Zuku kama Tanesco wakati wote ni no signal

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,867
8,282
Wadau hebu nisaidieni kwa maana nimeshachoka hawa mafundi wa Zuku kila leo nawaita kurekibisha tatizo la no signal mpaka nimewachoka kwangu Zuku ni kama Tanesco leo nipate signal baada ya dakika kidogo hakuna signal,nilikuwa na wasiwasi na ufungaji wa dish lakini mbona kuna wakati napati channel halafu hupotea tena baada ya muda si mrefu,hapo nyuma kulikuwa hakuna tatizo lakini kuanzia April ndio hayo mambo yameanza,mwezi May ndio usiseme hela yangu imeenda buure,fundi wao alikuja akarekebisha baada ya siku chache tatizo ndio likazidi,jana ndio niliona kidogo baada ikawa byebye mpaka saa hizi ,kama kuna mdau ambaye anaweza nipa ufumbuzi wa hili tatizo naomba anijuze,nimeboreka kweli kweli hadi nataka nirudi StarTimes hawa sikuwa na tatizo nao ingawa niliondoka sababu kila channel ni michina yao
 
mkuu hilo tatizo linatokea kila mara au kwa miezi mi3 au mi4 maana ninampango wa kupitia Moroko leo ninunue. Sasa kama hali yenyewe ndio hiyo unanitisha kwa kweli.
 
Walitoa matangazo kuwa wameongeza channels kama vile Man U tv, Arsenal tv,Je,channels hizo zipo kweli? na je,zinaonesha mechi za EPL live?
Nisaidieni kwa hilo.
 
Back
Top Bottom