Nianze kwa kurudia kutoa pole kwa makocha,familia ndugu na jamaa wa marehemu Marsh.Mchango wa Marsh katika maendeleo ya mpira kuanzia akiwa mchezaji hadi kocha ni wa kuenzi daima.
TFF kwa kushirikiana na makocha tuliuchukua msiba huu ukawa wa kwetu.Zaidi sipendi kuyaongelea maisha binafsi ya marehwmu maana katika hali ya kawaida familia ya marehemu ndio ingetuongoza katika kutoa maamuzi muhimu kuhusu taratibu za msiba,usafirishaji wa mwili na maziko.Ilibidi tuchukue maamuzi ambayo kusema kweli kiutaratibu na kwa mila zetu za kiafrika hatukustahili kuyachukua.
Usafiri wa kupeleka mwili mikoani kwa Coaster ni wa kawaida kabisa hata kwa familia zenye uwezo.Mimi mwenyewe nimesafirisha marehemu wengi ndugu zangu kwenda Bukoba kwa Coaster,it is a normal practice.Kutoka Dar kupeleka maiti Moshi Iringa Songea Tanga Mwanza nk kwa Coaster ndio utaratibu wa kawaida kabisa.Uzuri wa Coaster ni kuwa ndugu jamaa na marafiki nao wanapanda gari hilo hilo na marehemu,wanamuimbia mapambio na kumuaga njia nzima.Ubaya ungekuwa kama TFF tunge abandon maiti Muhimbili.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF wamechangia msiba huu,makocha wamechangia msiba huu.TFF imewakilishwa mazikoni na mjumbe wa Kamati ya utendaji Lufano,Mkurugenzi Madadi na uongozi wa chama cha mpira Mkoa wa Mwanza.
Tumuache mwenzetu apumzike kwa amani,tusiingize siasa za mpira kwenye jambo zito kama hili.
RIP Marsh