Najiuliza tu, hayo mamia ya mamilioni kayatoa wapi wakati juzi tu tulikuwa tunamchangia apate usafiri? Na akaandamana na watu wengi sana, wengine wamelipiwa nauli kutoka mikoani na kulazwa kwenye hoteli zenye fahari kuu jijini Dar es salaam?
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe kubwa, hususan harusi, inavyozidi kushika kasi hapa nchini. Kinachoshangaza zaidi ni kwamba ule wigo wa kuomba michango sasa umepanuka kiasi cha kutisha. Leo hii, mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza kukuomba...