‘utacheka ufe!’

laigwenan

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Posts
325
Reaction score
80
Ndugu wana wa Tanzania HABARI Hivi ni Vichekesho sana hebu Tazama
Pamoja na kuwa Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania, Pia Kilimo kuchangia takriban nusu ya pato zima la taifa na robo tatu ya bidhaa zote zinazouzwa nchi za nje, Pia Pamoja na Kilimo kutoa chakula, na vile vile kutoa ajira kwa asilimia 80 ya WatanzaniaSerekali chini ya CCM kimesindwa kutenga japo alisilimia 10 ya Budget yake kwenye kilimo Hakika kwangu mimi hivi ni vichekesho , Na najiuliza Hivi ni kweli Kilimo ni Uti wa Mgongo au ni Hadithi tu!.
Sehemu kubwa ya kilimo Tanzania ni cha wakulima wadogo-wadogo ambao mashamba yao yana ukubwa wa kati ya hekta 0.9 na hekta 3.0 kila moja. Karibu asilimia 70 ya ardhi ya ukulima wa mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono hii ni kichekesho sana kwenye karne



asilimia 20 kwa kutumia maksai na asilimia 10 kwa kutumia trekta. Kilimo cha Tanzania ni cha kutegemea mvua. Uzalishaji wa mazao ya chakula ndio unaoongoza katika uchumi wa Kilimo. Hekta milioni 5.1 zinalimwa nchi nzima kila mwaka,Msomi mmoja alisema kumtetea Mkulima mdogo hapa Tanzania Kunahitaji Ujasiri wa ‘Kiwendawazimu’ na alimaanisha ni vigumu kuendelea hapa Tanzania kwa kutegemea jembe la Mkono na Wa Tanzania tutaendelea kuzaliwa na kufa MASIKINI.Nchi ya Misri ni ya Jangwa Kwa sehemu kubwa lakini ni wazalishaji wa kubwa wa Mpunga hapa Afrika na inatumia Hekta 500,000 tu kumwagilia Mpunga na serekali ndiye Mzalishaji Mkuu.Ninacho kijua nikwamba iwapo uwekezaji wa kutosha ungefanyika kwa kiwango cha angalau asilimia 50 tu kwenye Mashamba ya Mpunga ya Dakawa , Mbarali, na Bonde la Rufiji, Tanzania ingekuwa wauzaji na wasambazaji nambari moja wa Mchele AFRIKA lakini kinacho fanyika Kwangu ni Vichekesho eti Tanzania inaagiza Mchele Nchi za nje Kwa kweli haya ni Maajabu na Sijui kwa kweli Watanzania wanao ishi Misri wanajisikiaje. Serekali kupitia Wizara ya kilimo ,Wizara ya Ajira na Vijana ,JKT, na Magereza Wange simamia Uzalishaji wa Mahindi na Mpunga na Tanzania ingekuwa ‘Ghala la Afrika’ kwa kweli sera za kilimo Tanzania zingefanikiwa kwa Vitendo lakini kinacho fanyika chini ya CCM ni Maigizo eti serekali inanunua Chakula badala ya kulima Hivi kweli Kilimo ni Uti wa Mgongo au ni Utani tuu! Hivi ni kweli serekali haija lima hata eka moja Huko Morogoro na Songea au watu wanasema tu ! kama hii ndiyo hali Halisi basi CCM wameshindwa kazi na wapumzike! Tuna hitaji serekali inayo weza kuingia shambani na Kulima kwa vitendo na kutumia njia za kisasa kabisa sio kutuletea sera zisizo na Mashiko.






 
Umeongea mambo ya msingi lakini kichwa cha habari hakivutii.
 
Hii ndiyo Tanzania , maneno ni mengi kuliko vitendo !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…