WanaJF,
Mfalme wa rhymes nchini, ajulikanae kama afande sele, ametoa ya moyoni baada ya kuona watu wengi wanamsakama kuhusu maisha yake ya usanii kwa tuhuma kuwa ni mvuta mmea tu, hivyo kwa tabia hiyo astahili kuwa mwakilishi wa wananchi!
Afande sele ambae hapo awali alikuwa moja kati ya wanachama wenye majina makubwa CHADEMA, ameamua kutoa ya moyoni na kuuweka umma wa Watanzania wazi juu ya tabia za wabunge wa CHADEMA ambazo wengi wetu hatuzijui.
Afande Sele ameeleza kuwa kipindi yupo CHADEMA alikuwa anatumiwa ipasavyo na wabunge wa CHADEMA pamoja na makamanda wengine kuwapatia 'mmea' au kwa jina lingine bangi. Pamoja na kufunguka huko lakini hakuwa tayari kutaja majina ya wabunge hao watumia 'mmea' ingawa alitoa idadi yao kuwa wapo 9 na wote ni wanaume.
Aidha, afande Sele amemshauri Dr Slaa kuwa badala ya kupigania gongo ni wakati sasa chama chake kianzishe ajenda za kuiwezesha bangi kuruhusiwa kisheria kwa kuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa mtumiaji ukiachilia mbali uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Source: Clouds FM