Zitto Kabwe For Tanzanian President Candidate - Golden Chance

Status
Not open for further replies.
Naona Zitto ajibu mapigo kwa kujiunga na CUF ili arudishe hadhi yake .ni hapo tu atakapo anza kupaa na huenda hata nafasi ya kugombea Uraisi akapewa ,Zitto hiyo ni Golden Chance kuukwaa Uraisi wa Tanzania kupitia CUF kazi kwako.Hii ni tiketi ambayo ipo wazi kabisa na labda utaona kama masihara lakini nafasi ya kugombea Uraisi kwa tiketi ya CUF ipo wazi kabiza ,Lipumba ni mtu mwenye akili sana na nahisi angependa kupata kijana mbadala ambae ana msimamo wa kuikomboa Nchi hii na mwenye kukubalika katika jamii ,hivyo jishauri na utakuja kunikumbuka ,tatizo vijana mnakuwa mnashindwa kuelewa kuwa Chama kinachowafaa ni CUF ili kupambana na CCM na si chama kingine chochote kile ,ipeleke nguvu yako CUF ichanganywe na ya Maalim Seif tuone kama CCM hawakuanguka.
Wakuu mnasemaje kwa hili ,mpeni ushauri wa bure Zitto.
Nasikia Lwakatale ajuuuuuuta kujunga na Chadema.

Kuhama CHADEMA (chama cha uchagga daima) na kuhamia CUF (chama cha udini na fujo) hakuna tija yoyote. Bora abanane humohumo CHADEMA, ni rahisi kupambana na uchagga kuliko udini, maana uchagga ni kabila moja kati ya 120, lakini huo udini iko kama ni pande mbili tu, fujo isiyoisha. Baki huko CHADEMA kaka, imarisha chama chako utafanikiwa tu.
 
Zitto abaki CHADEMA. Agombee urais mwaka 2015.Mwakani agombee ubunge, na kuendeleza mapambano ya kuongeza nguvu za upinzani bungeni ili kuandaa mazingira mazuri ya uchaguzi 2015 i.e tume huru ya uchaguzi.

Hapo wewe waneena tunaweza kukubaliana. Kama nia ya Zitto ni wenyekiti NAWEZA KUANZISHA CHAMA CHAKE PIA LAKINI KAMA NI U President ASUBIRI 2015 kupitia ticket ya CHADEMA
 
Mwiba umeongea poit sana mimi nakuunga mkono njia pekee kwa Mh.Zitto ni kujiunga na CUF.Chama pekee ambacho ccm wanakiogopa ni cuf hawaogopi chadema wala tlp vyote hivyo wanajua ni vyama ambavyo vimeunndwa kaw malengo ama ya udini,kukomoana au ukanda na sio kushika dola na kuongoza Tanzania na wanajua fika chadema ni sawa na TLP nccr-mageuzi.Huwezi kabisa kukilinganisha na CUF.
Jamani ebu angalieni acheni jazba mbona haihitaji uende chuo?
CUF inapigwa vita na CCM, VYOMBO VYA HABARI,MAJESHI YOTE,NA WENGINE SI VIZURI KUWATA KWA SASA ILA WANAJIFAHAMU VIZURI.
ZITTO NENDA CUF KAKA.
 
Mwiba mkuu nimekupata. kwa kweli Bwana mdogo anaweza kuja Cuf kujiunga lkn watu wengi wanajua Cuf ni chama pekee ambacho kinaenda kidemocras na ambacho ni chama kweli cha upinzani,ni chama ambacho hakina doa,ila kwa kupakaziwa na usalama wa taifa kwa faida ya ccm, tulijaribu kuangalia chadema nguvu yao lkn sasa lipo wazi bora TLP kuliko chadema kwa sababu ya kushirikiana na mafisadi na hapo inakuja ile dhanna kamili kuwa chadema ni ya ccm,na ndio maana kuna baadhi ya viongozi ni wa kweli lkn wanashindwa kufurukuta.
Pr Safari aligombea nafasi ya uenyekiti na Lipumba alimsifu yeye pamoja na yule mwengine alogombania nafasi hiyo,na walipomaliza uchaguzi Lipumba akashinda,na wakapeana mikono,hiyo ndio democras na Pr safari atagombea ubunge kupitia Cuf. yale maneno yaliokuwa yakisemwa ni CCM kupitia usalama wa taifa tu,ilikuwa ni propaganda dhidi ya Cuf lkn hatimaye tumeona kwamba ni uongo baada ya wazee wawili Lipumba na safari kuwa kitu kimoja na hata siku moja hawakujibizana.

Naunga mkono hoja tena kwa vidole kumi sio vitano. lkn nina suali, Je na Lwakatare arudi au?
 
Ama kweli CCM.Inaonekana CCM wamefanikiwa kweli kweli,wakiwa ZANZIBAR wanasema CUF chama cha WAPEMBA wakiwa BARA CUF Udini.Ila wazanzibari ni waelewa wanawapuuza leo hii uchaguzi ukipigwa HURU CCM itaambulia aibu atawabunge na wawakilishi itakuwa kati ya 7 mpaka 10 Zanzibar nzima na wajaribu waone.Ila uku BARA inaonesha vichwa ngumu hawaelewi na utaona wengi wanaosema cuf ni udini ni wakristo ivo tukisema CHADEMA ni chakidini pia tutakosea DR.SLAA PADRI mstaafu,MENGI anae kifadhili ni mshika hazina wa kanisa EAST AFRICA, UKIACHIA UKABILA NA UKRISTO WAKINA MBOWE NA UDUGU WA MTEI,
ZITTO NENDA CUF KAKA.
 
Huo ni utani! Huyo Zitto mnayemfagilia ni activist zaidi kuliko politician. Ila anafaa kwa nafasi aliyonayo sasa kama mbunge. Hana sifa yoyote ya kuwa rais. Halafu CUF sio chama sahihi kwake kwani ni chama chenye sifa mbaya ya udini na hivyo hakikubaliki sana huku Bara. Abakie hapo hapo Chadema ila aache kuwa over ambitious na kujiona ni bora kuliko wanasiasa wenzake.
 
Kwani Rais anatakiwa kuwa na sifa gani? Unaposema hana sifa yoyote ya kuwa Rais, Sifa mojawapo ya kuwa Rais ni uraia... Kwani Zitto sio raia wa Tanzania????

Kwani Rais anatakiwa kuwa na sifa gani? Unaposema hana sifa yoyote ya kuwa Rais, Sifa mojawapo ya kuwa Rais ni uraia... Kwani Zitto sio raia wa Tanzania????

Kama uraia ndiyo umeona ni sifa kubwa ya kuwa rais basi tunao vichaa wengi tu barabarani wanaweza kuukwaa urais.
 
Safari alifanywa nini na Zitto amefanywa nini ?

.

NA LWAKATARE KAKIMBIA NINI?

Pia mwambie na sitta anataka kufanywa nini? Mutungirehi alifanywa nini TLP, Salasini kakimbia nini NCCR,

Zitto pima mwenyewe
 
Nimemsikia leo asubuhi akijibu maswali ya watangazaji wa Power Breakfast - Clouds, akieleza sababu za kujitoa kwake kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti, kwamba amekubali ushauri wa wazee wa Chadema kwamba ajitoe na kwamba eti muda wake haujafika. Zitto alikuwa maarufu sana na hata mimi nilimwona kama kiongozi kijana na mwenye msimamo, lakini alichemsha sana pale alipokuwa Mwenyekiti wa ile Kamati ya Bunge ya kushauri Serikali kununua au kutoinunua mitambo ya Dowans. Something happened there to make Zitto give in and support the government to buy Dowans Machines. Sasa mtu wa hivyo kweli utamwacha agombee Uenyekiti wa Chama kama Chadema kweli? Viongozi wa Juu wa Chadema wana akili na wameona kilichotokea kwa Zitto. Mheshimwa Zitto pale ulipokubali Uenyekiti kwenye ile Kamati ya Kushauri serikali kununua mitambo ya Dowans na majibu mliyotoa pale Bungeni ndipo umaarufu wako ulipopotea.
 
NA LWAKATARE KAKIMBIA NINI?

Pia mwambie na sitta anataka kufanywa nini? Mutungirehi alifanywa nini TLP, Salasini kakimbia nini NCCR,

Zitto pima mwenyewe

Lwakatere hajakimbia,bali baada ya kufanya ubadhirifu,ndipo aliposubiriwa wakati wake umalize,akaitwa akaambiwa baba angalia ulichokifanya hapa,so nafasi yake huwa Mwenyekiti anapendekeza majina matatu amabayo yanapelekwa kwenye baraza kuu kupigiwa kura,sasa kwa kutumia katiba Pr Lipumba kama mwenyekiti akawa hajapeleka jina la Lwakatare,na kumbe bwana mkumbwa alikuwa anatiliwa shaka ya mahusiano na ccm na chadema kabla,mwache abaki huko huko kwenye vurugu,kwetu hatutaki vurugu,mpeni cheo huko kwani yeye ni cheo kwenda mbele.
 
Kwani Rais anatakiwa kuwa na sifa gani? Unaposema hana sifa yoyote ya kuwa Rais, Sifa mojawapo ya kuwa Rais ni uraia... Kwani Zitto sio raia wa Tanzania????

May be sifa watu wengi wanazo lakini bila uwezo wa kuongoza inakuwa kazi bure. Kama huyu wetu wa sasa sifa kibao, je uwezo upo???
 
Wenye mawazo ya kutaka Zitto awe Rais wa nchi yetu yaelekea bado hawajaelewa madhara ambayo Zitto na kundi lake wameyaleta kwa CHADEMA. Katika sakata la CHADEMA lililo hewani sasa hivi linadhihirisha wazi kwamba Zitto kama hafanyi makusudi kukiangamiza CHADEMA kwa kupalilia migawanyiko basi hana ukomavu wa kisiasa kama alivyosema Mzee Mtei.

CHADEMA bado ni chama kichanga. Kilichohitajika ndani ya CHADEMA ni viongozi kuhakikisha wanakuwa na mshikamano wa dhati na wanafanya kila linalowezekana kuepuka mambo ambayo yanaweza kukidhoofisha chama na badala yake wajitahidi kukijenga ili kizidi kuimarika. Kitendo cha Zitto kutaka kugombea ubunge wakati Chama wala hakijawa imara vya kutosha ni kosa kubwa ambalo litaendelea kuigharimu CHADEMA kwa kipindi kirefu. Wapo wanachama wasioelewa ambao tayari wamekwisha ku-take sides na tayari tunaambiwa kuna kundi la Zitto na la Mbowe! Haipendezi.

Kiongozi asiyejua madhara ya makundi ndani ya chama anawezaje kuwa Rais mzuri? CHADEMA hawajaweza kushika uongozi wa nchi wameanza kuwa na makundi, je watafika? Zitto na wengine ndani ya CHADEMA inabidi wajifunze kutoka kwa makosa ya kuwepo 'Mtandao' wa CCM kwamba makundi hayajengi chama ila yanabomoa.
 
Mwacheni abakie huko huko. Wakina Mtei, Lipumba, Maalim, Mbowe wapo vyama vyote.
 
Nauliza kosa la ZITTO aswa ni nini kutaka kugombea Uenyekiti si katiba ya CHADEMA inaruhusu ukiwa mwanachama waweza kugombea cheo chochote katika chama!!!
 
Nimemsikia leo asubuhi akijibu maswali ya watangazaji wa Power Breakfast - Clouds, akieleza sababu za kujitoa kwake kwenye kinyang'anyiro cha Uenyekiti, kwamba amekubali ushauri wa wazee wa Chadema kwamba ajitoe na kwamba eti muda wake haujafika. Zitto alikuwa maarufu sana na hata mimi nilimwona kama kiongozi kijana na mwenye msimamo, lakini alichemsha sana pale alipokuwa Mwenyekiti wa ile Kamati ya Bunge ya kushauri Serikali kununua au kutoinunua mitambo ya Dowans. Something happened there to make Zitto give in and support the government to buy Dowans Machines. Sasa mtu wa hivyo kweli utamwacha agombee Uenyekiti wa Chama kama Chadema kweli? Viongozi wa Juu wa Chadema wana akili na wameona kilichotokea kwa Zitto. Mheshimwa Zitto pale ulipokubali Uenyekiti kwenye ile Kamati ya Kushauri serikali kununua mitambo ya Dowans na majibu mliyotoa pale Bungeni ndipo umaarufu wako ulipopotea.

Kwa kuongezea tu,

Zitto alianza kuharibu pale alipokubali kujiunga na kamati ya Kikwete ya madini (kwa kupingana na viongozi wenzake wa CHADEMA) ambayo alijua kabisa kuwa haitafanya lolote (ukweli umethibitika).

Aliondoa momentum ambayo upinzani ulikuwa umeijenga dhidi ya Kikwete na mafisadi wa CCM (kama unakumbuka zile zomea zomea za nchi nzima). Yaliyofuatia kuhusu Zitto baada ya hapo ni historia.
 
Nauliza kosa la ZITTO aswa ni nini kutaka kugombea Uenyekiti si katiba ya CHADEMA inaruhusu ukiwa mwanachama waweza kugombea cheo chochote katika chama!!!

Zitto hana kosa kugombea uenyekiti wa CHADEMA (au chama chochote kile atakachopenda).

Kinachoongelewa na wengi hapa ni flip flop aliyoonyesha kwenye hii process.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom