Zitto asema hatahama Chadema

Mh.Zitto ni bora ukajisikia aibu kidogo japo unyamaze kwa kipindi tukusahau kidogo.Maana sasa unaonekana kama yule MPIGA FILIMBI WA HAMELINI WA ENZI HIZO.Kumbuka watanzania wa leo si wa mwaka 2005 wakati unaingia ubungeni, kwa sasa wanakushangaa unavyojidhalilisha, waachie watu wakupime wataongea tu na kutoa kama uko sawa au la .

Zitto Unatakiwa uige ustaarabu wa kunyamaza kama wa Dr.W.P.Slaa, yeye kanyamaza kawaachia watanzania wampime.Matokeo ya ukimya wa Dr.Slaa umeyashuhudia mwenyewe, kila kukicha achukua NISHANI na pongezi, sasa wewe umebaki kupiga kelele utadhani hujaenda shule.

ZITTO sasa tunakufananisha na Makamba na mgeja
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.
 
Bro Zitto nakupongeza kwa kuwa muelewa, mimi binafs natambua fikra zako naamini kabisa kwamba unadhamira njema kwa chama, ila kuna baadhi ya wa watu wanashindwa kutafsir vyema dhamira yako, bg up bro tujenge chama chetu.
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.

Mkuu zitto, nadhani hakuna anayepinga usiongee na wananchi na pia hakuna mtu anayepinga wanahabari wasikunukuu. Ambacho wanajadili watu ni kile unachotamka. Kwamba huna busara na ukomavu wa kujua nini useme wakati gani na kabla ya kutoa matamshi yoyote upime madhara yake kwako na kwa chama.

Ambacho watu wamekuwa wakikushauri mara zote hivi karibuni ni kwamba ukae kimya kidogo upepo mchafu dhidi yako utulie.

Kwamba kuna watu wanaokuchukia siwezi kulizungumzia. Lakini kwa nini usioneshe busara kuliko wabaya wako ili watu wachambue? Kuonesha jeuri haitufanyi sisi tukuone wewe wa maana au mwenye akili kuliko wao

si unaona mwenyekiti wenu wa mkoa wa Mbeya alivyofanya. Tuhuma zimekuja akawa mdogo hakufanya jeuri yoyote. Yalivyozidi akakaa mbeni, tena hakuhama chama. Baada ya uchunguzi amerudishwa na sasa amekuwa maarufu na anaheshimiwa zaidi. Nadhani wale wabaya wake sasa hawatakaa wamguse tena
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.

Wewe kijana una akili sana..hawa jamaa zako wakiwatumia mamluki wao humu jamvini wana taka wa kufrustrate kama walivyofanya kwa Kaburu ili chama ukione kichungu na uwaachie tena baada ya wewe binafsi na Kaburu kushiriki kukijenga katika hali ilivyo sasa hivi. Hawa watu wanataka wakufanye wewe kama muwa tu yaani ukishakwisha utamu wautupe.

Msimamo uliouonyesha ni muhimu na muweke Mungu mbele sana yeye ndie mlinzi. Naamini na sioni kama ulitania Masheikh wa Ujiji lazima walikufanyia duwa, nimefarijika mno siku ile kupna vijana wa mdrasa wakija kukusomea duwa pale Aghakan Hospital. Baada ya kumaliza thread hii ijumaa ya leo nakutilia ubani..inshAllah Mungu akuhifadhi na akulinde na kila aina ya ubaya.

Sheikh Yahya
Magomeni.
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na
wafuasi wao.

Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.
Huhitaji kuwa na digirii kupambanua uliyoyazungumza TBC mwezi ulopita!
 
@ Zitto
hivi issue za mayor zimefikia wapi katika halmashauri nne, mpaka sasa kuna uwezekano wa Chadema kuchukua ngapi, jana nilisikia CCM imechukua baadhi, ile ambayo mkutano ulivunjika, uchaguzi utafanyika lini?
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.

Je ni kweli ulisema haya maneno kama ilivyoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi la leo??

Zitto aliuambia mkutano wa hadhara kuwa kelele zote ndani ya Chadema zimetokana na fitina zinazotengenezwa dhidi yake kwa kuwa kuna uwezekano kwake wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
"Baada ya uchaguzi kumalizika, watu sasa wanajipanga kwa ajili ya uchaguzi mwingine. Kuna watu wanaotaka nihame Chadema kwa kuwa wananiona ni kikwazo kwao, lakini nasema siwezi kuhama kwa kuwa nina mtazamo wa mbele wa kugombea urais," alisema Zitto.

Au walikuqoute vibaya tu??
 
The only problem with Zitto Kabwe is seeking for popularity and mostly that preceding his political party.Akili zake muda mwingi zinafikiria umaarufu binafsi.Hajengi bali anabomoa.
 
Hapo tumekuelewa lakini tunachohitaji kwako kama mmoja wa viongozi wa juu wa chama KAA KIMYA usubiri hali ya hewa itulie.Kwa sisi tulio katika ndoa, panapotokea mgongano ndani ya nyumba busara inayotawala huwa ni mmoja wa wanandoa kujishusha hatimaye na mwingine hufuata nyayo na hapo harmony inarejea as usual.

Sasa wewe bro hutaki kufuata yale chama kilichofanya.Tunakumbuka msemaji wa CDM tangu alipotoa msimamo wa chama alirejea kukaa kimya cha ajabu wewe umeendelea kufukuta.Hii si vema mheshimiwa,tafadhali ruhusu busara ikamate nafasi yake, watu watakuheshimu zaidi.unafanya ndivyo sivyo
 
Zitto,umepewa heshima kubwa sana ndani ya Chadema lakini inaelekea bei yako imeshajulikana kwa wakubwa na huna ujanja.Umeimeza ndoana na hutatoka katika mdomo wa wasioipenda nchi hii.
Unaonyesha kabisa kuwa hupo katika collective responsibility na unataka kujipambanua kuwa wewe ni tofauti na wenzio.
Umeonyeshwa vipande vidogo tu vya udhaifu wako na kama unataka ubaki Chadema kiri makosa na jisahihishe la sivyo utafukuzwa ukiwa umeshavuliwa nguo na hutakuwa na thamani hata kwa hao wanaokuona wa maana sasa.
Binafsi nina mapenzi makubwa nawe,I wish ungebaki Chadema lakini If wishes were horses beggars could ride!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.

Mh Zitto nakupongeza kwa kujitokeza humu na kutoa ufafanuzi, Naomba niulize maswali mawili tu.

1. Kwa nini unapinga maswala ya ndani ya chama hadi kwenye media, kwani mkiyamaliza kwenye chama kuna tatizo gani?
2. Kwa nini umekuwa ukijitangaza kugombea mara Umwenyekiti, Urais hata kabla muda wako haujafika, kwa sababu mimi naamini miaka kama kumi na tano ijayo utakuwa angalau kama umetulia waTZ wanaweza wakakupendekeza kugombea kuliko kung'ng'ania sasa wakati kuna watu wanakubalika na wana uzoefu kuliko wewe?

Ahsante Sana.
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma.
Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.

Katika hatua nyingine, Zitto aliwataka viongozi wa Chadema kujiuliza sababu zilizosababisha NCCR Mageuzi kushinda majimbo manne mkoani Kigoma huku walioshinda ubunge wakiwa wanachama walioihama Chadema.
"Viongozi (Chadema), tunapaswa kukaa chini na kutafakari kwa kina, tatizo lipo kwetu sisi viongozi au tulisimika wagombea wasiokubalika?
"Kati ya wabunge wanne wa NCCR, watatu walikuwa viongozi wetu wa chama hadi mwaka 2009 na kama tungekaa nao vizuri, pengine leo hii wangekuwa wabunge wetu na kuongeza idadi yetu Kigoma."Mwananchi Newspaper.

Mh.Zito.
Kwa mtazamo wangu bado hujajifunza nini cha kuongea,labda kama gazeti limekunuku vibaya.
Habari hiyo hapo juu kwenye nyekundu kwa mtu mwenye kumbukumbu nzuri, wewe ulikuwa mbele kuwatetea unaowataja kupata Ubunge kupitia Nccr-Mageuzi wakati wanafukuzwa CDM kwa sababu za kinidhamu.
Usitake kuwa aminisha wasomaji wa Jf na watu wengine kuwa ndani ya CDM kuna viongozi ambao wana matatizo.
Ni na wasiwasi mkubwa kuwa bado kwa kauli kama hizi wewe unaweza kuwa mamluki wa kwanza ndani ya CDM kuliko hao unaodhani ndiyo wenye matatizo,wewe kama Naibu Katibu Mkuu huwezi kuja na kauli kama hizi hapo juu na watu wenye akili timamu waje kukuamini,binafsi bado kabisa.

NB.Kwa Kupitia JF umepewa ushauri mwingi na wenye busara lakini bado unarudi nyuma kuliko kusonga mbele.
 
Jamani muweke akiba ya maneno mnaposema. Mjue mazingira ya mkutano wangu. Nilikuwa nina mkutano wa hadhara Ujiji kwa ajili ya kufafanua uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kigoma. Ulikuwa mkutano wangu wa kwanza ambapo ilikuwa ni lazima nifafanue mambo mbalimbali. Sasa huwezi kuzuia media kuandika habari, kuna uhuru wa vyombo vya habari.
Nina haki ya kuzungumza na watu wangu mkoani kwangu na kuwafafanulia masuala mbali mbali.
Siku zote msimamo wangu ni kuwa siwezi kuondoka chadema. Sina sababu yeyote na mwenye kutaka niondoke chadema, kama ni mwanachadema ataondoka yeye na kama si mwanachadema abaki anaangalia tu kama fisi!
Tuhuma kuwa ninahujumu chama ni uzushi, uwongo na chuki tu za watu na wafuasi wao.
Dhamira yangu ni kujenga chama changu kipate mafanikio zaidi chaguzi zijazo ikiwemo chaguzi ndogo.

hahahaha,napata picha ya huyu mnyama anavo suburi mifupa kwa usongo,lakini haitumii ipasavyo zaidi ya kula "kaulaini kadogo" kisha anautupa kule
 
Zitto, ni kweli umesema bado utawasiliana na JK akuletee maendeleo kwenye jimbo lako? Je, kwanini usiwasiliane naye akaacha kunyanyasa na kudhulumu haki na maendeleo ya Chadema? Arusha? Mwanza?
 
Back
Top Bottom