Ajira Kwanza Vs Elimu Kwanza!

Wewe hata ubunge uliupata Kwa bahati tuuuu
 
Muheshimiwa. Asante sana kwa kuja jukwaani. Tangu 1961 Chama Cha TANU kisha CCM kimekuwa kikiweka kipaumbele kilimo. Utakumbuka kauli mbiu za kwanza Kilimo ni Uti wa mgongo na hapa karibu Kilimo Kwanza. Na wewe umekuja na ajira kwanza na ukikazia kilimo, swali langu ni Jee huoni kuendelea kuwekeza Kwenye kilimo ni kupoteza resource kama manpower.

Pili hawa wakulima kutokana na kukosa elimu wameshindwa kufaidika na kilimo Chao. Wamekuwa wakilaliwa na watu wachache, Jee uoni kwamba elimu ndio engine ya kuzalisha nguvu kazi zenye uweleo wa kuchanganua mambo?

Umegusia swala la viwanda vidogo, Jee ni jinsi gani serikali itaboresha viwanda vidogo vidogo?

Asante sana.
 
Huwezi kukuza uchumi wa taifa la watu wajinga...
 
Hapo bwana hamisi inabidi ujipange kwanza, hiyo slogan yako itakumaliza mapema. Itazua maswali na upinzani mwingi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…