hongera saana TRA, mmefanya kazi nzuri saana , mpira wa miguu ni mchezo unaotakiwa uwe wa mfano kwa matendo mazuri, kwani watoto wote wa kike na kiume wakiwa wadogo wote hupenda kucheza mchezo huo , sasa hapa kwetu mchezo huu bado unachezwa na watoto, maana hao walioshika uongozi wa mpira baado wana mawazo ya kitoto, TRA wabaneni mpaka walipe hizo fedha na fuatilieni mpaka faini wanazozipiga klabu hakikisheni mnakata kodi yenu. na zile fedha wanazopokea toka fifa kateni kodi mpaka watie akili na wawe mfano bora.maana hawa watu ni wavivu saana hata wa kusimamia mapato sahihi ya viingilio vya milangoni .siku moja simamieni nyinyi wenyewe ukataji tiketi na uingiaji uwanjani muone fedha kibao mtakusanya nasisitiza TFF ni wazembe,wazembe ile mbaya hivi inakuingia akilini kudaiwa hiyo fedha na hawana mikakati yoyote ya kulipa zaidi ya kufikiria kulipiwa au kusamehewa jamani hata kualika timu toka nje na kuandaa mashindano fulani mnashindwa?
nchi yetu ina udhaifu mwingi saana, ktk hili kwanza nashutumu saana kada ya uandishi wa habari , wanapaswa wachunguze na watupe taarifa njia ya malipo ya mishahara ya hawa watu ilikuaje? mf; walikuwa wanapokelea mshahara pale tff kwa maana ya wizara inaingiza kwenye akaunt za tff au walikuwa wanapokelea moja kwa moja wizarani? au walikuwa wanamlipa kienyeji mtaaani? kumbuka mh SUGU amekuwa anapiga kelele saaana juu ya hawa wasanii kutoka nje wanalipa kodi? na njia ya malipo yao inafanyikaje? binafsi napenda saana hawa TFF wabanwe mbavu haswa hebu ona mwenyewe mikakati yao, imekaa kikuhurumiwa badala ya kufuatilia na kubuni jinsi gani? ya kulipa hizo kodi, ahadi ya rais aliitekeleza kocha alikuja na hakuwahi kulalamika juu ya mshahara na hata akawaita na makocha wengine toka kwao kwa ajiri ya timu za vijana nao vp au tff ilipandia hapo na kukwepa kodi.Yote unayoongea juu ya udhaifu wa TFF nayakubali, lakini suala langu ni Hao makocha waliokuja kwa ahadi ya JK je TFF walitaarifwa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama na kama ndiyo je ahadi ya JK alikuwa anatuhadaa watanzania?
Siamini kama tff wana hela kwenye akaunti.
kibogo elewa kitu kimoja mwajiri wako akikulipe TShs. 1,000,000 ni wajibu wake kukukata wewe kibogo kodi ya mapato ya TShs. 1,000,000 na kuiwakilisha TRA. Haijalishi hiyo TShs. 1,000,000 ilitoka kwa nani kinachoangaliwa hapa ni kwamba wewe kibogo umepokea pato la TShs. 1,000,000 yule anayekupa hizo pesa anawajibika kukusanya kodi ya serikali na kuiwakilisha kunakohusikaNdugu wana JF nimesikia kupitia Channel 10 kuwa TRA wameamua kuifilisi akaunti ya TFF na sababu za msingi za wao kufanya hivyo ni TFF kushindwa kulipia gharama za makocha wa timu ya Taifa Kuanzia MAXIMO NA POUSELN, Nimepata shaka sana kwani katika kumbukumbu zangu hii ilikuwa ni ahadi za Rais Kikwete kuwa serikali italeta Makocha wa kigeni ili kuinua kiwango cha Soka hapa Bongo na italipia gharama zote za makocha hao.
My Take.
1. Kama ilikuwa ni ahadi ya Serikali na ikatekeleza ahadi ya kuleta makocha hao hivi nani alikuwa anawalipa na walikuwa wanalipwa Tsh. ngapi na je fedha walizokuwa wakilipwa zilitoka wapi?
2. Wakati wa ujio wa makocha hao TFF walipewa taarifa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama hao makocha, maana tukiangalia kwa Maximo kwa sasa hayupo na hakuna anacholidai taifa hili.
3. Hii pia inanipa wasiwasi na Ahadi za Rais inawezekana haweki kumbukumbu zake wakati anapoongea na inawezekana leo hii akiulizwa juu ya ahadi hii anaweza kukana kuwa hakuitoa.
** Kutokana ka kufilisiwa huko inasemekana inawezekana Round ya pili ya ligi kuu ikachelewa kuanza kwani fedha walizochukua ni zile Nauli za Timu zilizotolewa na wadhamini wa Ligi KUU.
na hata kama serikali ndio inapaswa kulipa ni kwa kuisaidia TFF, hivyo TFF nendeni serikalini muwaeleze wawape hiyo pesa mwalipe TRA.Yote unayoongea juu ya udhaifu wa TFF nayakubali, lakini suala langu ni Hao makocha waliokuja kwa ahadi ya JK je TFF walitaarifwa kuwa wanatakiwa kuwalipia gharama na kama ndiyo je ahadi ya JK alikuwa anatuhadaa watanzania?