Elections 2015 Zitto: Sitagombea Urais wala Ubunge 2015

Huyu zitto ni jembe sana bado tunahitaji chalenge zake sana maana bado kijana na mawazo ya kujenga sio kama wale wafanya vurugu




Zitto ameahidiwa uwaziri endapo ccm itashinda, mwache aende maana alikuwa haeleweki ndani ya chama.
 
Ben kapiga Multiple scores no matter what you say.......Kwanza aliona right way, alichofanya kukisimamia against popular and wild Zitto,psychopathic aliye tayari kusema na kufanya lolote kumuondoa anayemwekea usiku, ni kuamua panda kilimanjaro huku watu wato wote hata wanaotoa vibali wakiwa vikwazo, na baadae kupanda mlima, then watu wenye maumbile tofauti nao wakapanda mlima.Ben alikuwa na critics wengi sana, akasimama na kusema yupo tayari kuthibitisha, na yote aliyosema yametokea na yanaendelea tokea.......ni avalance ............bado ataumbuka sana Zitto.

Kajiona kuwa ni mjuaji kwa kublack mail kila mtu on his ways, ktk siasa, chama chake, ktk jamii kaingia kwa wasanii ili awaibie ring tones ,kwenye madini kote kanyamazishwa kwa hela.Soon utasikia na wasanii nao wakikomoaa naye...

Kuna msanii alimchana juzi kuwa wakati Sugu akikomaa na wezi wa kazi za wasanii yeye Zitto alikua busy kumchochea Ruge dhidi ya Sugu huku wakishirikiana na January Makamba kinafiki.

Nimrodi Mkono amemuunganisha na mafisadi.Uhusiano wake na Rostam Aziz alisema ulianza baada ya kutambulishwa kwake na mbowe.Ni aina ya watu wanaotambulishwa kwa mtu katika mazingira ya kikawaida tu ila baada ya hapo yeye anatumia nafasi ya kumjua mtu huyo kupiga dili na hata hujuma kwa taasisi.Hajawahi kukanusha au kueleza walichozungumza na Jack zoka.
 
Zitto ameahidiwa uwaziri endapo ccm itashinda, mwache aende maana alikuwa haeleweki ndani ya chama.

[h=2][/h]

  • Siri za Zitto nje
  • Mawasiliano yake yanaswa
  • Aponzwa na mwandishi wa habari

Na Saed Kubenea

SIRI kubwa kuhusu mwenendo wa Zitto Kabwe (Mb) ndani ya chama chake zimeanikwa mitaani na zinaweza kumzamisha kisiasa, MwanaHALISI sasa linaweza kuripoti.

Siku nne baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Willibrod Slaa kusema wamenasa taarifa za mawasiliano ya Zitto, baadhi ya taarifa zimepatikana jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Zitto ananukuliwa akiapa kusaidia wagombea uongozi katika vyama vingine; na katika moja ya taarifa ananukuliwa akisema atasaidia David Kafulila kupata ubunge "hata kabla ya akina John Mnyika…"

Mnyika ni Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema na Kafulila alikuwa Afisa Habari ambaye baada ya kuondolewa wadhifa huo amekimbilia NCCR-Mageuzi. Mnyika anatarajia kugombea ubunge jimbo la Ubungo.

Naye Zitto amenukuliwa na gazeti la Mwananchi la Jumatatu akilalamika kuwa ameingiliwa katika mawasiliano yake ya baruapepe (e-mail); jambo ambalo Mkurugenzi wa Upelelezi, Robert Manumba, amedakia haraka na kusema Zitto akiwapelekea malalamiko watashughulikia.

Kwa mujibu wa mpangilio wa taarifa husika, lazima aliyezitoa amepata ufunguo wa baruapepe (password) wa ama Zitto au mwandishi wa habari wa Mwananchi, Denis Msacky.

Karibu mawasiliano yote ni kati ya Zitto na Msacky juu ya "ushujaa" wa Zitto na jinsi anavyopendwa nje ya chama huku "akichukiwa" na viongozi wake wakuu.

Katika moja ya mawasiliano, inaonyeshwa kuwa Msacky alimwandikia Zitto akieleza, "Leo hii Mrema (Augustine Lyatonga) anasema anakuheshimu wewe, lakini si Mbowe; hivyo hivyo, Lipumba (Profesa Ibrahim) na James Mbatia wanasema wewe una visheni."

Katika mawasiliano hayo ya Jumanne, 1 Desemba 2009, saa 6.45 adhuhuri, Msacky anaonyeshwa kumwambia Zitto pia kuwa, "CCM nao…wanakusifu kwamba pamoja na kwamba unawaliza sana , lakini ni kiongozi shupavu."

"Leo hii siasa za Chadema zingekuwa zinatisha kama ungekuwa mwenyekiti wa Chadema, vijana nchi nzima wangejiunga na chama, uko nao karibu, unaongea nao, una elimu nzuri, unajua mambo, unasoma sana ," imeeleza sehemu ya mawasiliano kutoka kwa Msacky kwenda kwa Zitto.

Kinacholeta wasiwasi ndani ya Chadema kinaweza kuwa lugha inayotumiwa katika mawasiliano hayo. Kwa mfano, katika waraka huohuo, Msacky ananukuliwa akiandika:

"Wanataka kukumaliza, nami sitakubali mtu ammalize rafiki yangu nikiangalia…wanasema Mbowe hata Mbatia akikaa vema anaweza kumpita kama siasa za kufukuza zitaendelea. Muhimu, usisikilize watu, tulia, urudi tupange tufanye nini? Lakini ukweli ni kwamba sasa wanakuogopa…Mwenyekiti Mtarajiwa…"

Mawasiliano yanaonyesha kuwa Zitto hakufurahishwa sana na taarifa za Mwananchi kuwa amemsaidia Kafulila magari matatu kwenda Kigoma kufanya kampeni chini ya NCCR-Mageuzi, lakini Msacky anaonyesha kumfariji.

"Kaka, mimi nimeiona story, haina matatizo zaidi ya kuwafanya akina Mbowe kusitisha mpango mbaya dhidi yako maana wanaanza kuogopa. Hata Mrema Lyatonga amesema kwamba Zitto huwa unamsaidia akiwa na shida. This shows that ur a leader katika opposition, wewe ni mtu wa maridhiano, unakuza upinzani Kigoma," anaeleza.

Anasema, "Leo nasikia akina Mnyika wanahaha sana , waambie familia yako wasiingie katika mtego wa kuanza kuhojiwa na akina Kubenea (Saed wa MwanaHALISI), watawachanganya. Wewe usiongee kitu chochote, wabaki wanahaha, lakini for sure you are safe, na hizo kampeni za Mnyika kukuchafua huku akitaja majina ya Kafulila, ataziacha."

Akionyesha juhudi za kushawishi, kuliwaza au kufarakanisha, Msacky anaandika, "Katika hili Zitto, mimi niko na wewe, huna kosa ambalo umefanya, na wala usihofu maana wewe utakuwa nguzo ya upinzani Tanzania …Wanakupa majina ya ajabu, wanakuita Mr Dowans, wanatumia akina Halima Mdee kukuchafua katika magazeti…"

Awali Zitto alikuwa amemwandikia Msacky akisema, "Stori niliyoiona kwenye mwananchi
itaniletea matatizo sana ." Hiyo ilikuwa Jumatatu 30 Novemba 2009, saa 5.21 asubuhi. Baruapepe hiyo ilikuwa na kichwa kisemacho: "Muhimu na haraka."

Aidha, katika mawasiliano mengine, Zitto anaendelea kuonyesha kutofurahishwa na taarifa juu ya magari matatu kwa safari ya Kafulila.

Naye anaandika kwa Msacky, "tatizo la stori ni wingi wa magari, itaonekana mimi nina magari mengi na ni fisadi unajua? Hilo ndio tatizo."

Saini ya Zitto inatofautiana katika baadhi ya baruapepe. Pengine anaandika "zitto" na kwingine anaandika "Zi."

Moja ya mawasiliano ambayo yanazua mashaka yanaonyesha Zitto akikiri kuwa na mawasiliano na waasi nchini Kongo akiandika, "take it from me (niamini), nina contacts nyingi sana Congo na hao rebels (waasi) huwa wananiomba sana ushauri na kutaka kuwaunganisha."

Katika moja ya mawasiliano, Msacky anamwonya Zitto kutotumia baruapepe ya "Chadema kwa mawasiliano ya siri" na kutaka amwambie mama yake Shida Salum akatae kuongea na waandishi wa habari. "…nasikia Mbowe anataka mama awe akiongea na waandishi, usikubali," alieleza.

Zitto alipoulizwa kuhusu taarifa ya Mwananchi kuwa anatembea na barua mfukoni ya kujiuzulu uanachama Chadema, alisema "Sina la kusema."

Alipong'ang'anizwa kwamba imekuwaje hawezi kuzungumzia suala hilo ambalo ni muhimu kwa mustakabali wake wa kisiasa kwa chama chake, Zitto alisema, "Ni kwa sababu sitaki kuingia katika malumbano na katibu mkuu wangu (Dk. Willibrod Slaa) kwani malumbano hayo hayataijenga Chadema."

Alipotakiwa kueleza juu ya baruapepe ambazo zinadaiwa kuwa mawasiliano kati yake na Msacky, haraka alijibu, "Sina la kusema."

Alipoelezwa umuhimu wa yeye kueleza msimamo wake juu ya baruapepe hizo, Zitto alijibu, "Chochote nitakachosema sasa hivi, kitawachanganya Watanzania.

"Sitaki malumbano. Hakuna sababu ya kuwachanganya Watanzania. Hiyo haina maana yoyote," alisema Zitto kwa sauti ya ukali. Zitto alikuwa akiongea kutoka Ujerumani kwa simu Na. +4915222493231.

MwanaHALISI ilimtafuta Msacky. Baada ya kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa, hatimaye aliandika ujumbe "Kaka, niko katika kikao. Tuma ujumbe."

Msacky aliulizwa, "Kaka, tumesikia kwamba umetajwa katika sakata la Zitto na chama chake na kwamba wewe ndiye mtibuaji. Je, ni kweli?" Hakujibu ujumbe na alipopigiwa simu ilikuwa inaita hadi kukatika.

Gazeti lilipowasiliana na Mnyika na kumueleza kwamba amekuwa akitajwa katika ujumbe wa Zitto na Msacky, alikiri kupokea ujumbe huo wa baruapepe uliotoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni "Mtanzania mwema."

Alisema alipoona ujumbe mmoja unahusu Zitto kushauri Msacky kutochapisha habari za mkutano wake na waandishi wa habari, ndipo aliamua kupeleka ujumbe huo kwa Zitto.

"Nilimuuliza kuna hiki kitu nimetumiwa. Je, haya ni maandishi yako au kuna mtu ameingilia emaili yako na kujiandikia haya? Hadi leo hii, bado sijapata jibu," alisema Mnyika kwa sauti ya masikitiko. Alisema yeye hana cha kusema na kuongeza, "labda umuulize Zitto."

Alipoulizwa anachukuliaje suala hilo , Mnyika alisema, "Ukiniuliza mimi kwa upande wangu, nilitegemea mambo hayo yangemalizwa katika vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Lakini kwa hatua ya hivi sasa, nadhani Zitto bado anayo fursa ya kulieleza hili.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe alipoulizwa juu ya madai ya kuwapo njama za kuhujumu chama chake zinazofanywa na Msacky kwa kumtumia Zitto, haraka alijibu, "tuna utaratibu wetu wa kushungulikia mambo ndani ya Chadema."

Alisema, "Sina la kusema. Chadema ina utaratibu wake wa kushughulikia mambo yake."

Kwa kadri mawasiliano ya Zitto na Msacky yanavyoonyesha na iwapo yatathibitishwa kuwa kweli, jambo ambalo linaanza kuthibitishwa na Zitto kwa kulalamika kuingiliwa kwenye faragha, basi uhusiano wake katika chama utakuwa umepata nyufa.

Wachunguzi wa siasa za upinzani nchini wanasema kwa hali hii, uwezekano wa Zitto kubaki ndani ya chama chake ni mdogo. "Ama atajiondoa mwenyewe au hatimaye atafukuzwa," ameeleza mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam .

Hata hivyo, Zitto amenukuliwa na Mwananchi akisema, "Sitaki kugombana na mtu mimi. Wala msiniweke kwenye kifungo cha siasa. Ni bora niishi huru kuliko katika mateso ya siasa za kipumbavu kabisa. Nitafanya maamuzi ambayo hayajawahi kufikiriwa."

Wiki iliyopita Kafulila aliwaambia waandishi wa habari kwamba Zitto atafanya maamuzi makubwa ambayo hawakutegemea.

Chanzo: MwanaHalisi​
 
Nicholas, tatizo la uchambuzi wa matatizo ya psychology ni kwamba hakuna mzima. naweza nikachambua word selection yako katika argumentation zako nyingi hapa nikakuta wewe pia ni mgonjwa. Kwa hiyo tofauti zetu ni degrees--au pengine niseme viwango vya kuumwa. Hilo linazusha haja ya kuvumiliana katika ubinadamu wetu. Lakini pia ukifanya individual cost-benefit analysis ya hatma ya mwisho ya maamuzi ya mtu ndiyo hupunguza hukumu ya tendo lenye sura ya wehu. Hii ndiyo dhana inayotumiwa kuruhusu vita.

bottom line ya uamuzi wa zitto ni nini kwake at individual level? kwanza ataepuka migogoro ya kisiasa ambayo ni mingi. anataka kazi isiyokuwa na migogoro mingi. anataka amani at individual level. kuna wehu gani katika kutafuta a peaceful life? nadhani ni vizuri ukifuta kauli....usimwite zitto psychopath. hii kauli si sahihi.

Haha..km issue ni degree then kuna degree fulani ya kuumwa ni an acceptable.Otherwise hata vichaa watagombea urais ingawa kila mtu ana kiasi fulani cha wendawazimu.


Km nikuondoka ni vyema sana kwake,ila kwa jinsi alivyochelewa na alivyoji bahave, na atakchofanya tena kina mpact kwa simple minded people ambao si rahisi kwake kuacha drama zake.

Sijui ataibukia magamba km vijana wake au lah..lets see.
 
hawezi kuacha siasa anataka kuwa wazir mkuu wa tz maana katiba mpya haiitaji wazir mkuu ambae ni mbunge huyo kijana anaona mbali anataka ajiunge na ccm ili makamba ampatie u pm
hiyo ndo plani cdm mpooo
so you mean kuna combination ya Zitto na Makamba 2015?
 
>Unapokuwa kwenye vita alafu ukakimbia na kuacha wenzako unaonyesha wewe ni mwoga tu! Ktk mapambano hupaswi kuwakimbia wenzako... Zitto acha kuogopa mapambano... Siasa bado inakuhitaji sana...
 
As for me hii ni dalili ya kujiweka sawa ili akikosa aonekane hakutaka. Be free to do whatever you want Zitto but kutangaza kila wakati kunakuonesha unahangaika sana. Matendo yatakufanya uonekane una hekima sana kuliko matamko ya mara kwa mara.
 
asilimia 90 ya members mnaojadili hoja hii nadiriki kusema hamjui mnachojadili.....wengi mnaongea hisia zenu...dhima ya makala hiyo katika gazeti haiko kama ilivyo na mnavyoijadili....

you should think beyond the next meal

''nchi hii ngumu''
 
Hawa watoto ni wafu ingali wapo hai, ndio maana mabasha wanaongezeka kila siku kwa ajili ya watoto wenye njaa kama hawa ambao wako tayari kupakatwa ili wahongwe GX 110, kina dada wawe makini na vijana kama hawa njaa kali kwani wanawamezea matr hata mariana wa dada zao.

Kabisa,
Na kwa kias kikubwa sana CHADEMA kinapitia wakati mgum sana kwa sasa,asilimia kubwa ya vijana sampuli hiyo wamekimbizia matumain kwa CHADEMA moja kwa moja na kuacha kuhangaika kufanya kazi na kutafuta namna ya kujikwamua na utumwa wa fikra,

Wanadhani kama CHADEMA kikiingia madarakani kitakuwa kinawajaza pesa mifukoni,haitafanya hivyo,

Ikiingia Madarakan kwa ridhaa ya wananchi itachofanya ni kusimamia sera zake na kuahid kile kilichokuwa kinasemwa kwa wananchi,

Wao wanadhani kwa kukaa bila kufanya kazi na kushabikia shabikia basi maisha yao yatabadilika once chadema kikichukua inchi,wanashindwa kuelewa maisha ni haya haya,na kila siku watu wanakufa na kuzaliwa,
Tumaini Makene naomba wewe kama msemaji wa chama uchukue jukumu la kuwakemea hawa waganga njaa na wachumia tumbo wanaodhani kukesha kuwalamba lamba miguu viongoz wa juu wa chama basi itawarahishia maisha hapo baadae,

Mfano ni hawa vijana wababishaji na wenye njaa kali kama Yericko & Saa nane,itoke kauli ya uhakika dhidi ya hawa vijana,

Wanajenga taswira mbovu ya chama ili hali hawana influence yyte na by the way hakuna tuh anaewatambua kwa namna yoyote ile,

Wana kua ni taswira ya chama hali ya kuwa wao wana taswira zao binafsi zilizofifia na kukosa matumain,

Waambie wasitegemee kubebewa na taasis,wajenge identity yao,pia waache ufitini na udanganyifu kwa kutumia nembo ya chama,

WANATIA KICHEFU CHEFU
 
Last edited by a moderator:
Haha..km issue ni degree then kuna degree fulani ya kuumwa ni an acceptable.Otherwise hata vichaa watagombea urais ingawa kila mtu ana kiasi fulani cha wendawazimu.


Km nikuondoka ni vyema sana kwake,ila kwa jinsi alivyochelewa na alivyoji bahave, na atakchofanya tena kina mpact kwa simple minded people ambao si rahisi kwake kuacha drama zake.

Sijui ataibukia magamba km vijana wake au lah..lets see.

amechagua wakati mzuri kuacha siasa. lakini pia kazi anayotaka kufanya ya kufundisha ni nzuri. siasa ni complicated kuliko uhadhiri wa chuo. tumuombee dua mipango hii iende vizuri. kuhamia ccm si mwafaka sana kwake au mtu yeyote mwingine kwa sasa. wale watoto waliohamia kule nadhani ni utoto ulikuwa unawasumbua. hakuna mtu mzima angeshindwa kuona ccm ni jini nimefungwa kamba pamoja na tani ya mawe na kutupwa baharini. mtu kujaribu kuliokoa jini hili ni kutafuta kuzama nalo.... kwa hiyo nadhani hatafanya kosa hilo. na huu ni ushahidi mwingine si mwehu.
 
ndo maana yake...nawashauri hata kina lisu,mnyika,msigwa,lema,nasra,sugu,mdee waachane na ubunge,wasubiri kuja kuwa mawaziri,japo tena ccm ikishinda itakuwa imekula kwao.

CDM ni chama makini,kimeweza kutoa wanasiasa makini kama hao uliwataja hapo juu. Mchango wa Zitto ndani ya CDM ni mkubwa sana. Ni matumaini yetu Dr.W.Slaa na Kamanda Mbowe wataendelea kuibua vijana mahiri ili waendelee kuwatetea watanzania kama wafanyavyo akina John Mnyika,n.k
 
Last edited by a moderator:
Vijana wengi wa kitanzania ni wajinga, naona wimbi la vijana hapa JF wakidhihirisha ujinga. Zitto mwenyewe kama kasema kuwa hatagombea urais basi nae namweka kwenye kundi la wajinga.

Sielewi. Kwani Zitto hata akiutaka urais hawezi kugombea 2015 katiba haimruhusu, na pia hata km katiba haimruhusu kabla yaa kutoa dhamira atambue ktk chama kuna mchakato wa kumpata mgombe urais (wapo wengi chadema).

Ukiona mtu anaimba hii chorus ya Zito kusema hatagombea urais ni alama ya ujinga. Ni sawa na Juliana shonza, au mtela aseme nimeahirisha 2015 sitagombea urais. Alafu wewe unaanza kujenga hoja kuhusu hiyo kauli na unasikitika while in a real sense hata wangetaka wasinge weza sababu ya umri.

Zitto amegundua katiba mpya haitamfavor na pia amepoteza ile catch aliyokuwa nayo, siyo vibaya akapumzika labda (aje kuwa waziri km katiba itaruhusu ndicho anachowaza maana rasimu inaonesha mawazir hawatatokana na wabunge).

Zitto hana tofaut na JK. Anapenda kufanya movement within institution in the end apate reward yeye mwenyewe, na aonekane yeye ndio don. Kama jambo halimpi sifa yeye binafsi hawezi kulifanya (ubinafsi na sifa)

Ana tabia ya usaliti. Sasa hapa ni tabia ya watu wa kigoma (wild kaborou, nsanzugwanko, david kafulila)..hata tafuta mtu wa kigoma hapo ulipo wana asili ya kutait.


Pia sio msaada ndani ya cdm..ikumbukwe 2010 wakati wanamnadi Slaa yeye anajinadi kuwa atagombea urais, wakati wenzake wanapambana na wizi wa kura yeye anapigiana simu na Jaki zhoka, wakati wenzake wanalounch M4C yeye yupo na akina Ben sanane,akina juliana shonza wanajenga mikakati ya kumpindua mbowe, wakati wenzao wanaamsha maandamano yeye yupo na cloudsfm anaongea dili na ruge kuanzisha kampuni ya PERA ringtones.

In short Zitto ndani ya chadema hana lolote watu ambao wanakijenga chama wanajulikana. Zitto nadhan anajua kucheza na akili za watanzania wajinga ila sio mimi.

nilikuwa nikihitaji mchangiaji makini kama wewe umefunguka vilivyo bigup mkuu asieelewa na hataelewa forever
 
Kabisa,
Na kwa kias kikubwa sana CHADEMA kinapitia wakati mgum sana kwa sasa,asilimia kubwa ya vijana sampuli hiyo wamekimbizia matumain kwa CHADEMA moja kwa moja na kuacha kuhangaika kufanya kazi na kutafuta namna ya kujikwamua na utumwa wa fikra,

Wanadhani kama CHADEMA kikiingia madarakani kitakuwa kinawajaza pesa mifukoni,haitafanya hivyo,

Ikiingia Madarakan kwa ridhaa ya wananchi itachofanya ni kusimamia sera zake na kuahid kile kilichokuwa kinasemwa kwa wananchi,

Wao wanadhani kwa kukaa bila kufanya kazi na kushabikia shabikia basi maisha yao yatabadilika once chadema kikichukua inchi,wanashindwa kuelewa maisha ni haya haya,na kila siku watu wanakufa na kuzaliwa,
Tumaini Makene naomba wewe kama msemaji wa chama uchukue jukumu la kuwakemea hawa waganga njaa na wachumia tumbo wanaodhani kukesha kuwalamba lamba miguu viongoz wa juu wa chama basi itawarahishia maisha hapo baadae,

Mfano ni hawa vijana wababishaji na wenye njaa kali kama Yericko & Saa nane,itoke kauli ya uhakika dhidi ya hawa vijana,

Wanajenga taswira mbovu ya chama ili hali hawana influence yyte na by the way hakuna tuh anaewatambua kwa namna yoyote ile,

Wana kua ni taswira ya chama hali ya kuwa wao wana taswira zao binafsi zilizofifia na kukosa matumain,

Waambie wasitegemee kubebewa na taasis,wajenge identity yao,pia waache ufitini na udanganyifu kwa kutumia nembo ya chama,

WANATIA KICHEFU CHEFU
Mkuu hivi hawa vijana wamekosea wapi?Nimeona comment ya Yericko Hapo juu ambaye ni mwanachama na haina ubaya wowote labda uje useme ni kipi walichoandika kibaya
 
Dah! ina maana Zitto atakuwa kaona chombo sahihi cha kutolea habari kama hizi ni majira? Na kwa nini Habari hii itoke leo wakati bunge linaanza Dodoma? Any way jaalia imetoka kwa bahati nasibu, Hivi tunakumbuka mjada uliokuwa hot kabla ya huu? Wenzangu hamuhisi kwamba mjadala huu umeletwa sasa ili kufunika mjadala wa Sembe ?Kwa nini mjadala huu unakuja baada ya kumalizika mkutano wa CC ya CCM mjini DODOMA? Hivi wenzangu ninyi mmepata fununu kwamba kwenye kikao cha DODOMA; CCM wamekubaliana kubadili mbinu? Any way. ngoja tumsikilize zitto mwenyewe aseme kwanza. Kueni makini kwenye michango yenu kwenye mada hii mnayoitoa kabla ya Zitto mwenyewe hajatokeza humu.
 
Last edited by a moderator:
Why are you out of it?

To him Zito is not trustworthy, so he is waiting 2015 to witness whether or not Zito will abide to what he is uttering now. This is politics bwana, green might be yellow, red might be white at any time. Nothing remains constant and the change is sporadic.
 
Kabisa,
Na kwa kias kikubwa sana CHADEMA kinapitia wakati mgum sana kwa sasa,asilimia kubwa ya vijana sampuli hiyo wamekimbizia matumain kwa CHADEMA moja kwa moja na kuacha kuhangaika kufanya kazi na kutafuta namna ya kujikwamua na utumwa wa fikra,

Wanadhani kama CHADEMA kikiingia madarakani kitakuwa kinawajaza pesa mifukoni,haitafanya hivyo,

Ikiingia Madarakan kwa ridhaa ya wananchi itachofanya ni kusimamia sera zake na kuahid kile kilichokuwa kinasemwa kwa wananchi,

Wao wanadhani kwa kukaa bila kufanya kazi na kushabikia shabikia basi maisha yao yatabadilika once chadema kikichukua inchi,wanashindwa kuelewa maisha ni haya haya,na kila siku watu wanakufa na kuzaliwa,
Tumaini Makene naomba wewe kama msemaji wa chama uchukue jukumu la kuwakemea hawa waganga njaa na wachumia tumbo wanaodhani kukesha kuwalamba lamba miguu viongoz wa juu wa chama basi itawarahishia maisha hapo baadae,

Mfano ni hawa vijana wababishaji na wenye njaa kali kama Yericko & Saa nane,itoke kauli ya uhakika dhidi ya hawa vijana,

Wanajenga taswira mbovu ya chama ili hali hawana influence yyte na by the way hakuna tuh anaewatambua kwa namna yoyote ile,

Wana kua ni taswira ya chama hali ya kuwa wao wana taswira zao binafsi zilizofifia na kukosa matumain,

Waambie wasitegemee kubebewa na taasis,wajenge identity yao,pia waache ufitini na udanganyifu kwa kutumia nembo ya chama,

WANATIA KICHEFU CHEFU

Mkuu THE BIG SHOW umenena na pia vijana wanatakiwa waelewe kuwa wanaweza wakaisaidia jamii bila hata kuwa wanasiasa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom