Zitto Kabwe: Tanzania tunafanya Mijadala duni sana. Ni watu Wachache sana wenye uwezo wa kuchambua na kujenga hoja!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,977
141,988
Akizungumza kwenye kumbukizi la Mwalimu Nyerere KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema Tanzania ina Mijadala duni sana ndio sababu tumekwama kwenye kila jambo na kubaki tunazunguka pale pale.

Zitto amesema wapo vijana wachache sana wenye uwezo wa kuchambua na kujenga hoja ambao siyo Chawa hivyo amewaomba vijana hao waendeleze mijadala hata kama wana mawazo tofauti.

Source: ITV
 
Yeye mwenyewe hana hoja zaidi ya kumlamba viatu January.
Zitto ni mtu wa ajabu
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Kujadili ,kujenga hoja ,kuhoji ni swala la kufundishwa hauwezi ukaamka tuu na kuanza kujenga hoja na kujadili.

Swali ni , Je Tunafundisha namna ya kujenga hoja na kujadili?
 
Vijana wa nchi hii wameishia kwenye kutunga verse za Bongoflavour kila mmoja amenyoa kiduku na kuacha virasta uchwara.

Wanawaza mapenzi huku wakitembea suruali zikiwashinda kukaa viunoni.

Sasa wengi wanavaa kaptula na Sandals maana ndizo nyepesi.

Mawazo na fikra wameuza huko Google! Kupitia smartphone.

Hesabu wapiga kwa Calculator za Simu...hata salamu kwa wakubwa zinawashinda.

Tanzania ya kesho itachekesha sana.
 
Akizungumza kwenye kumbukizi la Mwalimu Nyerere KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema Tanzania ina Mijadala duni sana ndio sababu tumekwama kwenye kila jambo na kubaki tunazunguka pale pale.

Zitto amesema wapo vijana wachache sana wenye uwezo wa kuchambua na kujenga hoja ambao siyo Chawa hivyo amewaomba vijana hao waendeleze mijadala hata kama wana mawazo tofauti.

Source: ITV
Hilo ni kweli kabisa. Vijana wanakurupuka sana. Mambo ya udaku ndiyo yanapendwa kuliko mambo yenye tija.
 
Chama cha kijani ndio kimeua uwezo wa vijana kujenga hoja..mana kinaongozwa na viongozi waliojaa vioja na njaa kwenye bongo zao..hivyo hukimbilia kwenye vyombo vya dola kuua na kuangamiza vijana wenye hoja.

Lawama zote ziende kwenye chama cha kijani.

#MaendeleoHayanaChama
 
K
Kujadili ,kujenga hoja ,kuhoji ni swala la kufundishwa hauwezi ukaamka tuu na kuanza kujenga hoja na kujadili.

Swali ni , Je Tunafundisha namna ya kujenga hoja na kujadili?
Kwani uchawa unafundishwa?Acheni uchawa tumieni IQ zenu vizuri.
 
Akizungumza kwenye kumbukizi la Mwalimu Nyerere KC wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema Tanzania ina Mijadala duni sana ndio sababu tumekwama kwenye kila jambo na kubaki tunazunguka pale pale.

Zitto amesema wapo vijana wachache sana wenye uwezo wa kuchambua na kujenga hoja ambao siyo Chawa hivyo amewaomba vijana hao waendeleze mijadala hata kama wana mawazo tofauti.

Source: ITV
Kauli kwamba 'Tanzania ina mijadala duni' inamaanisha hata anachokisema yeye ni duni. Kwa nini sasa tumsikilize? Au anaona yeye peke yake yuko juu mawinguni na sisi wengine tuko ardhini? Hata kama ni hivyo, kwa kuwa naye ni Mtanzania basi tuko naye chungu kimoja isipokuwa kama anaukataa Utanzania.
 
Back
Top Bottom