Elections 2010 Zitto kabwe kawasaliti CHADEMA kigoma?

sisi wana wa kigoma tunachagua mtu mwenye uwezo na sio kwa sababu ati zitto kasema.....................umeona jimboni kwake walivyoshikana mashati na yule jamaa wa ccm.....na kama si kuchakachua basi alley wa chadema angeshinda kigoma mjini.

Sasa kaka una hakika Slaa hana uwezo? japo waamuzi ni ninyi lakini pia tunaweza kupima maamuzi yenu na vigezo kama ni scientific au vipi? Zitto alishachakachuliwa belive it or not.
 
Mugo"The Great";1216829 said:
Mwanzilishi wa post hii si mkweli na inaonekana ana chuki na Zitto Kabwe. Ni ukweli usiofichika kuwa NCCR ina nguvu sana Kigoma hasa Kasulu na Nguruka. Dada Agripina Zai wa Kasulu vijijini si mpambanaji wa leo amekuwepo tangu changuzi za nyuma ila uchakachuaji ndiyo ilikuwa issue kubwa. Hivi wewe uliyeanzisha post hii unaijua Kigoma na politics zake? I doubt. NCCR ilikuwa na nguvu hata kabla Nsanzugwanko hajaihama na kuingia sisiemu.

Sio Chuki katoa hoja mjibuni, unajua watanzania sasa hivi wanaona vizuri ni vigumu kuwapiga changa la macho. issue kwa nini yeye kama mjumbe wa Chadema Slaa kaanguka saana kwake?
 
I will come back to you after four years to see if Zitto Kabwe is still your favorable.
 
Kitu ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba umaarufu wa Zitto ulikwisha siku nyingi. Yeye alishakuwa wa upande wa pili look at the life style and arrogance. Tatizo la wapiga debe wengi ni njaa zao ndo zinazowapigisha kelele wazalendo ni wachache utabaki na akina nyerere na wengine wachache. Pale tu tutakapo weza kuleta usawa wa kimaisha ndipo tutaongea ukweli na kuusimamia
 
Labda ucaguzi huu utawafanya Watanzania muanze muwafahamu Waha, kabila lililo kubwa mkoani Kigoma na ambalo limesahaulika kabisa tangia zama za mkoloni, na tangu Uhuru wa Tanganyika. Kigoma wakiisha toa uamuzi, hawabadiliki badiliki kama bendera inayofuata upepo. Msingi wa NCCR-Mageuzi Kigoma Kusini ulijengwa na Kiffu Hussein Kiffu. Kiffu akanunuliwa na CCM, Waha wakamwambia nenda peke yako. Aligombea udiwani mara alipohamia CCM akanyimwa kura. Kipindi hicho Ruhuza alikuwa Kigoma akiongezea nguvu alizozikuta. Kafulila alipoondoka Chadema kwenda NCCR alifuata wananchi na wala siyo kwamba amechukua wana Chadema. Kasulu Vijijini nako huyo IRON LADY Agripina Zaituni Buyogera amejenga ngome imara sana (at grassroot level) ya NCCR-Mageuzi ambayo ilinyakua Serikali nyingi za Mitaa mwaka jana. Nguvu hiyo ya Iron Lady Buyogera ndiyo imezickua kata kadhaa za Kasulu na Kibondo pamoja na Majimbo matatu. Zitto Kabwe alielekeza nguvu zake Kigoma Mjini na Manyovu, majimbo ambayo Chadema imefanya vizuri sana na kwa Kigoma Mjini, wananchi wanaamini Chadema imeshinda lakini kura zao zikaibiwa. Aliyeshinda Jimbo la Manyovu Albert Ntabaliba anajua nguvu alizopambana nazo ikiwa ni panoja na Halmashauri ya Kasulu kutawaliwa na NCCR-Mageuzi na Chadema. Zitto Kabwe hajakisaliti chama cha CHadema. Hiyo ndiyo Kigoma, mkoa ambao haufifiki hasa baada ya Serikali kuua Reli ya Kati. Ninaamini kuwa NCCR-Mageuzi itaona umuhimu wa kuwa na Mwenyekiti mpya MWANAMKE ambaye amewezesha kupata viti vya ubunge vitatu. Kiffu wa CCM arudi nyumbani kwake NCCR kuendeleza Mageuzi. WAHA wameonyesha njia, Watanzania mko wapi?
 
Kama ni kweli Dr. Slaa amepata kura kidogo Kigoma, basi ni kweli kuna wizi wa kutisha wa kura. Hata wanaCCM Kigoma wamemchagua Dr. Slaa, licha ya NCCR wote na Cadema wote! Dr. Slaa awe na kura chache Kigoma? Basi hii ni hatari ya danger!
 
Kumbuka pia hata Dr alisema akishinda angechukua watu makini kutoka ccm pia,swala linaongaliwa hapo ni competence zaidi.
 
Kumbuka pia watanzania wengi sasa hivi wamefugua amcho hawachagui vyama wanaangali anani atatufaa au nani kafanya nini kwao. Uliza siri ya Prof. Tibaijuka kushinda kwa kishindd. Ni matokeo ya kazi zake. ZInaonekana sio maneno tuu
 
Labda ucaguzi huu utawafanya Watanzania muanze muwafahamu Waha, kabila lililo kubwa mkoani Kigoma na ambalo limesahaulika kabisa tangia zama za mkoloni, na tangu Uhuru wa Tanganyika. Kigoma wakiisha toa uamuzi, hawabadiliki badiliki kama bendera inayofuata upepo. Msingi wa NCCR-Mageuzi Kigoma Kusini ulijengwa na Kiffu Hussein Kiffu. Kiffu akanunuliwa na CCM, Waha wakamwambia nenda peke yako. Aligombea udiwani mara alipohamia CCM akanyimwa kura. Kipindi hicho Ruhuza alikuwa Kigoma akiongezea nguvu alizozikuta. Kafulila alipoondoka Chadema kwenda NCCR alifuata wananchi na wala siyo kwamba amechukua wana Chadema. Kasulu Vijijini nako huyo IRON LADY Agripina Zaituni Buyogera amejenga ngome imara sana (at grassroot level) ya NCCR-Mageuzi ambayo ilinyakua Serikali nyingi za Mitaa mwaka jana. Nguvu hiyo ya Iron Lady Buyogera ndiyo imezickua kata kadhaa za Kasulu na Kibondo pamoja na Majimbo matatu. Zitto Kabwe alielekeza nguvu zake Kigoma Mjini na Manyovu, majimbo ambayo Chadema imefanya vizuri sana na kwa Kigoma Mjini, wananchi wanaamini Chadema imeshinda lakini kura zao zikaibiwa. Aliyeshinda Jimbo la Manyovu Albert Ntabaliba anajua nguvu alizopambana nazo ikiwa ni panoja na Halmashauri ya Kasulu kutawaliwa na NCCR-Mageuzi na Chadema. Zitto Kabwe hajakisaliti chama cha CHadema. Hiyo ndiyo Kigoma, mkoa ambao haufifiki hasa baada ya Serikali kuua Reli ya Kati. Ninaamini kuwa NCCR-Mageuzi itaona umuhimu wa kuwa na Mwenyekiti mpya MWANAMKE ambaye amewezesha kupata viti vya ubunge vitatu. Kiffu wa CCM arudi nyumbani kwake NCCR kuendeleza Mageuzi. WAHA wameonyesha njia, Watanzania mko wapi?
well said
 
Sio Chuki katoa hoja mjibuni, unajua watanzania sasa hivi wanaona vizuri ni vigumu kuwapiga changa la macho. issue kwa nini yeye kama mjumbe wa Chadema Slaa kaanguka saana kwake?

kmechakachuliwa mfano kigoma mjini
 
zito ni jukumu lake kuhakikisha wabunge wengi zaidi wa chadema wanaingia bungen ili kuongeza ruzuku kwa chama na kukiimarisha cham tayari kwa 2015.........(kwa bara ikiwezekana kiti kichukuliwe na chadema basi iwe ivyo ila ikishindikana wengine wa upinzani wachukue...upinzani wote tunaupenda lakini kwa sasa chama ambacho hakijachakachuliwa na ccm ni chadema ambacho tunaamini wasomi wa kweli wote wanapeleka nguvu huko ili 2015 tuongee lugha moja....kwa umaarufu alionao zito naamini angeweza kukisaidia sana chama zaidi ya alivyofanya kwa kigoma na kasulu...... na kwa urafiki wa karibu na kafulila na machari (ambao walikuwa chadema wakatolewa kwa utovu wa nidhamu)ambao wote wamechukua majimbo kwa tiketi ya nccr pale kasulu haina ubishi amekuwa akiwa support kwa nguvu zote.........ningeweza kutoa ushaidi wa kina kwa ninayoyasema ili zitoe vielelezo zaidi lakini haitakuwa na maana kama tutanza kukosoana wenyewe kwa wenyewe wakati wote lengo ni kumtoa nduli amin(ccm).
Imekuwa wazi kwa chadema kwamba zito ametaka kuyumbisha chama si chini ya mara 2 kwa miaka 5 iliyopita kwa umaarufu wake.......na ccm si wajinga wameshaona hali na wanatafuta pa kuingilia ndani ya chadema kwa hii miaka mitano inyokuja......na sitashangaa kama watapitia kwa zito na mwisho chadema kuwa kama nccr......
Ni ukweli usiopingika zito amefanya makubwa kwa chadema na hasa kipindi cha mwanzo cha uteuzi wake lakini kama mwanadamu mwingine amekuwa na mapungufu yake aidha kwa kuanza kuitwaitwa na ccm au kwa kutojua ....kuanza kwenda tofauti na wenzake ndan ya chama kwenye kamati walizopewa kuongoza.........Namuomba kama ataona ujumbe huu.... na atulie na arudi kuwa zito wa mwanzo...ama chadema hawatamvumilia kama walivyofanya kwa marafiki zake kina kafulila na machali......ccm wameshajeruhiwa na wanakisaka sana chadema kwa nguvu yoyote ile na kama ataanza kutokuwa na msimamo wa chama atatuyumbisha washabiki wa chadema na 2015 kupotezwa kama ilivyokuwa nccr......ni vyema akaongea lugha moja sambamba na wakuu wake....dr slaa na mbowe pamoja na wengine!
kina slaa naomba wamvumilie na kumuonya kama mtoto wao ili awe na msimamo na asiyumbishwe na hasa kipindi hiki ambacho watu tunajipanga kumteketeza nduli kabisa kwa kukipa chama nguvu ya aina yake.............tumepeleka wanajeshi wa kutosha bungeni na naamini watafanya zaidi ya yaliyofanyika miaka mitano iliyopita........
Zito naomba na nakuomba tena utulie ili akili zako zilizo nyingi zitumike kiukweliii kukikomboa chama chenye mapinduzi ya kweli.......ccm wanakutizama kama walivyomwangalia marehemu chacha wangwe na lytonga akiwa nccr kipindi hicho........naomba wote tumuombee huyu dogo ili asibadilishwe........maana kifaru kakoswa na risasi(ni maoni yangu kwa hali ninavyoiona na mnaweza kunirekebisha)
 
ZITTO alijitahidi kiasi chake na ametetea jimbo lake, IKUMBUKWE MTU KWAO Hashim Rungwe ni wa Kigoma na alikuwa anagombea urais hivyo watu wake wa karibu ni Kigoma na walimheshimu ZITTO vunnginevyo walikuwa na uwezo wa kumvurugia. Siri ya NCCR Kigoma ni kuwa na mgombea urais ambao watu walijivunia, hivyo walimpigia kura na kumpa wabunge. Tunde na mtazamo huo ndugu zangu.
 
Zitto anastahili pongezi kwa mchango wake pale kigoma. Tusisikitike sana kwa chadema majimbo mengi kukosa pale, kwa kuwa wabunge wengi ni upinzani, tujipongeze kwa hili- wainzania 5-ccm 3
 
Kumbuka hata yeye mwenyewe ilibidi apambane ili kutetea Jimbo lake unadhani CCM wanapenda kumwona anarudi Bungeni na kuwasumbua sumbua usimlaumu bila sababu za msingi..

KUPATA USHINDI KWA UPINZANI SIYO KAZI RAHISI , INAHITAJI JUHUDI NA MAARIFA, KUSHINDWA KUPITA CHADEMA KATIKA MAJIMBO KIGOMA MIMI NAONA SABABU SIYO ZITO, kuna sababu nyingi. afterall tunachotaka ni mapinduzi na upinzni wachukue nafasi, HILO NDILO LA MSINGI, NAOMBA KUWASILISHA HOJA
 
Na ndio maana Zitto alishaanza kutaka kuhama jimbo kwa kuwa alijua kule hapakaliki, bahati yake kapita...huko kwingine angepata aibu.
 
Zitto watanzania wengi sana wametoa maoni ya kukusupport hii ni ishara kwamba wewe ni moja ya resources muhimu kwa chadema na ninaamini umejariwa kutembelea nchi za wenzetu huko ulaya na mashariki ya mbali umewaona walivyo royal kwa vyama vyao na watu wao. Watanzania wangependa kukuona ukiendelea chadema.DR.SLAA ni mentor wako mzuri ambaye sisi tunaamini anaendelea kukupika ufikie kilele cha mafANIKIO KATIKA SIASA.Sisi tulio nje ya chadema tunakuonea shauku jinsi anavyokuandaa huyo mzee SLAA hakika you have a bright future within chadema sphere.BE TOLERANCE YOU GONNA FLY!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
sisi WAHA tunajua tunachokifanya. Upinzani tumeuanza muda mrefu. Enzi za akina Dr. Walid Kabourou. Hatuyumbishwi ovyo. Kikwete alichotufanyia tumeona. Anajitofautisha na watangulizi wake ambao waliamini kuchagua upinzani ni sababu ya kuwanyima maendeleo. Lakini pia hawakumchagua Dr. Slaa kutokana na mwenendo wake mbaya - Muovu. Waha tunaamini Mungu na tunathamini maisha ya Ndoa.
 
Mwanzilishi wa post hii si mkweli na inaonekana ana chuki na Zitto Kabwe. LAKINI TUJIULIZE; KWA NINI WANACHADEMA WANA CHUKI NA ZITTO?. KUNA AJENDA YAO NYUMA.

NIMEMFAHAMU ZITO SIKU NYINGI. NI MPAMBANAJI. REVOLUTIONARY SQUARE PALE MLIMANI ALIKUWA NDIYE MTETEA HAKI ZA WANAFUNZI. ANAYEMCHUKIA BILA SHAKA ANA CHEMBE ZA UMIMI AU U-SISI AU U-KASKAZI AU U-DINI. HAISAIDII KUJENGA CHAMA WALA UMOJA WA WATANZANIA.
 
Back
Top Bottom