MKWECHE
JF-Expert Member
- Apr 8, 2011
- 299
- 64
Budget ya Zitto haina Jipya!Kelele nyingii mpaka wanasahau vitu muhimu vya Kiufundi!Sehemu kubwa Budget Mh.Zito Kadesa kwa Dr.Mgimwa,Budget ya zito Wala haina mashiko ya kuwa budget mbadala!Kikubwa ni kurekebisha mapungufu kule kwa Dr Mgimwa ili buget isimame kama ruler!Hii ya Upinzani ni MKWECHE kama mimi!Ndo mana mchemba anaitupa![h=6]Maelezo ya Bajeti Kivuli Katika mjadala unaoendelea Bungeni kuhusu Bajeti, baadhi ya wabunge wameeleza kwamba Bajeti Kivuli haikuonyesha vyanzo vya mapato na hivyo kuita ni vyanzo sifuri. Ukweli ni kwamba tumeweka vyanzo vya mapato ya ndani kwa ujumla bila kuainisha mapato ya kikodi ni ngapi, mapato yasiyo ya kikodi ni ngapi na mapato ya Halmashauri ni kiasi gani. Hivyo tunakiri kosa hili na tumechukua hatua ya kuainisha mapato hayo Kama inavyoonekana kwenye jedwali hili hapa chini. Mapato haya yamo ndani ya Hotuba ya Bajeti Mbadala lakini kwa makosa ya kihariri hayakuonyeshwa kwenye jedwali na hivyo kuleta usumbufu kwa Wabunge na Watanzania wengine waliopata fursa ya kusoma Hotuba yetu. Tunaomba radhi kwa usumbufu. Nawashukuru walioona tatizo hili na hii inaonyesha kuwa wabunge wanasoma kwa makini Bajeti ya Upinzani. Ninawatakia mjadala mwema wa Bajeti. JUMLA YA MAPATO YA NDANI Tshs. Millioni 11,889,078/- MAPATO YA KODI Tshs. Millioni 10,232,539/- MAPATO YASIYO YA KODI Tshs. Milion 1,163,533/- MAPATO YA HALMASHAURI Tshs. Milioni. 493,006/- Kabwe Zuberi Zitto,Mb Waziri Kivuli wa Fedha[/h]