Aikimbia CHADEMA baada ya kutapeliwa

Mr Chin

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
4,625
Reaction score
1,024
​
Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kata ya Igowole, Josephat Soda akikabidhi bendera ya chama hicho kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya yeye na wenzie 26 kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
​
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akimkabidhi kadi ya CCM, Josephat Soda baada ya kutanga kujiunga na CCM katika mkutano huo.
​
Josephat Soda akielezea jinsi alivyoamua kuondoka Chadema na kujiunga na CCM, ambapo alisema amechoka na chama kilichosheheni uongo na ulaghai, ambapo alidai viongozi wa Chadema walitoa maagizo kuwa akope fedha za kujengea Mnara wa mwandishi wa habari Marehemu David Mwangosi, aliyeuawa wakati wa vurugu za CHADEMA na Polisi katika Mji wa Nyololo, ambapo walimuahidi kumtumia fedha zilizotumika kujenga mnara huo ahadi ambayo hadi sasa hawajaitimiza na anadaiwa na muuza simenti na muuza saruji alikokopa. Kutokana na maelezo yako, CCM imeamua kulipa madeni yote aliyokuwa akidaiwa ili kutunza heshima.
​
Wanachama wa CCM wakiwemo wale wapya kutoka Chadema, wakiapa kiapo cha utii cha CCM baada ya kukabidhiwa kadi wakati wa mkutano huo
 
Namba unayopiga inaongea na simu nyingine.
 
Huu ndo ushahidi wa kuwa Chadema hawatoi pesa kujiunga wala kuja kwenye mkutano
 
Njaa kitu kingine waliyemuua huyo mwandishi ni akina nani?
 
Kama ni Igowole wala sishangai sana, uelewa wa watu wa Iringa juu ya vyama vya upinzani ni mdogo sana!

Hata hivyo ni maajabu sana, wakati CHADEMA ikisomba watu km kina Kingunge, nyie mnahangaika na Katibu wa CHADEMA ngazi ya kata! Ama kweli hali ni mbaya kwenu!
 

Vikongwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…