Airtel Rising Stars - Huko Nigeria

dfk-agent

Senior Member
Joined
Aug 5, 2013
Posts
131
Reaction score
163
Habari zenu wana JF?
Nimekuwa nikijaribu kufuatilia maendeleo ya timu yetu ya ARS iliyokwenda huko Nigeria kupitia media mbalimbali online. Cha kusikitisha ni kwamba watu wa media hawajawapatia hawa vijana kipaumbele katika kutuelezea nini kinaendelea huko. Nimegundua kwamba kwa upande wa Tanzania na media zetu, habari zilikuwa zinapatikana siku mbili baada ya tukio. Ninavyojua hadi sasa kupitia mawasiliano Nigeria ni kwamba vijana wetu walicheza nusu fainali jana na Zambia. Sasa sijui kama wametolewa au la. Ila najua Niger wako fainali leo.

Media zetu na wengi wetu tunapenda sana ligi za Ulaya kama EPL, La Liga, Bundesliga etc....inasikitisha kuona blog zetu (na wanaopenda kuTweet mambo ya mpira) zimejaa picha na matokeo ya hizi ligi (ambalo sio tatizo), lakini habari za vijana wetu hazipatikani. Imesikitisha kuona hata website ya Airtel wenyewe pale facebook hawana updates zozote. Ni kama wanafanya sponsor ili wafikie wateja wakijua waafrika wanapenda mpira, lakini wanakuwa inefficient kuripoti maendeleo. Nia yao nini?

Ujumbe wangu ni kwamba, hawa vijana ndio wachezaji wetu wa Taifa Stars huko mbeleni na ni muhimu tuwape kipaumbele sasa. Tusisubiri tu wafikie kiwango cha kuchezea timu zetu kubwa hapo Tanzania (tena wakiwa wamegushi umri) ndio tuone umuhimu wao. Mpira wetu hautaendelea kama hatuwapi kipaumbele hawa vijana.

Nawakilisha. CC Jamal Malinzi, TFF na wadau wote wapenda maendeleo ya soka Tanzania.
 
sio siri nimekua nikitoa machozi ya furaha kwa ajili ya wasichana wetu waliotuletea heshima mana wao ndo washindi. Tz 1 ke 0 matokeo ya mwisho na hii ilikua fainali.
Kwa kifupi tumekua hatushindi hapo mwanzo na hii ikapelekea tusishabikie sana timu zetu.
To me, the girls have surprised the nation by that victory and the boys too made it to the final.
Should this be sustained, i mean frequent victories there will be nothing to stop tanzanians from cheering for their teams.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…