Airtel mmeamua kutusaliti?

Yaani wameniboa kuliko maelezo nilikwa nanunua kifurushi 19999 napata dk 650 nimeshangaa leo napata dk450 wiZi mtupu tuhamie mtandao gani zantel vp?
 
Tanzania ni walalamishi lakini wakiambiwa wachukue hatua ni waoga. Umewahi kujiuliza sms ngapi makampuni ya simu yanakutumia bila ridhaa yako na wanakukata fedha bila ridhaa yako? hivi kila callertune unayowekewa na haya makampuni unakuwa umeichagua wewe? mchungaji mmoja alikuwa analalamika airtel wamemwekea kaswida na bado wanamkata! wanasheria wetu mpo!!!! achaneni na mambo ya siasa wasaidieni wananchi kwa mambo kama haya!
 
Mkuu mie si mtaalamu wa haya mambo, ila inaonekana ni idea nzuri japo sijui namna ya kufanya kama wewe unavyofanya, ingawa mie huwa nina-tether kwenye laptop full time,
 
jamani tumelalamika vya kutosha hawa jamaa bila kuwachukulia hatua au kuwaexpose hawataacha mchezo wao mchafu kesho naenda kulay fomal complain kwani nimeongeza salio naagalia balance naona wamekata bila kutumia huyo makmba ni zuzu kazi kuingilia wizara za wenzake wakati yake tunamshinda niliwahi kuwalalamikia kabla lakini safari hii nitaenda nao hadi mwisho
 
VAT jamani.airtel ipo cheap sana hamjagundua tuu.mmesahau kama kuna kodi iliyotangazwa....napita tu jamani
 
VAT jamani.airtel ipo cheap sana hamjagundua tuu.mmesahau kama kuna kodi iliyotangazwa....napita tu jamani

Mkuu hatukatai ila jiulize poromoko la 2gb mpaka 500mb ni kubwa mno ni bora wangepunguza ma sms yao maana watu siku hizi ni whatsap na watu wamenunua smart phone mpaka za elfu themanini na haya makampuni yaliwashawishi watu kununua smart phone sasa leo kifurush wanabana. Wakihujumiwa wanalalamika
 
Walitudanganya kwa kwa airtel yatosha,sasa imekuwa airtel haitoshi,sasa line ya airtel naweka kapuni,
 
Mie nimejiunga kwa bk 3 nikaambulia dk 75, badala ya 100, hovyo kabisa.
 
nilifikiri labda mi nimejichanganya, nlikuwa nachukua kifurushi cha wiki 1999/= unapata dk 60 kama sikosei, juzi naingia naona dk 40 nikafikiri labda siwazi sawa sawa. kama kuna mabadiliko kinachowafanya wasiwahabarishe wateja ili wanunue wakijua mabadiliko ya gharama ni kitu gani zaidi ya wizi?
 
Jamani ile minikabang ya 2000 unazopata dk 65 kwa wiki, je ni kwa kupiga mitandao yote?
 
Airtel wamegeuka mfano kifurushi cha 1999 kilikuwa dk 60 sasa ni dk 40 tu na MB zimeepungua.
haya mashirika ya simu yanatuchezea sana akili zetu. Yaani lazima mtu ujiunge na Bundle ndipo upate nafuu la sivyo wewe ni wa kuumia tu! Mamlaka ya mawasiliano ilijigamba mwanzoni mwa mwaka jana kuweka viwango vya kupiga simu kwa mitandao yote hakuna llote lililofanyika. Walaji kila seehemu tunapelekeshwa ukienda kwenye elimu hayo hayo. kwenye umeme, ving'amuzi, simu, TRA na EFD zao vurugu tupu. hawa watoa maamuzi wana degedege au wanaota?
 
mimi mwenyewe nimewahama nimerudi zangu tigo
 
Embu ngoja nikawaangalie zantel!!!
 
kuna kale kakodi ka miezi 6 serikali imekaweka hapo...tuvumiliane tu wananchi.. kuna Bunge la Katiba na uchaguzi ndio huu...tufunge mikanda
 
kweli kabisa jamani mim nilikua voda ikafika mahala hasa december mwaka jana mtandao ulivokua unasumbua nkahamia airtel nkaema mambo si haya basi.zile 2gb za net ndo zilinidatisha nkijiunga ile ya elf 6 kasoro 1.sasa nashangaa kweli wamepunguza dk na. mb sasa hayo masms 1000 nani ana muda nayo? imebidi nisogee tena tigo naona angalao.voda na airtel sijui lini mwisho nimeweka vocha waendelee tu wee hatimaye tutajiunga za 500 mpaka chini ya hapo maana naona wamechoka hizo elf 6 zetu sasa wanataka mia tanotano.ambapo nikijiunga ya 450 kwa. kila siku kwa wiki hata elf 4 haifiki.hasara kwao
 


NAUNGA MKONO HOJA, Naona airtel wanapepesa macho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…