kwahiyo tatizo ni mimi? kwanini hujaona tatizo zaidi ya mimi kuwa tatizo? je nikikwambia hata hiyo laki 8 yake ameanza kuhudumia miezi kadhaa iliyopita baada ya kukuta wali maharage kila siku bado utasema tatizo ni mimi?
unanikandamiza kwa kuwa nimesema kipato changu mkuu? nimejibu hapo juu shule ni ya kanisa na alishauri yeye mtoto aende shule ya kanisa. hapo tatizo ni mimi kivipi?
ndio kwetu mimi ndo tegemezi tupo wanne lakini mimi ndo tegemezi. kuhusu mchango tulifungua UTT account mimi nilichanga miezi yote 12 ya mwaka 2024 kulingana na kiwango tulichokubaliana lakini yeye aliweka mwezi mmoja nikimkumbusha anasema niachane na hayo mambo.
Hapa unakosea mkuu. sijawahi mforce kufanya kitu tunafanya kwa uwezo wake na sio uwezo wangu. hata hiyo shule alichagua yeye na sio mimi. kwa kifupi nyumba imetawaliwa na mume wangu mimi nipo chini yake sijawahi kujikweza hata siku moja.
ndio ila kama umesoma kuna mtu nimemjibu kuwa mshahara wangu ninahudumia wazazi wangu pia ninakatwa bima ya wazazi na mkwe kinachobaki ndo kinawekwa mezani kama familia. Pili biashara nilichukua mkopo kazini ambapo pia nakatwa na nilimshirikisha. nimempa wazo la biashara ila mtaji akaazime kwa...
Asante kwa ushauri. Kukopa bank hataki na hata kukopa kazini kwao hataki anasema hataki kujiingiza kwenye mikopo. sijaomba ushauri kwa yoyote nahisi nitadhalilisha familia.
Nimesema machache tu mkuu. Mshahara wangu ndo unalisha wazazi wangu , kulipa bills zao na ninakatwa bima yao na ya mkwe pia kwahiyo kinabaki kiasi kidogo cha fedha ambacho ndo tunatumia kwa pamoja na yake kwa familia.
Habari great thinkers.
Nimekuwa msomaji kwa muda mrefu sana humu, ila imenilazimu nijiunge ili nitoe nilichonacho maana ninahisi kuzidiwa moyoni sipati kulala usiku. Nahitaji ushauri.
Mimi ni mama wa mtoto mmoja wa miaka 6, nimeolewa miaka 8 iliyopita, nyumba tunayoishi tumepewa na mama mkwe...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.