Zombe Aishitaki serikali, adai 5.2 Billion!!

Zombe aidai Serikali fidia ya Sh5.2bilioni Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 21:42

James Magai na Tausi Ally
ALIYEKUWA mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teski wa Manzese, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe juzi ameishtaki serikali akiiomba mahakama iiamuru imlipe fidia ya Sh5.2bilioni.

Zombe alikamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 9, 2006 na kuunganishwa na askari wenzake wengine ambao jumla yao walikuwa 13 wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya Sabinus Chigumbi (Jongo), Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu, katika msitu wa Pande wilayani Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Januari 14 mwaka 2006. Hata hivyo, Agosti 17, 2009 watuhumiwa wote waliachiwa huru na Mahakama Kuu Dar es Salaam, mbele ya Jaji Salum Massati baada ya kuonekana kutokuwa na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.

Kiasi hicho anachodai Zombe ni fidia ya madhara ya jumla na Sh200 milioni ikiwa ni fidia kwa adhabu ya kumweka ndani, riba pamoja na gharama za kesi hiyo.Wakati Zombe akifungua kesi hiyo ya madai, Serikali imekata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu iliyomwachia huru yeye na wenzake wanane ambayo bado haijatolewa uamuzi wala kusikilizwa.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyoandaliwa na Wakili Mwandamizi, Richard Rweyongeza, Zombe anadai alipwe fidia ya kiasi hicho au kingine ambacho Mahakama itaona kifaa kutokana na madhara aliyopata kutokana na kesi hiyo kwa kosa la kukamatwa na kumshtaki kwa tuhuma hizo akidai kuwa ni ukiukwaji wa sheria.

Katika kesi hiyo iliyosajiliwa kwa namba 35 ya mwaka 2011, mbali na kuomba mahakama hiyo iiamuru Serikali imlipe fidia, Zombe pia anaomba hiyo itamke kuwa alikamatwa na kushtakiwa kinyume cha sheria na ni batili.
Zombe anadai kuwa kabla ya kukamatwa alikuwa amehamishiwa katika Mkoa wa Rukwa na alirejeshwa Makao Makuu ya Polisi siku 14 baada ya kuwa ameripoti katika kituo chake hicho kipya cha kazi. Anadai kuwa siku hiyo kabla ya kukamatwa na kupandishwa kizimbani aliitwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ambaye alimjulisha kuwa anatakiwa kuunganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo.

Anadai kuwa baada ya taarifa hizo alichukuliwa ghafla na kupelekwa mahakamani ambako Hakimu Mkazi Mkuu alikuwa akimsubiri na kwamba mara baada ya kusomewa mashtaka yake alipelekwa katika Gereza la Ukonga mahali ambako kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kumpokea.
Lakini analalamika kuwa baada ya kukamatwa, polisi walikuwa na wajibu wa kumwuliza kama alikuwa na jambo lolote la kusema ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu maelezo yake. Hati hiyo inadai kuwa kinyume chake, kukamatwa kwake kulifanyika kinyume cha wajibu huo, yaani bila kusikilizwa mlalamikaji kama alikuwa na cha kusema kuhusu ushiriki wake katika tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa hati hiyo, wakati akiwa mahabusu katika Gereza la Ukonga na baadaye Keko, Zombe aliwasilisha malalamiko yake kwa waziri mwenye dhamana ya masuala ya kisheria jinsi alivyotendewa lakini hakupata mwitiko wowote.
Analalamikia pia polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria na kutopewa haki ya kujieleza akiwa mtuhumiwa na matokeo yake kushtakiwa bila ushahidi wowote wa kumuunganisha katika tuhuma hizo.

"Kukamatwa na kushtakiwa kwa mlalamikaji kulifanywa kama matokeo ya Polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria waliopewa chini ya sheria za nchi," inasema sehemu ya hati hiyo ya madai na kuongeza;
"Matokeo yake mlalamikaji ambaye alikuwa na uelewa wa matakwa ya sheria alijeruhiwa sana kiakili na kupata usumbufu.
Mlalamikaji alifedheshwa na aliathirika kwa maumivu ya kiakili kutokana na mchakato wa mashtaka." Zombe katika hati hiyo anadai kuwa Polisi kwa makusudi waliacha kuchukua maelezo yake kuepuka uchunguzi linganifu ambayo yangewezesha kumwachia kabla ya kufikishwa mahakamani, kosa ambalo anadai fidia ya Sh200 milioni kwa madhara aliyopata.

"Kama matokeo ya Polisi kushindwa kutimiza wajibu wake na madhara yaliyompata mlalamikaji, sasa anadai fidia ya Sh5 bilioni kwa madhara ya jumla au kiasi chochote kadri mahakama itakavyoona," inasisitiza hati hiyo ya madai. Sambamba na madai hayo ya fidia, pia Zombe katika hati hiyo ametoa utetezi wake kuhusu tukio la mauaji hayo aliyohusishwa akianza na alivyojiunga na jeshi hilo na kupanda vyeo na nyadhifa hatua kwa hatua, kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo.

Anasema alijiunga na jeshi hilo mwaka 1977 akiwa na cheo cha Konstebo huku akijinasibu kuwa alifanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kwa kujitoa na kupanda katika vyeo mbalimbali hadi alipofikia cheo cha ACP Juni 25, 2003. Anasema Julai, 2001 alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) na kwamba Julai 2 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

Anasema kabla ya kwenda kuripoti aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam alikuwa likizo hivyo yeye akawa anakaimu nafasi hiyo wakati huo pia akiwa bado anafanya kazi kama RCO. Anaeleza kuwa wakati akiendelea na wadhifa huo, Januari 14, 2006 watu wanne waliuawa na mauaji yao yalihusishwa na askari polisi na kwamba yeye alijulishwa kuhusu tukio hilo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Kinondoni.

Anasema Januari 30, 2006 alikabidhi madaraka aliyokuwa akitumikia na aliyokuwa akikaimu kisha Februari 2, mwaka huo akaondoka kwenda katika kituo chake kipya kutumikia wadhifa wa RPC mkoani Rukwa. Anasema kabla ya kwenda Rukwa, Rais alikuwa ameunda Tume ya kuchunguza tukio la mauaji hayo na kwamba ingawa na yeye alihojiwa na tume hiyo lakini anadai kuwa haikupendekeza akamatwe na kushtakiwa.

Comments

0 #4 josephjoel 2011-03-09 15:51 Zombe mwogope mungu mauaji ulioyafanya yalitisha sana.Kwa maoni ninaomba ukatubu vinginevyo malipizi ya mungu ya mungu ni makali sana kupita kiasi.Kwa hiyo ninaomba Bwana Zombe futa hiyo kesi kwa manufaa yako na kizazi chako.Ukumbuke kuwa watoto wa Marehemu uliowauwa bado wanakulalamikia .Na istoshe hata Mke wa Marehem Mine Chomba bado anakulalamikia.Nenda ukatubu haraka sana.
Quote

+1 #3 mkalimani 2011-03-09 11:02 Zombe, Zombe, Zombe...kama wewe unadai mabilioni yote hayo, hao wazazi wa watu uliowaua kikatili nao wadai shilingi ngapi? Ngoja tusubiri tuone. Ukatili wako unafahamika. Watu kibao wamefia mikononi mwako, au kupata ulemavu usioelezeka, na watu wenye kufuatilia mambo katika nchi hii wanafahamu. Na huyo wakili wako, hivi ni njaa, au? Nadhani mawakili wazee sasa wanaanza kutishwa na kasi ya vijana wanaokuja juu. Yaani hata moral guilt hauna? Unamtetea muuaji huyo, ili alipwe fidia ya mabilioni, anunue silaha nyingi na nzito zaidi, aajiri majambazi wapya na wengi zaidi (nje ya jeshi la polisi) na aendeleze "trade" yake sio? I wish your own sons and daughters will be the first victims of "Zombe Murder Inc.," ambayo itaanzishwa as soon as you win your bloodfull civil case.
Quote

+1 #2 M-Tz 2011-03-09 09:34 Mungu anakuona Zombe, usijisafishe kwenye magazeti, we ni jambazi hatari sana, hustahili kuwepo hata uraiani maana hatuna imani na wewe.
Quote

+3 #1 Masoud 2011-03-09 08:02 HABARI BWANA ZOMBE
JEE NA WEWE ULIKUA UKIWAPA HAKI WATUHUMIWA WENGINE? JEE SHERIA ZA NCHI NA JESHI LA POLISI ULIZIPA KIPAOMBELE ULIVYOKUA UNASHUGHULIKIA WATUHUMIWA WENGINE? AU
" MKUKI KWA NGURUWE TUU KWA BINAADAMU NI MCHUNGU "
YOU DESERVED WORSE
 
“Kukamatwa na kushtakiwa kwa mlalamikaji kulifanywa kama matokeo ya Polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria waliopewa chini ya sheria za nchi,” inasema sehemu ya hati hiyo ya madai na kuongeza;
“Matokeo yake mlalamikaji ambaye alikuwa na uelewa wa matakwa ya sheria alijeruhiwa sana kiakili na kupata usumbufu.
Mlalamikaji alifedheshwa na aliathirika kwa maumivu ya kiakili kutokana na mchakato wa mashtaka.” Zombe katika hati hiyo anadai kuwa Polisi kwa makusudi waliacha kuchukua maelezo yake kuepuka uchunguzi linganifu ambayo yangewezesha kumwachia kabla ya kufikishwa mahakamani, kosa ambalo anadai fidia ya Sh200 milioni kwa madhara aliyopata.

“Kama matokeo ya Polisi kushindwa kutimiza wajibu wake na madhara yaliyompata mlalamikaji, sasa anadai fidia ya Sh5 bilioni kwa madhara ya jumla au kiasi chochote kadri mahakama itakavyoona,” inasisitiza hati hiyo ya madai. Sambamba na madai hayo ya fidia, pia Zombe katika hati hiyo ametoa utetezi wake kuhusu tukio la mauaji hayo aliyohusishwa akianza na alivyojiunga na jeshi hilo na kupanda vyeo na nyadhifa hatua kwa hatua, kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo.

Anasema alijiunga na jeshi hilo mwaka 1977 akiwa na cheo cha Konstebo huku akijinasibu kuwa alifanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kwa kujitoa na kupanda katika vyeo mbalimbali hadi alipofikia cheo cha ACP Juni 25, 2003. Anasema Julai, 2001 alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) na kwamba Julai 2 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

Anasema kabla ya kwenda kuripoti aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam alikuwa likizo hivyo yeye akawa anakaimu nafasi hiyo wakati huo pia akiwa bado anafanya kazi kama RCO. Anaeleza kuwa wakati akiendelea na wadhifa huo, Januari 14, 2006 watu wanne waliuawa na mauaji yao yalihusishwa na askari polisi na kwamba yeye alijulishwa kuhusu tukio hilo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Kinondoni.

Anasema Januari 30, 2006 alikabidhi madaraka aliyokuwa akitumikia na aliyokuwa akikaimu kisha Februari 2, mwaka huo akaondoka kwenda katika kituo chake kipya kutumikia wadhifa wa RPC mkoani Rukwa. Anasema kabla ya kwenda Rukwa, Rais alikuwa ameunda Tume ya kuchunguza tukio la mauaji hayo na kwamba ingawa na yeye alihojiwa na tume hiyo lakini anadai kuwa haikupendekeza akamatwe na kushtakiwa.

Comments

0 #4 josephjoel 2011-03-09 15:51 Zombe mwogope mungu mauaji ulioyafanya yalitisha sana.Kwa maoni ninaomba ukatubu vinginevyo malipizi ya mungu ya mungu ni makali sana kupita kiasi.Kwa hiyo ninaomba Bwana Zombe futa hiyo kesi kwa manufaa yako na kizazi chako.Ukumbuke kuwa watoto wa Marehemu uliowauwa bado wanakulalamikia .Na istoshe hata Mke wa Marehem Mine Chomba bado anakulalamikia.Nenda ukatubu haraka sana.
Quote

+1 #3 mkalimani 2011-03-09 11:02 Zombe, Zombe, Zombe...kama wewe unadai mabilioni yote hayo, hao wazazi wa watu uliowaua kikatili nao wadai shilingi ngapi? Ngoja tusubiri tuone. Ukatili wako unafahamika. Watu kibao wamefia mikononi mwako, au kupata ulemavu usioelezeka, na watu wenye kufuatilia mambo katika nchi hii wanafahamu. Na huyo wakili wako, hivi ni njaa, au? Nadhani mawakili wazee sasa wanaanza kutishwa na kasi ya vijana wanaokuja juu. Yaani hata moral guilt hauna? Unamtetea muuaji huyo, ili alipwe fidia ya mabilioni, anunue silaha nyingi na nzito zaidi, aajiri majambazi wapya na wengi zaidi (nje ya jeshi la polisi) na aendeleze "trade" yake sio? I wish your own sons and daughters will be the first victims of "Zombe Murder Inc.," ambayo itaanzishwa as soon as you win your bloodfull civil case.
Quote

+1 #2 M-Tz 2011-03-09 09:34 Mungu anakuona Zombe, usijisafishe kwenye magazeti, we ni jambazi hatari sana, hustahili kuwepo hata uraiani maana hatuna imani na wewe.
Quote

+3 #1 Masoud 2011-03-09 08:02 HABARI BWANA ZOMBE
JEE NA WEWE ULIKUA UKIWAPA HAKI WATUHUMIWA WENGINE? JEE SHERIA ZA NCHI NA JESHI LA POLISI ULIZIPA KIPAOMBELE ULIVYOKUA UNASHUGHULIKIA WATUHUMIWA WENGINE? AU
" MKUKI KWA NGURUWE TUU KWA BINAADAMU NI MCHUNGU "
YOU DESERVED WORSE
 
Zombe aishika pabaya serikali

na Happiness Katabazi

amka2.gif
HATIMAYE aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Mohamed Zombe (57), amefungua kesi ya madai ya fidia ya sh bilioni tano dhidi ya serikali kwa madai ya kunyanyaswa, kudhalilishwa, kumbakia kesi na kukiuka sheria na Katiba ya nchi.
Zombe ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wanne wa madini wa wilayani Ulanga, mkoani Morogoro, amefungua madai hayo juzi kupitia wakili wake Richard Rweyongeza.
Kesi hiyo ambayo imeanza kuvuta hisia za wengi, ilifunguliwa juzi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na kupata namba 35 ya mwaka 2011 ambapo mdaiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa hati ya madai yenye kurasa tisa ambayo Tanzania Daima Jumatano ina nakala yake, Zombe ametoa sababu 21 za kufungua kesi hiyo ya madai ya fidia ya sh bilioni tano na riba ya sh milioni 200.
Afisa huyo wa zamani wa Jeshi la Polisi, anadai kuwa polisi ilikiuka sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 2002, inayotaka kabla ya mtu kukamatwa, lazima aelezwe anakamatwa kwa sababu gani na akifikishwa kituo cha polisi lazima ahojiwe na kuchukuliwa maelezo yake ambayo baadaye hutumika mahakamani kama kielelezo.
"Jeshi la polisi lilikwenda kinyume na sheria hiyo kwani lilinikamata na kunifungulia kesi ya mauji bila hata ya kunihoji na kunichukua maelezo, kwa hiyo kitendo walichonifanyia, kilininyang'anya haki yangu ya msingi iliyoainishwa kwenye Katiba ya nchi inayosema kila mtu ana haki ya kusikilizwa.
"Mimi licha ya kuwa mshtakiwa, nilikuwa ninafahamu vyema sheria za nchi, hivyo kitendo hicho cha ukiukwaji wa sheria nilichofanyiwa na polisi, kilisababisha nifikishwe mahakamani bila kuchukuliwa maelezo ya awali na polisi, jambo ambalo liliniathiri kisaikolojia," alidai Zombe.
Aidha Zombe ambaye sasa anafanya shughuli zake zinazomuingizia kipato mkoani Morogoro na Rukwa, anadai kuwa sababu zingine zilizosababisha afungue kesi hiyo ni Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, kushindwa kulijibu kusudio lake la kuishtaki serikali hata baada ya kutoa notisi ya siku 90.
Anadai kuwa Septemba 27, 2010, alikabidhi barua ya kusudio la kufungua kesi kwa IGP-Mwema na ilionyesha kupokelewa na kiongozi huyo na kwamba siku 90 zilimalizika Desemba 25, 2010 bila kupata majibu.
Katika barua yake ya kusudio, mlalamikaji huyo alimweleza Mwema kuwa atakwenda mahakamani iwapo masharti ya kuombwa radhi na kulipwa fidia, yasingetekelezwa.
Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ilitoa hukumu ya kushtusha baada ya kumwachilia huru Zombe na wenzake wanane waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva teksi mmoja.
Serikali ilikata rufaa Oktoba 7, 2009 katika Mahakama ya Rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyomwachilia Zombe na wenzake.
Akisoma hukumu, Jaji wa Mahakama ya Rufani, Salum Massati, alisema baada ya kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, alibaini kuwa serikali ilishindwa kuthibitisha mashtaka na kuwa kamwe mahakama haiwezi kumtia hatiani mshtakiwa kwa ushahidi dhaifu na wa kusikia kama uliowasilishwa mahakamani hapo.
Jaji huyo alihitimisha hukumu yake kwa kusema kuwa washtakiwa hao si wauaji na aliliagiza Jeshi la Polisi liwatafute wauaji halisi wa wafanyabiashara waliouawa.
 
Zombe aidai Serikali fidia ya Sh5.2bilioni Send to a friend Tuesday, 08 March 2011 21:42

James Magai na Tausi Ally
ALIYEKUWA mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teski wa Manzese, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe juzi ameishtaki serikali akiiomba mahakama iiamuru imlipe fidia ya Sh5.2bilioni.

Zombe alikamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 9, 2006 na kuunganishwa na askari wenzake wengine ambao jumla yao walikuwa 13 wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya Sabinus Chigumbi (Jongo), Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu, katika msitu wa Pande wilayani Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Januari 14 mwaka 2006. Hata hivyo, Agosti 17, 2009 watuhumiwa wote waliachiwa huru na Mahakama Kuu Dar es Salaam, mbele ya Jaji Salum Massati baada ya kuonekana kutokuwa na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.

Kiasi hicho anachodai Zombe ni fidia ya madhara ya jumla na Sh200 milioni ikiwa ni fidia kwa adhabu ya kumweka ndani, riba pamoja na gharama za kesi hiyo.Wakati Zombe akifungua kesi hiyo ya madai, Serikali imekata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu iliyomwachia huru yeye na wenzake wanane ambayo bado haijatolewa uamuzi wala kusikilizwa.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyoandaliwa na Wakili Mwandamizi, Richard Rweyongeza, Zombe anadai alipwe fidia ya kiasi hicho au kingine ambacho Mahakama itaona kifaa kutokana na madhara aliyopata kutokana na kesi hiyo kwa kosa la kukamatwa na kumshtaki kwa tuhuma hizo akidai kuwa ni ukiukwaji wa sheria.

Katika kesi hiyo iliyosajiliwa kwa namba 35 ya mwaka 2011, mbali na kuomba mahakama hiyo iiamuru Serikali imlipe fidia, Zombe pia anaomba hiyo itamke kuwa alikamatwa na kushtakiwa kinyume cha sheria na ni batili.
Zombe anadai kuwa kabla ya kukamatwa alikuwa amehamishiwa katika Mkoa wa Rukwa na alirejeshwa Makao Makuu ya Polisi siku 14 baada ya kuwa ameripoti katika kituo chake hicho kipya cha kazi. Anadai kuwa siku hiyo kabla ya kukamatwa na kupandishwa kizimbani aliitwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ambaye alimjulisha kuwa anatakiwa kuunganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo.

Anadai kuwa baada ya taarifa hizo alichukuliwa ghafla na kupelekwa mahakamani ambako Hakimu Mkazi Mkuu alikuwa akimsubiri na kwamba mara baada ya kusomewa mashtaka yake alipelekwa katika Gereza la Ukonga mahali ambako kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kumpokea.
Lakini analalamika kuwa baada ya kukamatwa, polisi walikuwa na wajibu wa kumwuliza kama alikuwa na jambo lolote la kusema ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu maelezo yake. Hati hiyo inadai kuwa kinyume chake, kukamatwa kwake kulifanyika kinyume cha wajibu huo, yaani bila kusikilizwa mlalamikaji kama alikuwa na cha kusema kuhusu ushiriki wake katika tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa hati hiyo, wakati akiwa mahabusu katika Gereza la Ukonga na baadaye Keko, Zombe aliwasilisha malalamiko yake kwa waziri mwenye dhamana ya masuala ya kisheria jinsi alivyotendewa lakini hakupata mwitiko wowote.
Analalamikia pia polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria na kutopewa haki ya kujieleza akiwa mtuhumiwa na matokeo yake kushtakiwa bila ushahidi wowote wa kumuunganisha katika tuhuma hizo.

"Kukamatwa na kushtakiwa kwa mlalamikaji kulifanywa kama matokeo ya Polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria waliopewa chini ya sheria za nchi," inasema sehemu ya hati hiyo ya madai na kuongeza;
"Matokeo yake mlalamikaji ambaye alikuwa na uelewa wa matakwa ya sheria alijeruhiwa sana kiakili na kupata usumbufu.
Mlalamikaji alifedheshwa na aliathirika kwa maumivu ya kiakili kutokana na mchakato wa mashtaka." Zombe katika hati hiyo anadai kuwa Polisi kwa makusudi waliacha kuchukua maelezo yake kuepuka uchunguzi linganifu ambayo yangewezesha kumwachia kabla ya kufikishwa mahakamani, kosa ambalo anadai fidia ya Sh200 milioni kwa madhara aliyopata.

"Kama matokeo ya Polisi kushindwa kutimiza wajibu wake na madhara yaliyompata mlalamikaji, sasa anadai fidia ya Sh5 bilioni kwa madhara ya jumla au kiasi chochote kadri mahakama itakavyoona," inasisitiza hati hiyo ya madai. Sambamba na madai hayo ya fidia, pia Zombe katika hati hiyo ametoa utetezi wake kuhusu tukio la mauaji hayo aliyohusishwa akianza na alivyojiunga na jeshi hilo na kupanda vyeo na nyadhifa hatua kwa hatua, kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo.

Anasema alijiunga na jeshi hilo mwaka 1977 akiwa na cheo cha Konstebo huku akijinasibu kuwa alifanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kwa kujitoa na kupanda katika vyeo mbalimbali hadi alipofikia cheo cha ACP Juni 25, 2003. Anasema Julai, 2001 alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) na kwamba Julai 2 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

Anasema kabla ya kwenda kuripoti aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam alikuwa likizo hivyo yeye akawa anakaimu nafasi hiyo wakati huo pia akiwa bado anafanya kazi kama RCO. Anaeleza kuwa wakati akiendelea na wadhifa huo, Januari 14, 2006 watu wanne waliuawa na mauaji yao yalihusishwa na askari polisi na kwamba yeye alijulishwa kuhusu tukio hilo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Kinondoni.

Anasema Januari 30, 2006 alikabidhi madaraka aliyokuwa akitumikia na aliyokuwa akikaimu kisha Februari 2, mwaka huo akaondoka kwenda katika kituo chake kipya kutumikia wadhifa wa RPC mkoani Rukwa. Anasema kabla ya kwenda Rukwa, Rais alikuwa ameunda Tume ya kuchunguza tukio la mauaji hayo na kwamba ingawa na yeye alihojiwa na tume hiyo lakini anadai kuwa haikupendekeza akamatwe na kushtakiwa.

Comments

0 #4 josephjoel 2011-03-09 15:51 Zombe mwogope mungu mauaji ulioyafanya yalitisha sana.Kwa maoni ninaomba ukatubu vinginevyo malipizi ya mungu ya mungu ni makali sana kupita kiasi.Kwa hiyo ninaomba Bwana Zombe futa hiyo kesi kwa manufaa yako na kizazi chako.Ukumbuke kuwa watoto wa Marehemu uliowauwa bado wanakulalamikia .Na istoshe hata Mke wa Marehem Mine Chomba bado anakulalamikia.Nenda ukatubu haraka sana.
Quote

+1 #3 mkalimani 2011-03-09 11:02 Zombe, Zombe, Zombe...kama wewe unadai mabilioni yote hayo, hao wazazi wa watu uliowaua kikatili nao wadai shilingi ngapi? Ngoja tusubiri tuone. Ukatili wako unafahamika. Watu kibao wamefia mikononi mwako, au kupata ulemavu usioelezeka, na watu wenye kufuatilia mambo katika nchi hii wanafahamu. Na huyo wakili wako, hivi ni njaa, au? Nadhani mawakili wazee sasa wanaanza kutishwa na kasi ya vijana wanaokuja juu. Yaani hata moral guilt hauna? Unamtetea muuaji huyo, ili alipwe fidia ya mabilioni, anunue silaha nyingi na nzito zaidi, aajiri majambazi wapya na wengi zaidi (nje ya jeshi la polisi) na aendeleze "trade" yake sio? I wish your own sons and daughters will be the first victims of "Zombe Murder Inc.," ambayo itaanzishwa as soon as you win your bloodfull civil case.
Quote

+1 #2 M-Tz 2011-03-09 09:34 Mungu anakuona Zombe, usijisafishe kwenye magazeti, we ni jambazi hatari sana, hustahili kuwepo hata uraiani maana hatuna imani na wewe.
Quote

+3 #1 Masoud 2011-03-09 08:02 HABARI BWANA ZOMBE
JEE NA WEWE ULIKUA UKIWAPA HAKI WATUHUMIWA WENGINE? JEE SHERIA ZA NCHI NA JESHI LA POLISI ULIZIPA KIPAOMBELE ULIVYOKUA UNASHUGHULIKIA WATUHUMIWA WENGINE? AU
" MKUKI KWA NGURUWE TUU KWA BINAADAMU NI MCHUNGU "
YOU DESERVED WORSE
Quote
 
nashukuru kiongozi kwa thread. but sijaelewahapo CCM wanausika vipi na madai ya aliyekuwa ACP-ZOMBE?
Lakini hii pots imenipa maswali mengi kuwa uwenda kutakuwa nasiri ya madai hayo labda kuzidi kuiporomosha serikali kiuchumi,licha ya hayo yanayotukabili,cz bil 5 na riba ya Tsh mil200 si mchezo kwa hali ya taifa ya sasa
 
Mmh! Mbona nyingi hivyo.
Dah! Hivi serikali haiwezi kubargain hapo?
Nitamtafuta zombe anipe japo kamilioni.
 
alipwe kama hakutendewa haki, kwan serikal huwa haichelewi kulipa, hata mm nina mpango wa kudai kafidiba ka boom langu la miaka mmiitatu
 
Zombe anashinda hiyo kesi bila shaka.
Kwa Serikali hii hata sina hofu na ushindi wake wa kishindo.
 
Saafi shitaki chota pay anza zako kwa amani TZ ni shamba la bibi. Kukurupuka kushtaki watu ili serikali ionekane inafanya kazi kutatufilisi, bado kina Mramba na wenzake sikilizieni. Hafu unakuta m2 kavaa shati, kofia, khanga za ccm. Bongo lala.

Miradi ya ufisadi TZ ni mingi sana tofauti ni applications zake,Umeuwa ushahidi hakuna unapelekwa mahakamani na mmekwisha panga mgao kabisa,dhrura ya umeme hoo RICHMOND,DOWANS,IPTL,usalama wa taifa leteni RADA KUBWA,usafiri wa RAIS lete NDEGE mbovu, Malaria haikubaliki leteni NETI nyingi uchumi utaimarika,Ukimwi miradi mingi yote ya kifisadi tu,kila kitu ni magumashi nchi hii mungu tusaidie utuletee mababu wengi kama wa Loliondo tutapona wote.
 
Zombe anashinda hiyo kesi bila shaka.
Kwa Serikali hii hata sina hofu na ushindi wake wa kishindo.

Utashangaa Killer Zombe anashinda kesi, wale wazee wa East Africa community hadi leo wanasugua mguu hawajalipwa wakati ni haki yao ya msingi.:hatari:
 
1.Ngumbaru 2.Zuzu 3.Juha Mnisaidie kuwapa MAJINA kati ya hawa ANAYEDAI FIDIA ANAYEDAIWA FIDIA ANAYESIMAMIA SHERIA. Tusisahau kusali Mungu atatunusuru!!!!!
 
Back
Top Bottom