Sheikh wa Mkoa wa Singida, Sheikh Issa Nassoro, amewataka viongozi wa dini nchini kuwa waaminifu na kuacha kutumia nafasi zao kuchochea taharuki au migogoro ya kisiasa, akibainisha kuwa baadhi yao wamekuwa wakihusika katika matukio ya udanganyifu ikiwemo kujiteka wao wenyewe kwa maslahi binafsi...