Zitto Kabwe azungumzia uteuzi wa M/kiti wa ACT-Wazalendo, mama Anna Mghwira kuwa mkuu wa mkoa

Daaah
Yule mama anafany kazi gani?
Analipwa kiasi gani?
Yaani aache 3mil hivi hivi?
 
Ha ha ha siasa za njaa mbaya sana. Kila mtu anaangalia tumbo lake siasa za bongo DUH zinasikitisha. Unaambiwa adui yako mwombee njaa. Kupiga kelele kote wakipozwa kidogo tu wanatulia na kitu kibaya zaidi hata Zitto hawamwambii anasikia juu juu wakishamtosa!
 
Mbona kuna taarifa kuwa Mwenyekiti tayari keshajiuzulu nafasi yake ili awe huru "kuwatumikia" watanzania kupitia post ya Ukamishna wa mkoa wa Kilimanjaro?
 
Uenyekiti wa ACT- wazalendo si sawa na uenyekiti wa CHADEMA au CCM maana kule ACT mwenye madaraka na chama ni Zitto ambaye alijipachika cheo cha Mtendaji Mkuu wa chama. Yaani uenyekiti au ukatibu mkuu kwenye chama hicho hauna maana yo yote kwani madaraka yote yamehodhiwa na Zitto. Kama ni udikteta basi uko ACT ambako set up (mfumo) wa madaraka umehalalishwa na katiba ya chama.

Wamwache mama Anna Mgwira akapeperushe bendera ya serikali ya JMT kama mkuu wa mkoa, mwenye mamlaka makubwa serikalini yakiwamo ya kuwasweka wakorofi lock up wakiwemo wa vyama vya upinzani including Zitto. Wamwache akachape kazi na serikali ya Magufuli. Ni cheo chenye rank moja na ya uwaziri. Wasimwonee wivu. Ni mama mwerevu na mchapa kazi. Wameshindwa kumtumia vizuri ACT. She can be our next president after 2025 via CCM ticket of course. Mwaka 2020 she will definately be an MP of Singida constituency (the one held by Tundu Lissu presently) through ccm ticket, the number one!!

Wakimkatalia ajiuzuru chama cha Zitto.
 
MILIONI 7 KWA MWEZI KAMA BASIC SALARY.
Yay ndio mshahara wa mkuu wa mkoa ambaye kazi yake kuu kwa wananchi ni kuwafanyia figusu figisu katika harakati zao mbalimbali?ama kweli tunaliwa huku na kule ,kwa utendaji wa wakuu wa mikoa ningependekeza wapate hizo fringe benefit zote lakinu wachukue not more than a milion as a salary
 
chadema imewauma sana wanatamani angechaguliwa mtu kutoka chadema. na kama angechaguliwa kutoka chadema mpaka sasa kungekuwa na thread kama million hivi za kumsifia magu! unafanya mchezo na sitaki nataka!! nani yuko tayari afe njaa kisa chama!! siasa za hivyo bado sana tanzania labda baada ya karne 20 zijazo kama dunia bado itakuwepo!!!
 
Kwa hiyo zito hakua na taarifa yeyote?Halafu raisi wetu mpendwa akiwa unguja aliwahi kusema kamwe hatachagua upinzani nini kimempata?

Kwa ni mh rais amefanya u-turn na kuanza kushirikiana na chama cha Zito?Ngoja tuone sera za Act + ccm zikileta Viwanda!
Usiwaamini wanasiasa
 
Nazidi kushangaa...hivyo akiwa RC atatumika kuzuia shughuli za vyama vya upinzani mkoani mwake?atagandamiza kule alikokuwa upinzani?....njaa ni mbaya sana
 
Wakati tunamshutumu Mh.Zitto na ACT-Wazalendo,tunapaswa kufikiria upande wa pili.Tusiwalaumu,yawezekana teuzi hizi ni mkakati wa serikali na vyombo vyake kuudhoofisha upinzani nchini.

Mh.Zitto ni mmoja wa wanasiasa ambao wameshatangaza hadharani kabisa nia ya kushirikiana na upinzani ili kuunganisha nguvu ya kupambanua na chama "twawala" 2020.Serikali ina mikakati mingi ya kuuzima upinzani nchini,hili la kuwateua baadhi ya watu makini toka upinzani kushika nyadhifa mbalimbali,linaweza kuwa sehemu ya mikakati hiyo miovu.Ni juu ya mteuliwa kusimamia kile anachokiamini,akilambishwa sukari na kugeuka mazima,si suala la chama chake,ni suala lake binafsi.

Kuongoza chama cha siasa ni sawa na kuongoza kusanyiko la kiroho,kiongozi anapowatelekeza wafuasi wake na kuamua kukimbilia malisho mapya serikalini,inavunja moyo wale waliokuamini na kukufuata.Nimemuelewa Mh.Zitto,wao kama chama wanapaswa kukutana na mteuliwa na kumsikiliza,akiamua kuupokea uteuzi,chama kinapaswa kumuweka kando na kutafuta mtu mwingine atakayeweza kubeba "Taswira" ya chama katika eneo hilo.

Kama ambavyo Kitila aliteuliwa kushika wadhifa serikalini na tukaendelea kuwa na imani na ACT,bado tunapaswa kukiamini chama na kamwe tusiyumbishwe na fursa hizi wanazopewa watu muhimu katika chama.Chama ni watu,chama kinapokea watu kutoka sehemu mbalimbali,miongoni mwa wanachama wanaweza kuwa watu maalumu wanaojiunga na chama kwa kazi maalumu,tusitahayari tuwaonapo baadhi ya watu wakitunukiwa vyeo kwa kazi nzuri waliyoifanya kutimiza malengo ya waliowatuma.

Binafsi ninamuamini Zitto na ACT yake,yanayotokea kwenye chama ni nafasi kwa chama kutumia vyombo vyake vya kiintelijensia ili kubaini kilicho nyuma ya teuzi hizi zinazoleta sintofahamu kwetu tulioamua kuuunga mkono upinzani.
 
Back
Top Bottom