Zitto matatani tena

saidi kindole

JF-Expert Member
Sep 21, 2012
310
792
Mabilioni ya Uswisi yamtia hatiani, anusurika kulimwa faini ya Sh bilioni 8
*Ni kwa kumtuhumu mfanyabiashara kutoa rushwa kwa vigogo serikalini

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara nyingine ameingia matatani baada ya kushindwa kesi iliyofunguliwa na mfanyabiashara raia wa Afrika Kusini.

Katika kesi hiyo, Zitto alituhumiwa kutoa madai kupitia tovuti yake
Zitto na Demokrasia | Zitto na Demokrasia kuwa mlalamikaji, Moto Mabanga alitoa rushwa ya mabilioni ya fedha kwa maofisa wa Serikali ya Tanzania ili kufanikisha kampuni ya Ophir Energy kupata vitalu vitatu vya gesi mkoani Mtwara kati ya mwaka 2004/2005.

Katika kesi hiyo ya madai Namba 153 ya 2013 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara huyo pamoja na mambo mengine alidai kulipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 5 ambazo ni sawa na Sh bilioni 8 za Tanzania.

Katika hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Sundi Fimbo, Novemba 21 mwaka huu bila Zitto kuwapo, Mahakama ilijiridhisha kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye tovuti binafsi ya Zitto na kwenye mitandao ya jamii yalimkashifu mlalamikaji na mlalamikiwa ameshindwa kuyathibitisha.

Mahakama hiyo imemtaka Zitto kuomba radhi kwenye tovuti yake na mitandao ya jamii ambako aliandika kashfa dhidi ya mfanyabiashara huyo.

Pia imemuamuru mlalamikiwa pamoja na washirika wake kuacha kwa njia yoyote ile kuendelea kuandika na kusambaza habari zenye kumkashifu mlalamikaji.

Mwanasiasa huyo kijana ambaye katika siku za karibu amekumbwa na misukosuko ya kisiasa, pia ameamriwa kumlipa mlalamikaji jumla ya Sh milioni 3 kutokana na madhara yaliyotokana na kashfa husika.

Awali, mlalamikaji alitaka kulipwa Dola za Marekani milioni 5, lakini akashindwa kuithibitishia Mahakama ni jinsi gani alipata hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kashfa hiyo. Pia Zitto ametakiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Alipoulizwa jana kama anakubaliana na hukumu hiyo au anakusudia kukata rufaa, Zitto alijibu kwa ufupi; "Sijaona hukumu wala sijawahi kufika mahakamani."

Julai mwaka jana, Mabanga alifikisha malalamiko mahakamani akidai Zitto ameandika taarifa zenye kumkashifu kwa kumhusisha na utoaji mkubwa wa rushwa.

Mbali na kujihusisha na biashara sehemu mbalimbali duniani, Mabanga amekuwa akitumika kama kiunganishi kati ya wawekezaji wakubwa na Serikali mbalimbali ikiwamo Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika madai yake, aliitaka Mahakama kumuamuru Zitto kutoka uthibitisho dhidi ya madai ya kuwapa rushwa maofisa wa Serikali katika mchakato wa kupata vitalu vya gesi wa kampuni ya Ophir Energy.

Pia aliiomba Mahakama kutamka kuwa maneno yaliyoandikwa na Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha kwenye tovuti yake na mitandao ya jamii si ya kweli bali ni kashfa.

Wakati hali ikiwa hivyo, wiki mbili zilizopita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilimvua nyadhifa zote Zitto Kabwe ikiwamo ile ya Naibu Katibu Mkuu.

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya Chadema uliofanyika Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu, alisema Zitto na wenzake wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha mpango unaoitwa Mkakati 2013 ukilenga kukisambaratisha chama hicho, ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake.

Wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, ambapo walipewa siku 14 wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwamo kuvuliwa uanachama.

source: Raia Mwema
 
hii ndiyo ile miaka mibaya, mtu unapanda mchicha inaota mibange!!! duh
 
zitto ndio kaisha kabisa.... Yaani sasa anakimavi usoni system imemshusha kuzimu ili aone uharisia wa maisha ya usaliti yalivyo: Ukipanda unafiki unavuna unaviki tu.

Kwaheri zitto kalime mawesse.
 
Mahakama baba, tunaomba mumsitiri kidogo huyo kijana, ni utoto na Ulimbukeni tu ndio unaomsumbua. Pandikizi mwenzie, Dr. Fuatamkumbo ndo yameshamkuta huko kibaruani kwake, sijui ule mchango kwa ajili ya M2 na M3 wataupata wapi!
 
Ndo huyo CCM wanataka awe Mwenyekiti wa Chadema? Kweli Chadema milifanya kazi nzuri sana kumuona huyu jamaa mapema. Sasa hivi CCM wanahangaika na matamko ya kitoto kitoto tu. Hii inaweza kuwageuka CCM na kuanza kuwala wenyewe
 
Mabilioni ya Uswisi yamtia hatiani, anusurika kulimwa faini ya Sh bilioni 8
*Ni kwa kumtuhumu mfanyabiashara kutoa rushwa kwa vigogo serikalini

zkabwe.jpg
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), kwa mara nyingine ameingia matatani baada ya kushindwa kesi iliyofunguliwa na mfanyabiashara raia wa Afrika Kusini.

Katika kesi hiyo, Zitto alituhumiwa kutoa madai kupitia tovuti yake
Zitto na Demokrasia | Zitto na Demokrasia kuwa mlalamikaji, Moto Mabanga alitoa rushwa ya mabilioni ya fedha kwa maofisa wa Serikali ya Tanzania ili kufanikisha kampuni ya Ophir Energy kupata vitalu vitatu vya gesi mkoani Mtwara kati ya mwaka 2004/2005.

Katika kesi hiyo ya madai Namba 153 ya 2013 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, mfanyabiashara huyo pamoja na mambo mengine alidai kulipwa fidia ya Dola za Marekani milioni 5 ambazo ni sawa na Sh bilioni 8 za Tanzania.

Katika hukumu iliyotolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Sundi Fimbo, Novemba 21 mwaka huu bila Zitto kuwapo, Mahakama ilijiridhisha kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye tovuti binafsi ya Zitto na kwenye mitandao ya jamii yalimkashifu mlalamikaji na mlalamikiwa ameshindwa kuyathibitisha.

Mahakama hiyo imemtaka Zitto kuomba radhi kwenye tovuti yake na mitandao ya jamii ambako aliandika kashfa dhidi ya mfanyabiashara huyo.

Pia imemuamuru mlalamikiwa pamoja na washirika wake kuacha kwa njia yoyote ile kuendelea kuandika na kusambaza habari zenye kumkashifu mlalamikaji.

Mwanasiasa huyo kijana ambaye katika siku za karibu amekumbwa na misukosuko ya kisiasa, pia ameamriwa kumlipa mlalamikaji jumla ya Sh milioni 3 kutokana na madhara yaliyotokana na kashfa husika.

Awali, mlalamikaji alitaka kulipwa Dola za Marekani milioni 5, lakini akashindwa kuithibitishia Mahakama ni jinsi gani alipata hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kashfa hiyo. Pia Zitto ametakiwa kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Alipoulizwa jana kama anakubaliana na hukumu hiyo au anakusudia kukata rufaa, Zitto alijibu kwa ufupi; "Sijaona hukumu wala sijawahi kufika mahakamani."

Julai mwaka jana, Mabanga alifikisha malalamiko mahakamani akidai Zitto ameandika taarifa zenye kumkashifu kwa kumhusisha na utoaji mkubwa wa rushwa.

Mbali na kujihusisha na biashara sehemu mbalimbali duniani, Mabanga amekuwa akitumika kama kiunganishi kati ya wawekezaji wakubwa na Serikali mbalimbali ikiwamo Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Katika madai yake, aliitaka Mahakama kumuamuru Zitto kutoka uthibitisho dhidi ya madai ya kuwapa rushwa maofisa wa Serikali katika mchakato wa kupata vitalu vya gesi wa kampuni ya Ophir Energy.

Pia aliiomba Mahakama kutamka kuwa maneno yaliyoandikwa na Zitto ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Fedha kwenye tovuti yake na mitandao ya jamii si ya kweli bali ni kashfa.

Wakati hali ikiwa hivyo, wiki mbili zilizopita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilimvua nyadhifa zote Zitto Kabwe ikiwamo ile ya Naibu Katibu Mkuu.

Katika mkutano wa Kamati Kuu ya Chadema uliofanyika Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Tundu Lissu, alisema Zitto na wenzake wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha mpango unaoitwa Mkakati 2013 ukilenga kukisambaratisha chama hicho, ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake.

Wengine waliovuliwa nyadhifa zao ni pamoja Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, ambapo walipewa siku 14 wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwamo kuvuliwa uanachama.

source: Raia Mwema
Hivi kuna correlation yoyote kati ya aya hizo mbili zenye maneno niliyo-bold hapo juu kweli? Au ndio waandishi makanjanja hawa, wenye vyeti vya Division 5 lakini baada ya miezi 3 unawasikia wakijiita Waandishi wa Habari? Sijawahi kuona nchi yenye vilaza kama hii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Zitto ana kiherehere sana ndo tabu yake...angekuwa mrefu sijui ingekuwaje
 
...hili toto ongo sana,kwanza hata hiyo hukumu imechakachuliwa angepigwa faini ya bilioni moja angalau ingekuwa sawa...
 
Dogo bora ameondolewa CDM make hii ilikuwa ni aibu ya nyingine kwa chama kwa ujiko wa mwehu mmoja,sifa zimemmaliza zitto sasa anaanza kuikashifu serikali eti maafisa wamehongwa wakati ushaidi hana ...umeidharirisha serikali ya JK

Safari imeanza kaka,wahi mapema ukavue migebuka
 
Mabilioni ya Uswisi yamtia hatiani, anusurika kulimwa faini ya Sh bilioni 8
*Ni kwa kumtuhumu mfanyabiashara kutoa rushwa kwa vigogo serikalini

source: Raia Mwema

Weka Raia mwema ya lini? na Namba gani ? au Unganisha link ili taarifa iwe ya uhakika.
 
CDM bila zitto haiwezekani..........!!!!!!!!!
hamuwezi kumpa zitto tuhuma za kitoto namna iyo,anafahamika ni mtanzania wa kweli,hayupo kicham,yupo ki-Tanzania zaidi,,,
hata ccm wana-mhanya,kama kunasehemu cdm mmkosea kufukuza ni kwa zitto...........
shame on cdm
 
zitto ndio kaisha kabisa.... Yaani sasa anakimavi usoni system imemshusha kuzimu ili aone uharisia wa maisha ya usaliti yalivyo: Ukipanda unafiki unavuna unaviki tu.

Kwaheri zitto kalime mawesse.

haya ndo madhara ya kuwa msaliti,unapokuwa vitani unapambana na adui then,adui anakurubuni na unaanza kuua askari wenzako,mwisho wa yote huyo adui atakuua hata wewe,kwani wewe sio mmoja wake,wewe ni kama toilet paper tu,ukishatumiwa kuchambiwa unatupwa.the system has aborted him.kwishneyyyyyy
 
CDM bila zitto haiwezekani..........!!!!!!!!!
hamuwezi kumpa zitto tuhuma za kitoto namna iyo,anafahamika ni mtanzania wa kweli,hayupo kicham,yupo ki-Tanzania zaidi,,,
hata ccm wana-mhanya,kama kunasehemu cdm mmkosea kufukuza ni kwa zitto...........
shame on cdm

CDM ni mpango wa Mungu.Yeyote anaeuvuruga lazima apate Mapigo.CC.DR.Kitila Mkumbo.
 
ujuaji unamponza, watu wa namna ya zito uzeeni huwa wanakuwa wachawi, nyie suburini
 
Ukimkana Zitto, umeukana uzalendo wako. Siasa ni mchezo mchafu. Madudu ya nchi hii huonekana kwa jicho pevu. Anayeitwa msaliti Tanzania, ndiye msemakweli kwa critical thinkers. Think Big to Get Big results. Zitto ni mwiba kwa Chadema, Mafisadi na Serikali kwa ujumla. Kwa namna yoyote, mabadiliko ndani ya Chadema yanahitajika. Hakuna demokrasia ya kweli. Kama Chadema kitachukua dola kabla ya mabadiliko hayo, nchi itakuwa imepotea.
 
Back
Top Bottom