You are using an out of date browser. It may not display this or other websites correctly. You should upgrade or use an alternative browser.
Amos Muhagachi
Nafikiria sana juu ya mabadiliko ya kisiasa nchini Tanzania na hasa wanasiasa kuhama vyama toka chama A kwenda chama C hii ni haki ya kikatiba na inapaswa kuheshimiwa kwa mjibu wa Katiba ya Tanzania.
Maswali wamenunuliwa yanaleta ukakasi wa kisiasa katika mstakabili wa kisiasa hapa nchini mwetu.
Tangu enzi za Mh.Mrema kuihama CCM na baadaye wakafuata mawaziri wakuu wastaafu Mh.Lowasa, Mh.Sumaye na hivi karibu Mh.Nyalandu sijui hawa nao walinunuliwa kiasi gani cha fedha maana hoja nazozisikia kutoka upande wa Chadema ni kuwa wabunge na madiwani wanao hama kutoka chadema kujiunga na CCM wamenunuliwa hii inaanza kutujengea imani kuwa kweli huenda hawa wenzetu wanaijua biashara hii ya kukunua wanasiasa au hata kukunua chama.
Mfano Mh.Lema aliisha kuwa katika chama cha TLP, NCCR-MAGEUZI na hatimaye sasa yupo Chadema alikuwa akinunuliwa kwa bei gani ya kiasi gani?
Mimi nadhani watu wapewe uhuru wa kuamua chama gani aende au chama kipi atoke ili mradi tu asitumie kauli za uongo na kashfa ya kule alikotoka.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.