 10 na wameishauza ng’ombe 15 waliokuwa nao.

Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikotibiwa Wambura kwa miezi sita, ubongo wake upande wa kushoto umesinyaa na kusababisha mwili mzima kutetemeka, hali inayomfanya kuzungumza kwa taabu.

Wambura alifukiwa ndani ya machimbo ya Nyangalata, Oktoba 5 mwaka 2015, akiwa na wenzake Msafiri Gerald, Joseph Bulule na Amos Kuhangwa.

Mchimbaji Onyiwa Kahindo alifariki dunia akiwa hospitali na Musa Supana alifia shimoni baada ya kukataa kula mende, vyura na magome ya miti na nguo walizokuwa wamevaa.

Wambura aliomba mtu yeyote atakayeguswa anaweza kumchangia kupitia simu namba 0758 885 378 au 0757 650 301.


Chanzo: Nipashe
 
Kuna watu wanapitia magumu sana,Mungu amsaidie.
 
Yarrab mrejeshee afya yake mja wako.
Kwa magumu aliyopitia atakuwa amekutambua kuwa upo mola wake na ameshakutaja sana.
 
hawa wachimbaji wadogo wadogo hamna namna ya kuwawezesha kupata bima. Hii hali inatisha sana ,familia yake ipo katika wakati mgumu sana .
 

​
MMOJA kati ya watu sita waliokaa siku 41 chini ya ardhi kufuatia kufunikwa na kifusi katika machimbo ya Nyangalata, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Chacha Wambura, anaomba msaada wa matibabu.

Wambura (51), alitembelewa na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake na kuomba msaada wa Sh. milioni 25 kwa ajili ya matibabu nchini India, baada ya matibabu yake kushindikana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili mtoto wa Wambura, Marwa Chacha, alisema hali ya maisha nyumbani inazidi kuwa ngumu, licha ya kuishi maisha ya kimaskini na familia yao wako watoto 10 na wameishauza ng’ombe 15 waliokuwa nao.

Kwa mujibu wa ripoti ya madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikotibiwa Wambura kwa miezi sita, ubongo wake upande wa kushoto umesinyaa na kusababisha mwili mzima kutetemeka, hali inayomfanya kuzungumza kwa taabu.

Wambura alifukiwa ndani ya machimbo ya Nyangalata, Oktoba 5 mwaka 2015, akiwa na wenzake Msafiri Gerald, Joseph Bulule na Amos Kuhangwa.

Mchimbaji Onyiwa Kahindo alifariki dunia akiwa hospitali na Musa Supana alifia shimoni baada ya kukataa kula mende, vyura na magome ya miti na nguo walizokuwa wamevaa.

Wambura aliomba mtu yeyote atakayeguswa anaweza kumchangia kupitia simu namba 0758 885 378 au 0757 650 301

Chanzo: Nipashe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…