Zitto: Sijengwi na Kikwete, najijenga mwenyewe

Status
Not open for further replies.
Je,waliwasiliana na Zitto kupata maoni yake kabla hawajachapisha?Je,jamii imetendewa haki?Je, Zitto ametendewa haki?

Kama hawakufanya hivyo,huo uwezo wa kuandika heading na subheading zenye mwelekeo huo zinatoa taswira gani?Hebu tujaribu kuwa analytical kidogo

Hapo uko sawa kabisa mkuu!!! je kama habari iliyoandikwa ingemuhusu Mbowe wasingewasiliana nae kwanza!!!!??
 
Ila hapo hukumuelewa Zitto vizuri. Siyo kwamba Zitto anamshutumu Mbowe kutumia au kuachia gazeti lake limchafue. Zitto alicho kuwa anasema ni kwamba si mara ya kwanza gazeti hilo kufanya hivyo na Mbowe kama mmiliki ana nafasi ya kuwaambia wahariri wake waache kuandika yasiyo ya kweli haswa juu ya mwanachama mwenzake. Tatizo inaelekea kwamba nje ya chama Chadema ni wamoja ila ndani ya chama kuna power struggle kubwa sana imeanza kutokea.

Kweli naungana na kauli yako kwamba ndani ya Chadema kuna 'Power struggle'. Lakini sisi kama wapiga kura wa ZITTTO KABWE, tunahisi Mbunge wetu anataka kufanyiwa kama alivyofanyiwa KAFULILA. tukumbuke Kafulila anatoka Mkoa mmoja na Zitto, sasa wasifike mahala wakawaaminisha Watanzania kuhusu tuhuma dhidi ya Chadema kwamba ni chama cha.......... Hata hivyo sisi wakazi wa Mkoa wa Kigoma bado Rais Jakaya Kikwete ndiye Rais pekee aliyeugeukia Mkoa wa Kigoma kuliko hao wote waliomtangulia. Tutamkumbukla kwa maendeleo angalau kidogo ya Miundo mbinu katika Mkoa wa Kigoma. Kwa maana hiyo Mhe. Zitto kuqambatana na JK sio dhambi ukizingatia Serikali ya Jk imefanya jambo kubwa kwenye jimbo letu la Kigoma Kaskazini. Tuachieni Zitto wetu.
 
Je,waliwasiliana na Zitto kupata maoni yake kabla hawajachapisha?Je,jamii imetendewa haki?Je, Zitto ametendewa haki?Kama hawakufanya hivyo,huo uwezo wa kuandika heading na subheading zenye mwelekeo huo zinatoa taswira gani?Hebu tujaribu kuwa analytical kidogo
Mambo mengine yapo ndani ya wahusika zaidi, simtetei zitto, simtetei mhandishi wa gazeti bt nadhan km mhandishi, mchambuzi wa siasa kuna mambo hayapo sawa, zitto kabwe anaweza akawa anatumika pasipo ya yeye mwenyewe kujijua, anahaki ya kukana bt inabidi a'evaluate nyayo yake na mwenendo wake!
 
Binafsi sijaisoma habari ya Tz Daima na wala hayo malalamiko ya Mh Zitto. Lakini kwani suala la kujengwa (au kubomolewa for that matter) kisiasa ni voluntary kwa kiasi gani? Kama mtu anakufanyia vitu fulani (ambavyo unavikubali) na vitu hivyo vinakupa/kuongezea credentials (political or politically), then suala 'kujengwa' (public opinion) naamini linakuwa involuntary kwa muhusika.

Btw, tatizo hapa ni 'kujengwa' (vs kujijenga) au ni nani anakujenga (in this case JK, a CCM Chairman)? Yaani kama ingeandikwa kwa mfano, Mh Mbowe anamjenga Mh Zitto, bado lingekuwa ni Tatizo?

SMU

Nimependa mtizamo wako. Kujengwa huwezi kukuzuwia kwa upande mmoja lakini kwa kesi ya Zitto angeweza kupunguza walau kama hapendi kujengwa na Kikwete.

Kuandika FB kuwa JK anataka mtu wa rika lake; maneno yaliyosemwa faragha inaonyesha kuwa aliipenda promo ya JK
 
Zitto ni mtoto si ridhiki anapenda sana kukwamisha movement za chadema in any form yuko very strategic,na time bound anajua wakati gani wakuingiza kero na mtafaruku na mwenyekiti wake nakukimbia mbio kwa umma kusick sympathy,mitandao yote imeweka picha zake akiwa Sudan ye mwenyewe kwenye wall yake ya facebook alisema Raisi Kikwete amewaasa yeye na Kafulila wasikubali kuwa na Raisi Mzee na yeye aliandika yuko Sudan ,sasa hata mimi ningekuwa mwandishi ni ngesema anajengwa na JK ,kumhusisha Mbowe na TDaima anatimiza kazi yake aliyoiaanza siku nyingi hawezi kutudanganya ,kwa sababu mambo mengine angemconfront mhariri amsikie anasema nini badala ya kuingiza uongo wa chama,wiki zote tangu bunge lianze tunamuona Zitto front page za Tanzania Daima akiandikwa mambo anayoyofanya bungeni , hatujaona kaweka kwenye FB yake kuuliza kwa nini yuko front page au kumhusidha Mbowe ,huyu ni mtata sana ,ni mgomvi wa asili hapendi amani anachefua sana
 
Nasikitikia sana kwa Zitto kukosa busara. Hivi anasababu gani kuanzisha mijadala kwenye facebook yake ambayo hana hata uwezo wa kuitawala??Alianza kwa kusema kikwete kawaambia yeye na Kafulila kwamba raisi ajaye awe Kijana (nahisi kama yeye) kwa umri. Statement hii moja inaweza kumaanisha kwamba kwa kigezo cha umri amekua "indosed" na JK kuwa mgombea. Hii inatoa ujumbe kwa mgombea aliyepita Dr Slaa kwamba yeye Zitto anastahili kuwa mgombea wa chadema kwani Slaa ni Mkubwa kwa umri( Kwa mujibu wa kikwete).
Aliyoyasema tena leo kuhusu Mtanzania Daima na Mbowe yanaonyesha kwamba kuna tatizo la mawasiliano kati ya Mbowe mwenyekiti wake na yeye jambo ambalo si la manufaa kwa chama chao. Hakuna asiyeona dhahiri kwamba Zitto amekua "favourate" wa watawala na hii imemjengea Kiburi. Kiburi hiki kimemfanya afanye matendo yasiyo ya busara na yasiyojenga chama chake.
My take: Zitto anatumiwa kwa kujua au kwa kutojua na kiburi kinachojengeka ndani yake ndio sumu yake ya kisiasa... I feel that "His arogance is detrimental to his polical carrier"
 
ZITTO ni mzigo mwengine ndani ya Chadema, ni kiongozi anaenunulika kirahisi hana issue, tulidani kajirekebisha kumbe wapi? toka lini na wapi ukamkosoa m/kiti through f/book.... shame on you guy... njaa zitakuponza siitto ni GAMBA ndani ya chadema na Shibuda wake wanatuboa memberz
 
Kweli naungana na kauli yako kwamba ndani ya Chadema kuna 'Power struggle'. Lakini sisi kama wapiga kura wa ZITTTO KABWE, tunahisi Mbunge wetu anataka kufanyiwa kama alivyofanyiwa KAFULILA. tukumbuke Kafulila anatoka Mkoa mmoja na Zitto, sasa wasifike mahala wakawaaminisha Watanzania kuhusu tuhuma dhidi ya Chadema kwamba ni chama cha.......... Hata hivyo sisi wakazi wa Mkoa wa Kigoma bado Rais Jakaya Kikwete ndiye Rais pekee aliyeugeukia Mkoa wa Kigoma kuliko hao wote waliomtangulia. Tutamkumbukla kwa maendeleo angalau kidogo ya Miundo mbinu katika Mkoa wa Kigoma. Kwa maana hiyo Mhe. Zitto kuqambatana na JK sio dhambi ukizingatia Serikali ya Jk imefanya jambo kubwa kwenye jimbo letu la Kigoma Kaskazini. Tuachieni Zitto wetu.
Hicho ndicho Zitto anachokitaka kuonyesha negative picture ya chama chake,anajua wapambe wa Jakaya KIkwete watalivaria njuga swala kama hilo akiweka kwenye wall yake ya Facebook,anajua kabisa kesho Jambo leo,Uhuru,Mtanzania na Habari leo watabeba habari hiyo ukurasa wa mbele tuwaachia Zitto wenu kwani hulka yake ni kuingiza mitafaruku hata pasipohitajika,tumeambiwa Raisi Jakaya Kikwete ememtambulisha Chadema MP kwa Raisi Salva watu mpaka sasa tunajiuliza aliteuliwa na chama chake -mbona waziri kuvuli mambo ya nje asiende ,alichaguliwa na Bunge ,mbona kiongozi wa upinzani Bungeni asiende,alienda kama individual kwa nini awe kwenye government delegation,maswali mengi hayajajibiwa na angeweza kuyaweka wazi kwa vile hayuko sahihi katika safari hiyo sasa anapandikiza picha tofauti kabisa,ana majivuno ya kijinga sana na maono yake ya muda mfupi
 
Zitto anazungukwa, anahadaliwa na wafanyao hvyo ni magamba, asitafute mchawi CDM
 
Zitto alishalalamikia suala hilo hapa JF na kusema kuwa Mbowe anajua. Hakufafanua kuwa walizungumza nae makhsusi au alijuaje.

Lakini gazeti linalomilikiwa na mwentekiti Wa chama linaonekana kuwa credible kwenye mambo yake inayowahusu wanachama hata kama hakuna ukweli huo.

Ikiwa Zitto ameshajadiliana na Mbowe lkn hakuna hatua zilizochukuliwa, kutakuwa na tatizo kubwa na labda ameshindwa njia za kutatua hilo na akaona awaachie wananchi
Gaijin, amelipeleka kwenye vikao vya chama navyo vikashindwa? Nimekuwa kiongozi kwa level fulani though siyo kubwa kama ya Zitto, but kama kuna vitu ambavyo ninakumbuka niliwahi kuonywa, ni namna gani unampresent bosi wako mbele ya jamii. Kiongozi wa juu wa chama ndani ya chama ambacho wewe mwenyewe ni katibu msaidizi huwezi kwenda kumlaumu publicly. Sijawahi kuona hicho kitu kwenye institution yoyote.

Kama Zitto anadhani kwamba anabomolewa au anapigwa vita na Mwenyekiti wake, anayo nafasi ya kuyapeleka malalamiko yake kwenye vikao vya chama. Kama vikao vya chama vimeshindwa, then anayo option moja tu kubwa, kuresign vyeo vyote ndani ya chama na kubaki na kadi tu ya chama kama kweli anakipenda CHADEMA kwa dhati. Na akiona hiyo hailipi, anayo pia nafasi ya kuachana na CHADEMA, Hakuna anayemzuia.

Mbona hatusikii hivi vijembe kutoka kwa akina Mnyika, Lisu, Mkumbo au Slaa? Sijawahi kuona popote pale Slaa, Mnyika au kiongozi mwingine yeyote wa chama akimlaumu kiongozi mwenzake chama kwenye public. Mara nyingi ukiwauliza watakwambia tunakwenda kukaa kwenye vikao vyetu then tutaamua. Sasa huyu Zito ni maadili gani ya uongozi yanayomwelekeza kwamba matatizo ya chama yanatatuliwa na wananchi? Au ndiyo mbinu nyingine ya kukimaliza chama? Ukijenga chuki kati ya wananchi na uongozi wa juu wa chama, wewe utasimama wapi?
 
Katika facebook wall yake, Zito Kabwe amelilaumu gazeti la Tanzania daima kwa kuandika habari inayohusu Zitto kujengwa na Kikwete. Binafsi sina shida na lawama alizolitupia gazeti, kwa kuwa kiuhalisia kwa kuandika hivyo kunawapotezea imani wapinzani dhidi ya Zitto. Hilo naungana naye kwa asilimia nyingi, kwamba Tanzania Daima haikupaswa kuandika hivyo.

Lakini kilichonisikitisha ni kitenda cha Zitto kuweka hoja zake kwa kulihusisha gazeti la Tanzania Daima na Mbowe (mwenyekiti wa CHADEMA). Sidhani kama mhariri wa gazeti anapoihariri habari huwa anampelekea Mbowe aangalie kama habari hiyo inakubalika au haikubaliki. Kwahiyo sioni mantiki ya kuihusisha habari ile moja kwa moja na Mbowe. Na kwa namna nyingine naona kama kauli ya Zitto imelenga kuibua mgogoro mwingine na viongozi wenzake ndani ya chama.
Nawasilisha.

Labda mngesema Zitto anamjenga Kikwete hapo ningewaelewa - Kikwete kwa level yake ilivyoshuka atamjenga mwanasiasa gani? mbona mnataka kumharibia Zitto? na ndiyo maana Zitto anasema mnamfuata fuata sana nyie waandishi wa habari, kupotosha mambo.

Hata mimi ukiniambia najengwa na JK aisee ugomvi wake ni balaa...
 
Spika Kamchagua kwa maelekezo ya Kikwete na yeye
GO9G9056.JPG
 
kwani, mie naomba kuuliza! utaratibu ukoje? Kikwete anavyochagua mtu wa kuambatana nae kwa safari za nje kutoka upinzani, je anawasiliana na chama kuchagua nani aende nae? au anajichagulia tu! kama anajichagulia kwa utashi wake, basi Zitto inabidi ajiulize mara mbili mbili nia na madhumuni haswa ni yapi ya Kikwete! asiwe anafuatanafuatana kila wakati anapoitwa awe na staha ya angalau kumwambia Kikwete wasiliana na chama changu!
 
Gaijin, amelipeleka kwenye vikao vya chama navyo vikashindwa? Nimekuwa kiongozi kwa level fulani though siyo kubwa kama ya Zitto, but kama kuna vitu ambavyo ninakumbuka niliwahi kuonywa, ni namna gani unampresent bosi wako mbele ya jamii. Kiongozi wa juu wa chama ndani ya chama ambacho wewe mwenyewe ni katibu msaidizi huwezi kwenda kumlaumu publicly. Sijawahi kuona hicho kitu kwenye institution yoyote.

Kama Zitto anadhani kwamba anabomolewa au anapigwa vita na Mwenyekiti wake, anayo nafasi ya kuyapeleka malalamiko yake kwenye vikao vya chama. Kama vikao vya chama vimeshindwa, then anayo option moja tu kubwa, kuresign vyeo vyote ndani ya chama na kubaki na kadi tu ya chama kama kweli anakipenda CHADEMA kwa dhati. Na akiona hiyo hailipi, anayo pia nafasi ya kuachana na CHADEMA, Hakuna anayemzuia.

Mbona hatusikii hivi vijembe kutoka kwa akina Mnyika, Lisu, Mkumbo au Slaa? Sijawahi kuona popote pale Slaa, Mnyika au kiongozi mwingine yeyote wa chama akimlaumu kiongozi mwenzake chama kwenye public. Mara nyingi ukiwauliza watakwambia tunakwenda kukaa kwenye vikao vyetu then tutaamua. Sasa huyu Zito ni maadili gani ya uongozi yanayomwelekeza kwamba matatizo ya chama yanatatuliwa na wananchi? Au ndiyo mbinu nyingine ya kukimaliza chama? Ukijenga chuki kati ya wananchi na uongozi wa juu wa chama, wewe utasimama wapi?

Mzee haya si tumeshayamaliza kitambo bado tu mnayarudisha? sasa hizi ndiyo chokochoko zenyewe. Jamani tunarudi nyuma au tunasonga mbele?
 
kwani, mie naomba kuuliza! utaratibu ukoje? Kikwete anavyochagua mtu wa kuambatana nae kwa safari za nje kutoka upinzani, je anawasiliana na chama kuchagua nani aende nae? au anajichagulia tu! kama anajichagulia kwa utashi wake, basi Zitto inabidi ajiulize mara mbili mbili nia na madhumuni haswa ni yapi ya Kikwete! asiwe anafuatanafuatana kila wakati anapoitwa awe na staha ya angalau kumwambia Kikwete wasiliana na chama changu!

Ofisi za bunge ndizo zinazochagua
 
Zitto ni mtoto si ridhiki anapenda sana kukwamisha movement za chadema in any form yuko very strategic,na time bound anajua wakati gani wakuingiza kero na mtafaruku na mwenyekiti wake nakukimbia mbio kwa umma kusick sympathy,mitandao yote imeweka picha zake akiwa Sudan ye mwenyewe kwenye wall yake ya facebook alisema Raisi Kikwete amewaasa yeye na Kafulila wasikubali kuwa na Raisi Mzee na yeye aliandika yuko Sudan ,sasa hata mimi ningekuwa mwandishi ni ngesema anajengwa na JK ,kumhusisha Mbowe na TDaima anatimiza kazi yake aliyoiaanza siku nyingi hawezi kutudanganya ,kwa sababu mambo mengine angemconfront mhariri amsikie anasema nini badala ya kuingiza uongo wa chama,wiki zote tangu bunge lianze tunamuona Zitto front page za Tanzania Daima akiandikwa mambo anayoyofanya bungeni , hatujaona kaweka kwenye FB yake kuuliza kwa nini yuko front page au kumhusidha Mbowe ,huyu ni mtata sana ,ni mgomvi wa asili hapendi amani anachefua sana
Uko sahihi kabisa Froida, gazeti hili la Tz Daima limefanya kazi kubwa sana ya kumjenga Zitto kisiasa, lakini hakuwahi kushukuru popote kwa kazi nzuri ambayo gazeti hili limeifanya dhidi yake. Leo kuandika tu kwamba Kikwete anamjenga, tena kwa kurefer hoja yake mwenyewe ya kwamba Kikwete anamtaka Rais ajaye awe kijana kama yeye, bado amegeuka na kuliona gazeti hili halina jema kwake. Halafu huyu ndiye mwenye ndoto za kuwa Rais, kwa akili hii, sidhani kama anafaa kuwa rais wa nchi. Anaweza kuiingiza nchi vitani huyu. CHADEMA wakitaka kupoteza, basi wampitishe huyu dogo kugombea urais, maana kwa hakika usalama wa taifa hawatakubali nchi ichukuliwe na rais mwenye akili kama hii ya Zito, mara mia bora agombee Mnyika, yuko more grown kuliko huyu Zito. Utoto kwenda mbele.
 
Zitto anazungukwa, anahadaliwa na wafanyao hvyo ni magamba, asitafute mchawi CDM

Nyie mmezidi, juzi niliona Spika Makinda na Lissu wakifungua mziki kule dodoma kwenye ghafla moja hivi, sasa angekuwa Zitto mngesema maneno kibao.
 
Hivi ni kwamba Magambani hakuna vijana mpaka Zitto aone yeye ni zaidi na zaidi kwa Kikwete? Hii tabia ya wanasiasa vijana kujisahau kwa kuwa eti ni vijana ndio kunaleta shida katika harakati za mabadiliko. Toka lini au ni nani amejengwa na JK akanusurika? Zitto nae anadai eti anajijenga mwenyewe, hizo kura anajipigia mwenyewe? Aaaaaagggggggghhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!
 
Gaijin, amelipeleka kwenye vikao vya chama navyo vikashindwa? Nimekuwa kiongozi kwa level fulani though siyo kubwa kama ya Zitto, but kama kuna vitu ambavyo ninakumbuka niliwahi kuonywa, ni namna gani unampresent bosi wako mbele ya jamii. Kiongozi wa juu wa chama ndani ya chama ambacho wewe mwenyewe ni katibu msaidizi huwezi kwenda kumlaumu publicly. Sijawahi kuona hicho kitu kwenye institution yoyote.

Kama Zitto anadhani kwamba anabomolewa au anapigwa vita na Mwenyekiti wake, anayo nafasi ya kuyapeleka malalamiko yake kwenye vikao vya chama. Kama vikao vya chama vimeshindwa, then anayo option moja tu kubwa, kuresign vyeo vyote ndani ya chama na kubaki na kadi tu ya chama kama kweli anakipenda CHADEMA kwa dhati. Na akiona hiyo hailipi, anayo pia nafasi ya kuachana na CHADEMA, Hakuna anayemzuia.

Mbona hatusikii hivi vijembe kutoka kwa akina Mnyika, Lisu, Mkumbo au Slaa? Sijawahi kuona popote pale Slaa, Mnyika au kiongozi mwingine yeyote wa chama akimlaumu kiongozi mwenzake chama kwenye public. Mara nyingi ukiwauliza watakwambia tunakwenda kukaa kwenye vikao vyetu then tutaamua. Sasa huyu Zito ni maadili gani ya uongozi yanayomwelekeza kwamba matatizo ya chama yanatatuliwa na wananchi? Au ndiyo mbinu nyingine ya kukimaliza chama? Ukijenga chuki kati ya wananchi na uongozi wa juu wa chama, wewe utasimama wapi?

Mimi binafsi siku Zitto alipotamka maneno kama hayo ya FB hapa JF, nilimpinga kuwa uongozi hawendi hivyo. Ila inaonyesha tatizo limekuwa sugu.

Juu ya hivyo twende hypothetical tu kwanza, tuseme Zitto amelalama kwenye chama na hatua hazijachukuliwa, ushauri wako wa kuwa yeye ajiuzulu wadhifa au ahame chama naona si sahihi. Ni sawa na kumtaka Zitto awe selfless wakati watu wengine wako more than selfish kwake.

Kwangu nadhani tatizo kubwa limejitokeza baada ya Zitto kupigiwa kura ya kutokuwa na imani pale Bagamoyo. Hapa tena tunamtaka awe selfless, asiweke kinyongo na afanye kazi na watu ndani ya chama vizuri, lakini kibinaadamu ngumu. Na ndio maana anaonekana mambo mengi sasa anafanya kivyake tu (ndio kujijenga mwenyewe?)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom