hasan124
JF-Expert Member
- Jan 2, 2012
- 716
- 128
Lile zoezi la Uhakiki Wanachama kwa chama cha ADC linaendelea vyema na kwa mafanikio. Zoezi Hilo lilianza mkoani Tanga jumapili ya tar.08-07-2012 likifunguliwa rasmi na msajili WA vyama vya Siasa NCHINI MHE. John Tendwa na kusifia namna Uongozi WA ADC CHINI ya MHE. Said Miraji (m/kiti TAIFA) ulivyojipanga kukamilisha kazi hiyo.
Tar. 10-07-2012 ILIKUWA Zamu ya mkoa WA Mwanza ambapo kwa mujibu WA televisheni ya TAIFA TBC1 zoezi Hilo lilikamilika vyema ambapo wanachama zaidi ya 1000 walijitokeza kutoka wilaya za Nyamagana, Ilemela na Magu hivyo kuvuka kwa mbaaaali idadi ya wanachama 200 inayohitajika na Ofisi za Msajili WA chama Kisheria. Hali iliyopelekea Muwakilishi WA Msajili Kanda ya Ziwa kusajili wanachama 240.
Zoezi hili linaendelea tena tar. 12-07-2012 huko Mkoani Mara CHINI ya usimamizi WA Kamishna WA ADC MHE. Jumanne Magafu na Pemba Visiwani CHINI ya Kamishna Said Seif sehemu inayoaminika miaka mingi kuwa ni ngome ya kisiasa ya chama cha wananchi CUF (INAYOLEGALEGA) na kuthibitisha Hilo katika jimbo moja tu la Wawi ADC kuna wanachama zaidi ya 1000 ambao wako Tayari kwa Uhakiki huo.
Baada ya Pemba tar. 14-07-2012 itakua ni zamu ya Unguja, na utaratibu huo utaendelea hadi hitimisho mnamo tar.17-08-2012 JiJiNi Dar ES Salaam hivyo kufanya mwanzo mwema wa ile safari inayosubiriwa na wananchi wengi WA Tanzania ya kupata chama Mbadala WA CCM chenye Madhumuni ya:
1. Kushika dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
2. Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa WaTanzania wote.
3. Kujenga Uchumi imara na kulinda raslimali za Nchi kwa manufaa ya WaTanzania wote.
4. Kupiga kwa nguvu zote aina zote za Ubaguzi na Ukandamizaji.
5. Kuheshimu mikataba ya kimataifa inayohusu haki halisi za binadamu.
ADC - DIRA ya Mabadiliko.