Mkuu Kitila, nakubaliana na wewe kuwa watu ni too sensitive, lakini natofautiana nawe kuwa maoni ya Zitto hayakuwa na tatizo. Lau kama angekomea kweny neno Jambo leo isingekuwa na shida, kuendelea na kumtaja kiongozi wa chama chake ilikuwa ni direct implication ya maudhui ya gazeti na mmiliki vikiunganishwa na Chama."Tanzania Daima Leo habari yao kuu ni 'Kikwete amjenga Zitto'. Nisingeshangaa Kama habari hii ya kizushi ingetoka Jamboleo. Nashangaa habari hii kuandikwa na gazeti linalomilikiwa na Kiongozi Mkuu wa Chama changu. Sijengwi na mtu, NINAJIJENGA!"
Nimeyapitia tena maoni ya Zitto kwenye Facebook kama nilivyoyanukuu hapo juu. Labda upeo wangu wa kuona mambo ni mdogo, lakini sijaona ni namna gani maoni haya ni tatizo kwa chama kama wengine wanavyodai. I think some colleagues here are just too sensitive with what Zitto says and does! Ni mara ngapi Tanzania Daima wameandika habari ambazo ukisoma huamini kwamba ni Gazeti linalomilikiwa na Kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani? Sasa kulishangaa Gazeti linalomilikuwa na Kiongozi wa chama upinzani kwa kuandika habari za kiaina haina maana moja kwa moja kwamba unamshangaa kiongozi huyo, unalishangaa gazeti!!
Katika facebook wall yake, Zito Kabwe amelilaumu gazeti la Tanzania daima kwa kuandika habari inayohusu Zitto kujengwa na Kikwete. Binafsi sina shida na lawama alizolitupia gazeti, kwa kuwa kiuhalisia kwa kuandika hivyo kunawapotezea imani wapinzani dhidi ya Zitto. Hilo naungana naye kwa asilimia nyingi, kwamba Tanzania Daima haikupaswa kuandika hivyo.
Lakini kilichonisikitisha ni kitenda cha Zitto kuweka hoja zake kwa kulihusisha gazeti la Tanzania Daima na Mbowe (mwenyekiti wa CHADEMA). Sidhani kama mhariri wa gazeti anapoihariri habari huwa anampelekea Mbowe aangalie kama habari hiyo inakubalika au haikubaliki. Kwahiyo sioni mantiki ya kuihusisha habari ile moja kwa moja na Mbowe. Na kwa namna nyingine naona kama kauli ya Zitto imelenga kuibua mgogoro mwingine na viongozi wenzake ndani ya chama.
Nawasilisha.
Hivi kwa ukaribu alionao Zito na Rais Kikwete atashindwa kweli kuwa anampatia mikakati ya Chadema kuiondoa CCM madarakani?, am so afraid with this guy.
Bwana mdogo mbona alishaisha huyu
mimi nilipomuona tu amaeanza kuendesha yale magari ya zamani ya wanajeshi wa wakimarekani nikajua oooh tayari kisha zimishwa na wajanja!
Bwana mdogo mbona alishaisha huyu
mimi nilipomuona tu amaeanza kuendesha yale magari ya zamani ya wanajeshi wa wakimarekani nikajua oooh tayari kisha zimishwa na wajanja!