Achinja mkewe, naye ajiua

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,185
Reaction score
64,574
MWANAMUME mwenye umri wa miaka 30 amejinyonga kwa kamba ya katani hadi kufa baada ya kumuua mkewe kwa kumchinja shingo kwa kisu kutokana na kile alichodai kuwa ni kudharauliwa na mkewe.


Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela ambaye amemtaja mwanamume huyo kuwa ni Ramadhani Abdallah, mkulima na mkazi wa kijiji cha Makale katika kata ya Mitundu, tarafa ya Itigi wilayani Manyoni anayedaiwa kumuua mkewe, Amina Waziri (30).


Katika tukio hilo la Oktoba 20 saa 9.15 alasiri, Kamanda Kamwela alidai kuwa Ramadhani baada ya kuhakikisha kuwa mke wake amekufa, alichukua kamba ya katani na kujitundika kwenye moja ya kenchi ya nyumba yao na kujinyonga hadi kufa.


“Kabla ya kujinyonga, Ramadhani aliacha ujumbe mfupi usemao kuwa amechukua hatua hiyo ya kukatisha maisha yake na mke wake kutokana na mkewe huyo kushirikiana na kaka zake kumuoza binti yake wa kufikia bila ridhaa yake,” alisema Kamanda Kamwela.Mia

Chanzo:Habarileo
 
Tatizo hapa ni frustration za kimaisha a.k.a ukosefu wa hela.
 
Aiseee binti wa kufikia ndio jamaa kajiua??!!
Alimlea tangu utoto au??!
 
kweli hela ni shetani alitaka alipwe yeye mahari si bure
 
Wakuu hamuoni equal ratio ya umri wao nayo inaweza kuwa imechangia? japo sababu aliyotoa ni ya kipuuzi lakini uwiano sawa wa umri kwa mwanamke na mwanaume au mke kuwa mkubwa kuliko mume kunaweza kuwa tatizo la kutosikilizana.
Au mnasemaje wadau?
 
Mh!!!
Mtoto huyo wa kufikia kuozwa na wajomba zake imemuuma hivyo! Bora kajiua maana angeulizwa kama alikuwa na mahusiano naye zaidi ya Baba na mwana.
 
Sasa mke ana umri wa miaka 30 amewezaje kuwa na mtoto wa kuweza kuolewa?sasa huyo mwanamke wa miaka 30 nae anakuwa mkwe?duh..
 
Aiseee binti wa kufikia ndio jamaa kajiua??!!
Alimlea tangu utoto au??!

Hata kama alimlea,kama majina yao yana reflect imani yao basi ni halali bint huyo kuozwa na wajomba.
Walikuwa na yao hao hawajayasema tu.
 
Mh!!!
Mtoto huyo wa kufikia kuozwa na wajomba zake imemuuma hivyo! Bora kajiua maana angeulizwa kama alikuwa na mahusiano naye zaidi ya Baba na mwana.

Haa ha ha...Baba aliondolewa chakula yake...
 
yawezekana jamaa alikuwa anadonoa mtoto wake huyo wa kufikia. haiwezekani achukue maamuzi magumu kiasi hicho
 
kuna la ziada may be ...

au alikuwa anamgegeda hyu binti....
 
Huo ujumbe ni wake kweli?!!!

Hainingii akilini kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…