Airtel na vifurushi vya OMG

Complex

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Posts
4,120
Reaction score
4,790
Nimekuwa sielewi mwenendo wa data usage za hivi vifurushi vya OMG kutoka Airtel takriban wiki sasa.

Mara utumiwe sms ya umetumia 90% ya kulifurushi chakk ilhali unakuta hata nusu hujatumia ( hii ni kwa kuangalia both upload na download )

Jana usiku nililala simu ikiwa na MB 300 za data, kuamka asubuhi nikakuta zote zimekwisha na niko disconnected na data. Nilijaribu kufanya followup jinsi nq namna gani MB 300 zimekwisha, nilikosa jibu. Nikachukua uamuzi wa kununua kifurushi kingine cha wiki cha 2500.

Nilipoweka salio, na kujiunga nikatumiwa flash msg kuwa nimefanikiwa. Huku data nikawa bado sipati. Kuangalia salio naona limekatawa, kuangalia salio la data stil ikawa 0 MB. Nikachukua uamuzi wa kuwapigia simu Airtel, mara ya kwanza mhudumu akaniambia kuwa amelipeleka tatizo sehemu husika nisubirie masaa matatu pasipo jibu, baada ya masaa matatu kupita nikapiga tena, nikakutana na mhudumu mwingine.

Huyu alikuwa anaonekana hafahamu hata anachokiongea na akawa anaforce kuwa pesa imeliwa na data kabla sijajiung. Hakutaka kuelewa point yangu ya flash message kuwa nilirudishiwa sms ya kufanikiwa, baada ya mabishano marefu akanikatia simu.

Nikapiga tena, nikaambiwa nisubiri masaa matatu tena. Mpaka sasa hakuna jibu. Ilipofika jioni nikaamua kununua kifurushi cha siku, maana maisha bila data ni dissaster. Cha kushangaza jioni hii naona MB zangu 300 za jana zimerejeshwa na salio nililonunua kwa siku lipo bado.

Kuna wadau mshakumbwa na tatizo kama hili.? Maana huku ni kutiana hasara pasipo sababu ya msingi. Inamaana airtel wameanza wizi wa data kama Tigo na voda.?
 
Pakukimbilia ni wapi??? Anyway...airtel nliwatumia..sikuona hiyo shida japo nimeshaiskia wa wenzangu!!! Kwa sasa natumia voda naona nao hawako vibaya...ila kwann usijarib zantel kama eneo lako linakubali 3g (town) ??
 

Iwe simu au Modem ukiangalia statistics majibu yanakua hapo

Inawezekana kweli wanatuibia lakini somo kwa wengine ni kwamba wafatilie statitiscs
 

Attachments

  • daily.JPG
    62.4 KB · Views: 200
yaani ni bora uwe na mb20 za voda kuliko mb300 za airtel. ipo slow sana na pia nikiwa salio sjui huwa wanalikata vipi unajikuta huna kitu.kwa hiyo ninachofanya ni kununua kifurushi cha hela yote iliyopo kwenye salio kabla hawajaniibia
 
Iwe simu au Modem ukiangalia statistics majibu yanakua hapo

Inawezekana kweli wanatuibia lakini somo kwa wengine ni kwamba wafatilie statitiscs

Mkuu majibu yote ninayo kuwa data ninayotumia haiendani na makato ya data katika akiba yangu ya data. Nimelichunguza hili kwa wiki sasa. Nimeweka hii post ili wadau tufuatilie na kwa waliofuatilia watoe shuhuda juu ya makato ya data kama yanaendana matumizi ama laa. ( Isije ikawa kwangu tuu)

Kuhusu kasi ya vifurushi kwangu mimi iko fair kwa maeneo ninayokaa. Toka wafanye swap ya erricson BTS kwenda Huawei BTS naona hali ni nzuri kidogo, kwa maeneo nilipo Speed inagonga mpaka around 800 KBps huku dashboard ikisoma mpaka above 6Mbps. Ishu inakuja hapo katika makato yao. Yaani toka wamebadili tariffs za OMG kwangu mimi naona mazingaombwe yamezidi kwa data kuisha pasipo matumizi stahiki.

Nimeweka uzi huu nikiamini kuna watu wao na wahusika, wanapita humu na waipate taarifa kuwa tumeshtukia mchezo wao ni jukumu lao waache na Kama ni bahati mbaya wafix tatizo.

Wasipofix hili tatizo mimi binafsi nitaanzisha kampeni ya kuhama data ya airtel kwa watu wanaonizunguka kwani nina watu si chini ya 20 ambao nikirecommend kwao watumie mtandao fulani kwa data wananisikiliza. Na wao wana watu wao, the chain goes. Kama nilivyowatoa voda kuja airtel ( kwa speed kupungua inapofika limit), ndivyo nitawashawishi kutoka airtel kwenda Zantel i think ( Bado nafanya research ya tariffs zao na service zao )
 
Kuhusu kuibiwa Data ni suala la kawaida sana kwa hii mitandao yetu yote, kwani vyombo vyetu vya usimamizi vimeshindwa kusimamia makampuni yote ya simu ndio maana wanatuibia mpaka basi. Kuhama sio issue kama wasemavyo wahenga kukimbia tatizo sio kutatua!!!! Kama watu wameliona hili waende wakaripoti TCRA ili nao wafanye kazi yao sio kula bata kusubiria mishahara kama ATC. WATANZANIA TUNAIBIWA SANA NA HII MITANDAO NA TUMENYAMAZA KISA TUNAONA PESA NI NDOGO LAKINI WAO WANAMAKE BINGO ILE MBAYA. TUAMKE ILI TUFAIDIKE NA HIZO FIBRE ZA CHINI YA BAHARI SIJUI NINI...!!! Hii Tanzania kila mahali majanga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…