Afande Sele: Wabunge wengi wa Tanzania wanavuta mmea

MKONGA

JF-Expert Member
Feb 19, 2015
667
453
Afande Sele kafunguka kupitia ‪#‎YouHeard‬ ya Power Breakfast Clouds Fm na kusema kuwa wabunge wengi wa Tanzania wanamfuata na kumuomba 'Mmea' wakidhania kuwa yeye bado anavuta. "Mimi huwa nawaelekeza kwa washikaji zangu nnaowajua kisha wao wanaenda kuchukua"

Pia amedai kuwa kuna nchi zilizoendelea na zimepitisha matumizi ya 'mmea' na zinaingiza ushuru wa kutosha kupitia mimea hiyo.
 
Banging Mbona Jani la kawaida tu la kiafrika ...miaka yote iPo lakini haijauwa Mtu au kumfanya mdhaifu kama unga

Bangi Ina risk chache kuliko sigara
 
1. Sugu

2. Lema

3. Msigwa

4. Mdee

n.k

Amesema 10 mbona hao wanne tu, ongeza list. Usitumie kifupisho n.k, maana yake nashindwa kufikiria, hicho kifupisho hakitakiwi hata kwenye mtihani. Wametafsiri kutoka neno la kiingereza etc, end of my thinking capacity.

Kutumia kifupisho hicho unatupa shida wenzako, malizia kabisa wataje tu.
 
WanaJF,

Mfalme wa rhymes nchini, ajulikanae kama afande sele, ametoa ya moyoni baada ya kuona watu wengi wanamsakama kuhusu maisha yake ya usanii kwa tuhuma kuwa ni mvuta mmea (bangi) tu, hivyo kwa tabia hiyo astahili kuwa mwakilishi wa wananchi!

Afande sele ambae hapo awali alikuwa moja kati ya wanachama wenye majina makubwa CHADEMA, ameamua kutoa ya moyoni na kuuweka umma wa Watanzania wazi juu ya tabia za wabunge wa CHADEMA ambazo wengi wetu hatuzijui.

Afande Sele ameeleza kuwa kipindi yupo CHADEMA alikuwa anatumiwa ipasavyo na wabunge wa CHADEMA pamoja na makamanda wengine kuwapatia 'mmea' au kwa jina lingine bangi. Pamoja na kufunguka huko lakini hakuwa tayari kutaja majina ya wabunge hao watumia 'mmea' ingawa alitoa idadi yao kuwa wapo 9 na wote ni wanaume.

Afande Sele aliongezea "wabunge wengi wa CHADEMA wanamfuata na kumuomba 'Mmea' wakidhania kuwa yeye bado anavuta, kwa sasa mimi uwa nawaelekeza kwa washikaji zangu nnaowajua kisha wao wanaenda kuchukua"

Aidha, afande Sele amemshauri Dr Slaa kuwa badala ya kupigania gongo ni wakati sasa chama chake kianzishe ajenda za kuiwezesha bangi kuruhusiwa kisheria kwa kuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa mtumiaji ukiachilia mbali uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Source: Clouds FM
 
WanaJF,

Mfalme wa rhymes nchini, ajulikanae kama afande sele, ametoa ya moyoni baada ya kuona watu wengi wanamsakama kuhusu maisha yake ya usanii kwa tuhuma kuwa ni mvuta mmea tu, hivyo kwa tabia hiyo astahili kuwa mwakilishi wa wananchi!

Afande sele ambae hapo awali alikuwa moja kati ya wanachama wenye majina makubwa CHADEMA, ameamua kutoa ya moyoni na kuuweka umma wa Watanzania wazi juu ya tabia za wabunge wa CHADEMA ambazo wengi wetu hatuzijui.

Afande Sele ameeleza kuwa kipindi yupo CHADEMA alikuwa anatumiwa ipasavyo na wabunge wa CHADEMA pamoja na makamanda wengine kuwapatia 'mmea' au kwa jina lingine bangi. Pamoja na kufunguka huko lakini hakuwa tayari kutaja majina ya wabunge hao watumia 'mmea' ingawa alitoa idadi yao kuwa wapo 9 na wote ni wanaume.

Aidha, afande Sele amemshauri Dr Slaa kuwa badala ya kupigania gongo ni wakati sasa chama chake kianzishe ajenda za kuiwezesha bangi kuruhusiwa kisheria kwa kuwa ni mmea wenye faida nyingi kwa mwili wa mtumiaji ukiachilia mbali uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Source: Clouds FM

yaani hata unachoandika hakieleweki
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom