Asante kwa taarifa hii muhimu, nasi pia tunafuatilia kupata habari zaidi. Wiki moja tu iliyopita ajali zimeua zaidi ya watu 14 Mbeya na Kahama. Hakuna muda wa kumtafuta mchawi ni nani kama sisi wenyewe wahanga wakubwa tutaendelea kubweteka, kunyosheana vidole na kungoja mabadiliko. Tuchukue tahadhari Watanzania na tusimamie haki zetu pale inapobidi maana ajali hizi zinatumaliza.