Utapata tu, wapo sema waoga wa interview halafu wengi wanapenda kazi za kukaa ofisini tu, kama za kutoka wanapenda wawe na usafiri au kampuni iwe na usafiri. Nami nimepata shida kumpata marketing officer, ikanibidi awe anatumia gari yangu binafsi (kampuni bado haina lake), siku nimempa aka consult wateja fulani akaenda kutembelea ndugu zake, amerudi namwuliza ripoti anasema wote hao hakuwakuta, japo niliwapigia simu kuwa kuna afisa wangu anakuja bila yeye kujua hivyo. Nikawapigia simu mbele yake, akaumbuka!! He is no longer with my company.