Zitto: Maelezo ya Waziri na Naibu wake sio ya kweli (Audio)

Oct 26, 2010
26
14
Wizara hazina huwajibikaji kabisa. Waziri anamiliki Tanpower Resources halafu anawaambia Stamico wasilipe deni hili kampuni yake iweze kuchukua tenda. Huyu aende na maji tu.

Ufafanuzi:
Anayetajwa hapa si Waziri wa sasa ni Daniel Yona, alipokua Waziri wa Nishati na Madini, na alikua yeye na familia yake wakimiliki kampuni ya Tanpower Resources Ltd, akiwa na ubia na Benjamin Mkapa na familia yake. Kampuni iliyopewa umiliki wa Kiwira Coal Limited. Mpaka baadae ameifilisi kampuni yake ya Anbem Ltd, akimwacha mwanae hadi sasa katika umiliki wa kampuni hizo.

Mawaziri wa sasa wanazuga kuwa hawajui.
 
Attachments

  • Zito.mp3
    2.7 MB · Views: 1,070
Natamani tuwaombe WACHINA watuazime sheria zao za kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa wiki moja tu tuzitumie hapa nchini kusafisha hawa mafisadi wa CCM. Mwalimu Nyerere alithubutu kutuwekea FAGIO LA CHUMA lakini huyu m.kwere anawabembeleza hawa mabazazi????
 
ahsante nimeisikia Zito yuko makini je unaweza attach mp3 nyingine za bungeni leo kwani hapa nilipo siwezi pata matangazo hata streaming inakataa kwenye arusha mambo
 
Natamani tuwaombe WACHINA watuazime sheria zao za kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa wiki moja tu tuzitumie hapa nchini kusafisha hawa mafisadi wa CCM. Mwalimu Nyerere alithubutu kutuwekea FAGIO LA CHUMA lakini huyu m.kwere anawabembeleza hawa mabazazi????

Hapana kwa sheria za china na mimi nitamkosa baba yangu..... kunyongwa!!!!!!!!

pole pole jamani ni heri afungwe kifungo cha maisha nitaweza kumtembelea gerezani
 
Kwa sasa hakuna Kama ZITTO.Hongereni sana Kigoma Kaskazini kwa kutuletea Heavy duty machine
 
Natamani tuwaombe WACHINA watuazime sheria zao za kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa wiki moja tu tuzitumie hapa nchini kusafisha hawa mafisadi wa CCM. Mwalimu Nyerere alithubutu kutuwekea FAGIO LA CHUMA lakini huyu m.kwere anawabembeleza hawa mabazazi????

Comrade wiki moja ni kubwa sana siku tatu tu zitatutosha waliobaki watajimaliza wenyewe hovyo sana hawa mabwana
 
Wako wengi wa hivyo na huenda si waziri mwenye kufanya uchafu huo pekee yake

Huenda mawaziri wengi wapo hivyo wanaiba na hawawezi kuwajibishwa na TAKUKURU wala uongozi wowote wa wilaya au mkoa husika
 
Hata wewe unatakiwa pia kupata hiyo adhabu coz ni mfaidika wa huo uozo!
 
Uozo ni mkubwa Serikalini miwaziri imekalia posho za vikao tu na kuwaacha watumishi wakifanya wanavyotaka. I can real see some light at the end of the Tunnel.... RIP CCM
 
Natamani tuwaombe WACHINA watuazime sheria zao za kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa wiki moja tu tuzitumie hapa nchini kusafisha hawa mafisadi wa CCM. Mwalimu Nyerere alithubutu kutuwekea FAGIO LA CHUMA lakini huyu m.kwere anawabembeleza hawa mabazazi????

wiki moja haitatosha kuwaondoa mafisadi wote
 
Suala la Kabulo kwa kweli ni zito na Zitto anasema kweli na kwa kweli Spika naye anasema kweli kwamba hili sualai "zito" na hivyo anaomba apelekewe upya kusiwapo longolongo kwamba zimepotea. Kwa kifupi Kabulo Mkapa na Yona walijigawia rasilimali zetu na leo tunamuone huruma. Yess Mkapa amefanya mazuri mengi katika nchi hii, lkini katika hili amekosea na kama anataka aombe radhi na alipe fidia si kulipwa 9bn
 
Natamani tuwaombe WACHINA watuazime sheria zao za kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa wiki moja tu tuzitumie hapa nchini kusafisha hawa mafisadi wa CCM. Mwalimu Nyerere alithubutu kutuwekea FAGIO LA CHUMA lakini huyu m.kwere anawabembeleza hawa mabazazi????

anakula nao
 
kwakweli nawapongeza sana wananchi waliotuchagulia mbunge zito, maana kazi yake tunaiona. na inafaa tuingize maoni ya mabadiliko ya katiba ili kipengele cha umri kirekebishwe ili vijana kama hawa wasaidie nchi.
 
Natamani tuwaombe WACHINA watuazime sheria zao za kupambana na rushwa na ufisadi hata kwa wiki moja tu tuzitumie hapa nchini kusafisha hawa mafisadi wa CCM. Mwalimu Nyerere alithubutu kutuwekea FAGIO LA CHUMA lakini huyu m.kwere anawabembeleza hawa mabazazi????

Mkuu, fagio la chuma aliliasisi Ali Hassan Mwinyi. Nakukumbusha tu.
 
Back
Top Bottom