Zitto atoa kauli juu ya Zuio la Gesi ya Tanzania kuingia nchini Kenya

Kwa nini tuongee nao wakati wameshachukua hatua tayari? tunachotakiwa Tanzania ni kuchukua hatua tu hakuna haja ya kuongea nao, serikali ipunguze idadi ya ndege zao ( KQ) kuingia nchini basi ,route ya kuingia nchini iwe mara tatu tu kwa siku au mara mbili. Wakenya ni vichwa maji sana,ni vigumu kukaa na kuongea nao bila vitendo. Achana na issue za maziwa ,hili la ndege tutakuwa tumewapata ipasavyo.
 
Safi sana, Wakenya wanazidi kutugwaya, hawajui watz wakiamua kuhamasishana kususia biadhaa za Kenya wataomba poo. Wabongo vurugu za mitandao yajamii hawajawahi kushindwa.
 
sometimes huwa najiuliza kama tuna watu wenye uwezo wa kufikiri huko serikalini. wizara ya viwanda na biashara walitakiwa watoe tamko mara moja kupinga uamuzi wa serikali ya kenya kuzuia fursa za biashara i.e. mitungi ya gesi... serikali ya kenya imekiuka ibara ya 74 ya mkataba wa jumuia ya Africa Mashariki inayotaka uwepo wa fursa sawa katika ushindani wa kibiashara ndani ya jumuia. nanukuu;-
In order to promote the achievement of the objectives of the Community as set out in Article 5 of this Treaty, and in furtherance of Article 2 of this Treaty, the Partner States shall develop and adopt an East African Trade Regime and co-operate in trade liberalisation and development in accordance therewith.
Hii inamaanisha kuwa kenya ime-breach treaty obligation na consequences zake kwenye bilateral trade ni kuwa export ya gesi kwenda kenya itakufa na kwa upande mwingine Tanzania italipa kisasi ( trade retaliation) na italeta sintofahamu kwenye sector ya biashara na jumuia itakosa mvuto (Afya).

Hata hivyo Tanzania na Kenya zime-sign bilateral agreement on trade kwa miaka mingi iliyopita. lakini nchi hizi zimekuwa hazifuati masharti ya mkataba (Makubaliano/agreements). na hii inasababishwa na ushindani plus kudharauliana kwenye mambo nyeti kama haya ya kiuchumi...kwa mfano, mwaka juzi (2015) kenya walitoa ultimatum ya week 2 kwa Tanzania kupitia upya mkataba wa utalii kwa pande mbili unaozuia Min-bus kuingia airport. kuweka historia sawa, makubaliano haya ( bilateral agreement that barred both Kenyan and Tanzanian tourist vans from accessing game parks and international airports) yalisainiwa mwaka 1985...na Tanzania walijibu mapigo kwa kupunguza route za KQ... kwenye vita za namna hii huwa hakuna mshindi-kwa sababu wote tunategemeana!

Ushauri kwa waziri wa viwanda;

waziri mwijage acha kulala na kuota viwanda as if umeshikiwa akili...toa tamko na fanya maamuzi ili kunusuru fursa ya wafanyabiashara wa kibongo. "mwenzenu akimwaga mboga, wewe unamwaga ugali"

Prof




 
Ingekuwa ni serikali ya Kikwete ipo madarakani tayari ungekuta Wakenya wamesha anza kulia.... hapo ni kupunguza idadi ya ndege za KQ kuingia Tz...... kwa wiki ziwe zinafanya ruti moja tu tena ndege moja tu.... hawa jamaa ni wanafiki sana....
 
Hoja kwa hoja,

Fahamu kwanza hoja walizonazo wakenya juu ya jambo hili...

No more cooking gas imports via Tanzania in a week, says PS
MONDAY APRIL 24 2017












kamau.jpg

Petroleum Principal Secretary Andrew Kamau. PHOTO | SALATON NJAU

In Summary
  • Traders will not be allowed to import gas imports via land borders in a week’s time.
  • The move, according to Mr Kamau, is meant to eliminate illegal cooking gas filling plants which have cropped up in various parts of the country posing safety and security risks.
  • The ban is likely to catch the dealers who rely on the gas from Tanzania unawares as most of them denied knowledge of the plan.
ADVERTISEMENT
edwinokoth.jpg

By EDWIN OKOTH
More by this Author
The Ministry of Energy has banned imports of cooking gas through the Kenya-Tanzania border, raising the possibility of a shortage and surge in the price of the commodity.

Petroleum Principal Secretary Andrew Kamau on Monday said traders will not be allowed to import gas imports via land borders in a week’s time.
The move, according to Mr Kamau, is meant to eliminate illegal cooking gas filling plants which have cropped up in various parts of the country posing safety and security risks.

“The Cabinet Secretary has written a letter to Energy Regulatory Commissions, Customs and Kenya Bureau of Standards and designated Mombasa as the only point of import for LPG. So if you want to play in this game, come and invest in Kenya, import through Mombasa and then we can now follow up who is supplying unlicensed dealers. But now this whole thing about Tanzania is a thing of the past,” Mr Kamau told a briefing for the oil marketing companies organised by Kenya Pipeline Company.

Mr Kamau later confirmed that the full implementation will begin before the end of the month, which implies this week.

The OMCs had complained of being undercut by the illegal gas refillers who take their cylinders, fill them and return them into the market.

The ban is, however, likely to catch the dealers who rely on the gas from Tanzania unawares as most of them denied knowledge of the plan.
Energy Dealers Association said it was yet to receive communication regarding the ban.
 
Soko letu la ndani lina mahitaji makubwa sana hasa mikoa ya magharibi kama Kigoma/Kagera.Wengi katika maeneo hayo wangependa kutumia gesi kwa kupikia lakini upatikanaji haujarahisishwa kwa kiasi kikubwa.Kama soko Kenya linalipa hivyo,basi humu ndani kwa logistic hiyo hiyo wanaweza kuingiza hata zaidi ya Kenya. Nchi hiyo ya jirani kwa sasa iko kwenye kampeni ya kununua na kutumia bidhaa za kwao,Kwa maana hiyo watakuwa wanapambana kulinda soko la viwanda vyao na ule utaratibu wetu uliozoeleka wa soko Holera.biashara ni mbinu ila mwamuzi ni mnunuzi hapa.
Wasindikaji wa gesi na wasambazaji ningewaomba wawe makini na hatua hizi za ushindani wa soko na kama wanataka kuliteka soko la Kenya basi wafuate huo utaratibu uliowekwa ila mzigo unaotumwa Kenya uwe mkubwa. Waswahili wanasema samaki mkaange kwa mafuta yake mwenyewe.
 
Ni uoepo utapita tu. Ndio maana sijaona tamko lolote kutoka mamlaka husika
 
Tanzania akili yetu ya kulalamika ndio inatufanya tuchelewe sana katika maendeleo yetu na uoga wa maamuzi ni kikwazo kikubwa kwa taifa letu, the best answer to them is ban all Kenya commodities to our market na kuwazuia kuwauzia malighafi zetu ambazo zinalisha viwanda vyao lazima tukubali hawa ndugu wanaurafiki wa kinafiki kuna solo kubwa sana sadc lakini hatulitumii ipasavyo kuna solo kubwa Uganda Sudan zote mbili Asia na afrika magharibi kule Comoro lakini kwa vile ni waoga wacha watutingishe sisi tupige siasa za mitandao huku tukiwa tunalaumu laumu tu business need extra capacity to innovative new market you can't fear barrier face it
 
Kwa nini tuongee nao wakati wameshachukua hatua tayari? tunachotakiwa Tanzania ni kuchukua hatua tu hakuna haja ya kuongea nao, serikali ipunguze idadi ya ndege zao ( KQ) kuingia nchini basi ,route ya kuingia nchini iwe mara tatu tu kwa siku au mara mbili. Wakenya ni vichwa maji sana,ni vigumu kukaa na kuongea nao bila vitendo. Achana na issue za maziwa ,hili la ndege tutakuwa tumewapata ipasavyo.
Mkuu route tatu kwa siku nyingi sana kwa wiki ni one route that is all hatuwezi kukuza uchumi wetu tukiwa magoigoi ladhima tupate changamoto kama hizo na hakuna kukaa mezani that's all
 
Wanachotakiwa mbongo movie mkuu ni kutengeneza filamu bora na nzuri tutanunua tu mbona enzi za marehemu industry yao ilikuwa sana tatizo lao sasa wanajifanya masuper star wakati hawafika huko na kitu kingine ni jukumu LA serikali kukaa nao ili msambazaji wa hizo movie awalipe kulingana na thamani ya kazi yao? Huwezi lazimisha watu wanunue kitu kibovu,wakenya wao wanalinda bandari yao kwenye miundombinu ya gesi na uzuri kuna utengamano wa A.mashariki kama Zitto alivyoshauri ni vyema wakae mawaziri ili watatue ilo swala
Kama Zito ameshauri mawaziri wakae watatue tatizo lililoibuka kwenye gesi ili kuongeza mapato ya serikali alishindwa nini kushauri waziri Wa Habari akae na Mkuu Wa mikoa na Bongo movie ili washauriane kuboresha kiwango badala ya kutufungia Maduka yetu walalahoi. Kwa furaha ya watu wachache, kama mbwai na iwe mbwai tu INA maana mapato ya serikali ni bora zaidi kuliko kipato cha mtanzania Wa kawaida ambaye akipatacho ndio alacho
 
Safi sana, Wakenya wanazidi kutugwaya, hawajui watz wakiamua kuhamasishana kususia biadhaa za Kenya wataomba poo. Wabongo vurugu za mitandao yajamii hawajawahi kushindwa.
Kuanzia Leo nitapunguza matumizi ya bidhaa zao
 
Ni kweli ni muhimu sana Tanzania nayo ichukue hatua stahiki kuhusu hili suala, Zitto ameongea point. Tukikaa kimya na wao wakaendelea kuleta bidhaa zao huku kwetu bila ya masharti hali ya kuwa wanakataa za kwetu hakutakua na umaana wowote. Ni muhimu kama jumuia ya Afrika Mashariki tuwe na "Win Win situation" ktk biashara tunazofanya miongoni mwetu. Kipindi cha Rais Kikwete walianza kujaribu kwa namna hii hii, Kikwete akajibu kwa hatua zaidi ya zao; wakarudi ktk mstari tukaendelea.
Hili suala siyo dogo, ni muhimu wakajibiwa kimkakati (siyo lazima kutumia ndege kama alivyofanya Kikwete, kuna bidhaa nyingi za Kenya hapa nchini zaidi ya ndege).
 
Kuna umuhimu wa serikali ya Tanzania kuangalia watanzania kuendelea kutumia bandari ya Mombasa wakati hapa Tanzania kuna bandari zaidi ya tatu.
 
Tuvunje hii jumuia haina maana
Big Up I support u 100 percent wakenya maruhuni au crooks in English wamezuia watanzania madaktari wasiajiriwe kenya magufuli jibu mapigo kila mkenya mwenye kibali cha kufanya kazi Tanzania kikiisha usimpe kingine na kuanzia sasa piga marufuku serikali au shirika la umma kununua bidhaa kenya na sekta binafsi kuajiri wakenya au kutoa leseni za biashara kwa wakenya pia wakenya wote wanaofanya kazi Tanzania Kwenye Ngo au mashirika ya dini vibali vyao vikiisha warudi kwao wawaachie wazawa watanzania.Magufuli kwa hili be very serious tubaki na waganda wanyarwanda na warundi let Kenyans go to hell. Zito pigania hilo hata bungeni tuko pamoja
 
Kenya Kuzuia Gesi ya Tanzania: Tanzania ichukue hatua dhidi ya Kenya

Wizara ya Nishati ya Kenya imepiga marufuku gesi ya kupikia kutoka Tanzania kuingia nchini humo. Tamko la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya Kenya linasema ' ndani ya siku 7 kuanzia juzi tarehe 24 Aprili 2017, itakuwa ni marufuku Kwa Kenya kuagiza Gesi ya kupikia kutoka Tanzania '.

Uamuzi huu wa Kenya ni kinyume na misingi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Tanzania na Kenya ni wanachama. Kwa mujibu wa Itifaki ya Soko la Pamoja, bidhaa za nchi zetu zinaruhusiwa kusambaa ndani ya jumuiya bila vikwazo.

Gesi ya kupikia kuingia Kenya hutokea Tanzania Kwa sababu Tanzania ni nchi pekee katika ukanda huu ambayo imewekeza mitambo ya kupokea Gesi na kuiweka kwenye mitungi. Bandari ya Dar Es salaam na mfumo mzuri zaidi wa kupokea gesi kuliko Bandari ya Mombasa na hivyo kuifanya gesi inayotoka Tanzania kuwa na gharama nafuu nchini Kenya kuliko gesi inayoagizwa kupitia bandari ya mombasa.

Uamuzi wa kuzuia Gesi kutoka Tanzania ni uamuzi wenye kulenga kuilinda bandari ya Mombasa Kwa kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kwa kutaka kuifanya Tanzania iendelee kuwa muuzaji wa malighafi kwenda Kenya badala ya bidhaa zilizokamili Kama gesi ya kupikia.

Uamuzi huu wa Serikali ya Kenya una lengo la kuathiri urari wa biashara kati ya Tanzania na Kenya ambapo Kwa miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikiuza bidhaa nyingi zaidi huko Kenya kuliko inazoagiza kutoka nchi hiyo.

Ninamsihi Waziri wa Biashara na Viwanda wa Tanzania afuatilie suala hili na kuzungumza na mwenzake wa Kenya ili waondoe vikwazo Hivi vya biashara ambavyo havina maana yeyote na vinazuia raia wa kenya kupata bidhaa nafuu kutoka Tanzania.

Viwanda vingi vya Kenya hutegemea malighafi kutoka Tanzania, kuzuia gesi ya kupikia na kuendelea kuagiza malighafi za kuendesha viwanda vyao ni sera ya Kenya kuifanya Tanzania kuwa chanzo cha malighafi tu na sio chanzo cha bidhaa zilizoongezwa thamani.

Serikali ya Tanzania isikubali hili na ianze mazungumzo mara moja na Serikali ya Kenya ili Watanzania wanaouza gesi ya kupikia huko Kenya waendelee kuuza na kutumia Bandari ya Dar Es Salaam. Kama Serikali ya Kenya ikiendelea na msimamo wake basi Tanzania ichukue msimamo kama huo Kwa bidhaa za Kenya Kama maziwa ambayo yamejaa kwenye soko letu.

Zitto Kabwe, Mb
Kigoma mjini
26/4/2017

Absolutely ZZK. Scratch my back, I scratch yours!! Time for bullying each other are over. Kenya has many advantages in manufacturing industry as compared to Tanzania. They should never try to deprive us the little advantage we have!!
 
Back
Top Bottom