Pole sana aisee, ila kheri mmefika salama japo kwa mashaka mashaka.
Nchini kwetu kuna aina kama bili hivi ya wafanya biashara (kusafirisha abiria):-
1. Kuna wale wanaofanya biashara hiyo kwa utaalam (namaanisha professionally). Hawa hata staff wao huwa naona wana maadili na wanaheshimu kazi zao. Mfano wanavaa na kuongea vizuri na hivyo kumfanya abiria kufurahia safari na kutamani wakati mwingine huduma yao.
2. Kundi la pili ni wale wanaofanya biashara ya mazoea (kibabaishaji), mabasi yao ni yale yale ya zamani yenye viwango vya chini (ya kuunga unga). Lakini kibaya zaidi ni huduma zitolewazo ndani ya hayo mabasi, mfano abiria ukifika unagombaniwa ka mpira wa kona, wafanyakazi ni wengi sana (maarufu kama mashanta ambao huambatana na basi na kwa mda mchache tu baada ya safari kuanza hushushwa baada ya kupata malipo yao). Haitoshi, wafanyakazi wao wengi hawana utu kabisa, midomo yao ni michafu na pia hawaeheshimu kazi zao. Usishangae kukuta kuku na watu wengine kwenye vigoda...kazi ipo.