Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeunga mkono na kufungua kesi ya kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania (Kanda Kuu Dodoma) kupinga uhalali wa matumizi ya adhabu ya viboko shuleni. Kesi hii imewasilishwa kwa niaba ya Samwel Maduhu Mangu, mlezi wa marehemu Mhoja Wilson Maduhu...