Ajali: Tyre kupasuka

DASA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
1,031
Reaction score
302
Habari members. Nilishawahi kupata ajali ya gari sababu ya tyre kupasuka kati ya chalinze na segera, Tukiwa na gari aina ya Landcruiser (shangingi) ilikuwa tufe, maana ilibidi tukutane uso kwa uso na Lori ambalo lilikuwa linakuja mbele yetu, Lakini sijui nilipata wapi ujasiri wa kung'ang'ania usukani ili tusikutane na hilo Lori sababu gari ilikuwa inavuta upande huo. Nashukuru Mungu ni kioo cha pembeni tu ndicho kilichogonga lile Lori na sisi kupona.

Tangu hapo nimekuwa nikiogopa sana habari ya tyre kupasuka, baadae nikapata habari kwa watu na mafundi mbalimbali kwamba nitumie tubeless tyres, kwamba hizi hata tyre ikipasuka gari haipigi chini upesi ukilinganisha na tyres zenye tube. kutokana na imani hiyo kweli niliamua kufanya hivyo.

Sasa karibu kila siku tunasikia ajali za mabasi zinazosababishwa na tyre kupasuka na watu wengi kupoteza maisha, sasa najiuliza hawatumii tubeless tyres!, au hii imani ya tubeless tyres sio kweli!. Hebu wanaofahamu ukweli wa hii kitu tuelimishane.
 
Hee! wataalam wa sekta hizi humu JF hatuna!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…