Inahitaji mtu kuwa jasiri kuongea yaliyokukuta huku ukijua ulirekodiwa video ukiwa uchi huku ukidhalilishwa kingono na kutishiwa video zako kuvuja ukifungua mdomo.
Safari ya kuitafuta haki hujaa maumivu na aibu, watanzania wengi huona bora kuficha aibu kuliko kupigania haki.
Binadamu ni akili inayoishi ndani ya mwili! Na akili inahitaji elimu bora ili kuikomaza vizuri. Siasa na serikali ni mifumo ya kijanja janja sana. Inahitajika akili iliyokomaa kuweza kukabiliana nayo!
Maandamano yanayofanyika nchini Kenya hayana viongozi wa kisiasa! Ni vijana walioelimisha...