AKILI ni NYWELE

olele

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2010
Posts
1,305
Reaction score
1,578
Kuna jamaa walianzisha ZOO (bustani za kufugia wanyama wa porini) basi wakaweka wanyama wote sasa kimbembe kikawa kumpata nyani, jamaa hangaika kweli hawakumpata, wakakubaliana mmoja wao avae kinyago awe nyani, ikaonekana freshi jamaa akawa anavaa kinyago anaruka ruka kwenye banda mbwembwe kibao pesa inaingia, siku moja wakaja wazungu jamaa akaambiwa hela itaongezeka, jamaa akazidisha mautundu mara aruke tawi hili mara aruke sarakasi, ilimradi katoa burudani ya nguvu, mzungu mmoja akatoa ndizi akamrushia jamaa akataka kuwaonyesha akapiga sarakasi kama tatu hivi hewani, sasa kumbe kule juu kulikuwa hapajazibwa akapitiliza kwenye banda la pembeni yake ambako kulikwa na simba. Balaa lililotokea hapo unaweza kulihisi?

nyani ngabu.
 
akabadilika kuwa msosi wa simba mwe
 
Mh! Teh teh teh! Nyani ngabu! Sitaki kuumia mbavu! Nawahi bar!
 
jamani haja ndogo yataka kutoka kwa kicheko..........
 
Simba mwenyewe alikuwa ni mshkaji aliyevalishwa kinyago ka simba..wala nyani ngabu hakuthurika
 
Baa, sasa bwana wewe jeee! kuruka ruka huko bila banda la chimba kuwawakuwaje?
 


Kilichio tokea:
Simba akamwambia:
Tulia dogo...tutatimuliwa kazi hapa!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…