Zitto amzidi kete Spika

utetezi wa Lema na Mchungaji Msigwa umeishia wapi??kila siku uthibitishi,sijui mwongozo...wanatuboa tu, hakuna tija yoyote
 
Friday, 01 July 2011 08:26

AWASILISHA USHAHIDI KUTHIBITISHA KWAMBA LILIRUBUNIWA

Kizitto Noya na Edwin Mjwahuzi, Dodoma

WAKATI Ofisi ya Bunge ikigoma kumsaidia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuthibitisha madai yake kuwa Baraza hilo limerubuniwa, mbunge huyo amewasilisha kurasa nne za ushahidi huo akitumia dokezo la kikao hicho cha siri.

Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zilisema kuwa Zitto aliwasilisha ushahidi huo kwenye Ofisi ya Bunge jana mchana, huku taarifa zaidi zikionyesha kuwa aliwasilisha ushahidi huo ukiwa na hoja tatu kuthibitisha madai yake.

Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge huyo aliwasilisha ushahidi wake uliosomeka “Tofauti kati ya mapendekezo ya Waraka wa Barazaa la Mawaziri na Pendekezo la Azimio la Bunge lililoletwa bungeni kuhusu kuongeza muda wa Shirika Hodhi la Mali za Mashnirika ya Umma, yaani Consolidated Holding Corporation (CHC)" .

"Amewasilisha ushahidi wake leo, uko hapa unafanyiwa kazi," alisema Joel alipoulizwa na gazeti hili.

Juzi, Spika Anne Makinda alimwongezea muda Zitto hadi Jumatatu Juni 4 mwaka huu, kuthibitisha madai yake hayo baada ya kueleza kuwa alishindwa kufanya hivyo juzi, Juni 29 kutokana na ofisi ya Spika kugoma kumsaidia kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa kuwa ni siri.

Akithibitisha hoja zake katika ushahidi huo ambao gazeti hili umefanikiwa kuuona, Zitto alisema, Azimio la Bunge lililowasilishwa bungeni na Serikali kabla ya marekebisho lilitaka CHC iongezewe muda wa mpito wa miaka mitatu na baadaye kazi zitakazokuwa zimebaki zipelekwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina ni tofauti na mapendekezo ya kitaalamu yaliyofikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa maelezo ya Zitto, waraka wa wataalamu ulikuwa na mapendekezo ya aina mbili na kwamba hakuna hata pendekezo moja katika mapendekezo hayo lililozungumzia CHC kuongezewa muda wa miaka mitatu.

"Pendekezo la kwanza linalopatikana katika Aya ya 11.0 ya waraka huo, lilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu. Pendekezo la pili linalopatikana katika Aya ya 12.0 ya waraka huo, liligusia mpango mbadala wa kuiongezea CHC muda wa miaka 5," ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Katika ushahidi huo, Zitto alisema Aya ya sita ya Azimio la Bunge ilianza kujenga hoja ya kutaka CHC iongezewe muda wa mpito na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina. Alisema aya hiyo ilisomeka hivi:

"Na kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuiongeza muda wa mpito wa shirika na Serikali inaandaa na kukamilisha utaratibu wa kuhamishia majukumu ya CHC kwenye Ofisi ya Hazina.

"Wakati Azimio lililoletwa bungeni lilijenga hoja hiyo ya kutaka majukumu ya CHC yaje kuhamishiwa kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, Waraka wa Baraza la Mawaziri katika pendekezo lake la pili, umetahadharisha kuwa mpango wa kuhamishia kazi za CHC kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, utakabiliwa na changamoto kubwa,"ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Ushahidi wake huo kwenye hoja ya tatu ulisema kuwa, wakati Azimio hilo lililoletwa bungeni (kabla ya kurekebishwa) lilijikita katika kutaka CHC iongezewe miaka mitatu na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, hitimisho la waraka uliowasilishwa kwa Baraza la Mawaziri katika Aya ya 13 linasomeka:

"Waheshimiwa mawaziri, mnombwa kutafakari mapendekezo yaliyomo kwenye Aya ya 11 ya waraka huu na kumshauri Mheshimiwa Rais ayakubali na aagize utekelezaji wake

"Hivi ni dhahiri kuwa Baraza lamawaziri lilikiuka maoni na ushauri wa wadau na watalaamu wote waliotaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu; na dhahiri kuwa Seriakli ilikiuka mapendekezo na sababu zake zote za msingi zilizowasilishwa katika kikao hicho ambazo zilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu" inahitimisha taarifa hiyo.

Juni 23 mwaka huu wakati anachangia Azimio hilo, Zitto alisisitiza mara tatu kwamba Baraza la Mawaziri limerubuniwa kufikia hatua hiyo na akawataka wabunge kwa umoja wao kutokubali kupitisha azimio hilo kwa kuwa lipo kwa maslahi ya watu.

"Waheshimiwa wabunge, nawaombeni kwa umoja wetu tulikatae azimio hilo, hicho sicho tulichokubaliana kufanya. Tayari tumeiagiza CHC kufuatilia madeni yetu kwenye kampuni za umma halafu leo, tunataka kuliua shirika hili? alihoji Zitto kabla Spika Makinda hajamtaka athibitishe kauli hiyo.

Kadhalika, wakati Makinda akimwongezea Zitto muda wa kuthibitisha madai yake alisema “Waheshimiwa wabunge itakumbukwa kuwa tarehe 23 mwezi huu Mheshimiwa Zitto wakati akichangia Azimio la Serikali kutaka kuliongezea uhai Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC), alitoa tuhuma bungeni kwamba Baraza la Mawaziri, limerubuniwa kufikia maamuzi hayo."

Aliongeza: "Itakumbwa pia kuwa baada ya kauli hiyo, nilimtaka (Zitto) alete ushahidi ifikapo tarehe 29 Juni yaani leo. Sasa kwa kuwa siku yenyewe ya kuleta ushahidi ni leo, naona bora nitoe taarifa rasmi kwenu."

"Kwamba siku ileile ya tarehe 23, Mheshimiwa Zitto aliniandikia barua kuniomba nimsaidie kumpatia nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopitisha uamuzi huo. Amefanya hivyo kwa kutumia Kanuni ya Haki, Sura na Madaraka ya Bunge zinazompa haki mbunge kuiomba ofisi ya umma kumpa nyaraka anazozihitaji.

Hata hivyo, Makinda alisema, ofisi yake haikuweza kumpatia Zitto nyaraka hizo kwa kuwa vikao vya Baraza la Mawaziri ni siri na nyaraka zake zote hazitolewi kwa umma.

Friday, 01 July 2011 08:26

AWASILISHA USHAHIDI KUTHIBITISHA KWAMBA LILIRUBUNIWA

Kizitto Noya na Edwin Mjwahuzi, Dodoma

WAKATI Ofisi ya Bunge ikigoma kumsaidia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuthibitisha madai yake kuwa Baraza hilo limerubuniwa, mbunge huyo amewasilisha kurasa nne za ushahidi huo akitumia dokezo la kikao hicho cha siri.

Habari zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel zilisema kuwa Zitto aliwasilisha ushahidi huo kwenye Ofisi ya Bunge jana mchana, huku taarifa zaidi zikionyesha kuwa aliwasilisha ushahidi huo ukiwa na hoja tatu kuthibitisha madai yake.

Kwa mujibu wa habari hizo, mbunge huyo aliwasilisha ushahidi wake uliosomeka "Tofauti kati ya mapendekezo ya Waraka wa Barazaa la Mawaziri na Pendekezo la Azimio la Bunge lililoletwa bungeni kuhusu kuongeza muda wa Shirika Hodhi la Mali za Mashnirika ya Umma, yaani Consolidated Holding Corporation (CHC)" .

"Amewasilisha ushahidi wake leo, uko hapa unafanyiwa kazi," alisema Joel alipoulizwa na gazeti hili.

Juzi, Spika Anne Makinda alimwongezea muda Zitto hadi Jumatatu Juni 4 mwaka huu, kuthibitisha madai yake hayo baada ya kueleza kuwa alishindwa kufanya hivyo juzi, Juni 29 kutokana na ofisi ya Spika kugoma kumsaidia kupata nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kwa kuwa ni siri.

Akithibitisha hoja zake katika ushahidi huo ambao gazeti hili umefanikiwa kuuona, Zitto alisema, Azimio la Bunge lililowasilishwa bungeni na Serikali kabla ya marekebisho lilitaka CHC iongezewe muda wa mpito wa miaka mitatu na baadaye kazi zitakazokuwa zimebaki zipelekwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina ni tofauti na mapendekezo ya kitaalamu yaliyofikishwa mbele ya Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa maelezo ya Zitto, waraka wa wataalamu ulikuwa na mapendekezo ya aina mbili na kwamba hakuna hata pendekezo moja katika mapendekezo hayo lililozungumzia CHC kuongezewa muda wa miaka mitatu.

"Pendekezo la kwanza linalopatikana katika Aya ya 11.0 ya waraka huo, lilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu. Pendekezo la pili linalopatikana katika Aya ya 12.0 ya waraka huo, liligusia mpango mbadala wa kuiongezea CHC muda wa miaka 5," ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Katika ushahidi huo, Zitto alisema Aya ya sita ya Azimio la Bunge ilianza kujenga hoja ya kutaka CHC iongezewe muda wa mpito na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye Ofisi ya Msajili wa Hazina. Alisema aya hiyo ilisomeka hivi:

"Na kwa kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuiongeza muda wa mpito wa shirika na Serikali inaandaa na kukamilisha utaratibu wa kuhamishia majukumu ya CHC kwenye Ofisi ya Hazina.

"Wakati Azimio lililoletwa bungeni lilijenga hoja hiyo ya kutaka majukumu ya CHC yaje kuhamishiwa kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, Waraka wa Baraza la Mawaziri katika pendekezo lake la pili, umetahadharisha kuwa mpango wa kuhamishia kazi za CHC kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, utakabiliwa na changamoto kubwa,"ilisema sehemu ya ushahidi huo.

Ushahidi wake huo kwenye hoja ya tatu ulisema kuwa, wakati Azimio hilo lililoletwa bungeni (kabla ya kurekebishwa) lilijikita katika kutaka CHC iongezewe miaka mitatu na baadaye majukumu yake yahamishiwe kwenye ofisi ya Msajili wa Hazina, hitimisho la waraka uliowasilishwa kwa Baraza la Mawaziri katika Aya ya 13 linasomeka:

"Waheshimiwa mawaziri, mnombwa kutafakari mapendekezo yaliyomo kwenye Aya ya 11 ya waraka huu na kumshauri Mheshimiwa Rais ayakubali na aagize utekelezaji wake

"Hivi ni dhahiri kuwa Baraza lamawaziri lilikiuka maoni na ushauri wa wadau na watalaamu wote waliotaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu; na dhahiri kuwa Seriakli ilikiuka mapendekezo na sababu zake zote za msingi zilizowasilishwa katika kikao hicho ambazo zilitaka CHC ifanywe kuwa taasisi ya kudumu" inahitimisha taarifa hiyo.

Juni 23 mwaka huu wakati anachangia Azimio hilo, Zitto alisisitiza mara tatu kwamba Baraza la Mawaziri limerubuniwa kufikia hatua hiyo na akawataka wabunge kwa umoja wao kutokubali kupitisha azimio hilo kwa kuwa lipo kwa maslahi ya watu.

"Waheshimiwa wabunge, nawaombeni kwa umoja wetu tulikatae azimio hilo, hicho sicho tulichokubaliana kufanya. Tayari tumeiagiza CHC kufuatilia madeni yetu kwenye kampuni za umma halafu leo, tunataka kuliua shirika hili? alihoji Zitto kabla Spika Makinda hajamtaka athibitishe kauli hiyo.

Kadhalika, wakati Makinda akimwongezea Zitto muda wa kuthibitisha madai yake alisema "Waheshimiwa wabunge itakumbukwa kuwa tarehe 23 mwezi huu Mheshimiwa Zitto wakati akichangia Azimio la Serikali kutaka kuliongezea uhai Shirika Hodhi la Mashirika ya Umma (CHC), alitoa tuhuma bungeni kwamba Baraza la Mawaziri, limerubuniwa kufikia maamuzi hayo."

Aliongeza: "Itakumbwa pia kuwa baada ya kauli hiyo, nilimtaka (Zitto) alete ushahidi ifikapo tarehe 29 Juni yaani leo. Sasa kwa kuwa siku yenyewe ya kuleta ushahidi ni leo, naona bora nitoe taarifa rasmi kwenu."

"Kwamba siku ileile ya tarehe 23, Mheshimiwa Zitto aliniandikia barua kuniomba nimsaidie kumpatia nyaraka za Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichopitisha uamuzi huo. Amefanya hivyo kwa kutumia Kanuni ya Haki, Sura na Madaraka ya Bunge zinazompa haki mbunge kuiomba ofisi ya umma kumpa nyaraka anazozihitaji.

Hata hivyo, Makinda alisema, ofisi yake haikuweza kumpatia Zitto nyaraka hizo kwa kuwa vikao vya Baraza la Mawaziri ni siri na nyaraka zake zote hazitolewi kwa umma.

Zitto bado naendelea kuamini ulipaswa kua mwenyekiti wa chadema, Is it was not a crime, to fight, for what was yours!!!!

Bado mtu makini akiwa ndani ya chama anaweza kufanya kazi ata kama si m/kiti. Jambo la msingi zito afanye kazi ata kama ni mjumbe asiye na cheo chochote. Ndo maana vilaza kibao wameongoza magamba na kwa weredi wa watendaji wamewajenga wananchi maskini kuendele kuwa na imani nao
 
Spika hana jipya na hawezi kutoa maamuzi yoyote hapo. Kwani kuna utetezi au maelezo megi wabunge wameandika katika kujibu tuhuma mbalimbali na kuzithitisha.

Lakini Soika hana maamuzi. Sidhani kama ataweza tolea maamuzi hili wakti akina Lema wa Arusha na Tundu lisu bado.

Spika amekuwa sawa na Mbwa bila meno. Bunge halina meno
 
Tulipochagua tulichagua kwa umakini this time hatukufanya masihara pamoaja na chakachu zao lakini this time they are facing what they have never faced before. Mungu tuongezee viongozi wengine wengi kama hawa na wageuze magamba waache kukubali kila baya linaloletwa mbele yao kana kwamba hawana watoto wala wajukuu ambao wataitaji kuishi katika nchi hii baada yao. ZITTO BIG UP AND KEEP ON DOING YOUR JOB THAT IS WHAT UR THERE FOR
 
Mh. Zitto tunaomba utumwagie humu jamvini uthibitisho wako hata kama kwa jina bandia kama
Mh. Lema alivyofanya ili Spika magamba usiuchakachue ni muhimu tukauona.

Spika wa Magamba Bi Mkora tunaomba utolee uamuzi wa Mh. Lema kuhusu uongo wa PM Pinda,
mbona unaukalia uthibitisho wakati ulishapewa siku nyingi?! Where is your credibility?!
 
Spika hana jipya na hawezi kutoa maamuzi yoyote hapo. Kwani kuna utetezi au maelezo megi wabunge wameandika katika kujibu tuhuma mbalimbali na kuzithitisha.

Lakini Soika hana maamuzi. Sidhani kama ataweza tolea maamuzi hili wakti akina Lema wa Arusha na Tundu lisu bado.

Spika amekuwa sawa na Mbwa bila meno. Bunge halina meno

Natamani Mheshimiwa Sammy Sitta arudi kukalia kiti chake cha Uspika!
Hii issue ingekuwa imeisha. Sammy Sitta alikuwa ni Spika wa Standard and Speed(SS). Kwa hiyo issue hii ya Zitto kulituhumu Baraza la Mawaziri angeikomalia kama alivyofanya kwa case ya RichMonduli!!

Hakuna cha kusema ati NI SIRI wakti Baraza la Mawaziri linapokaa na kujadili maswala nyeti ya kuhusu mstakabali wa Taifa letu kwa kisingizio cha USIRI! Hivi kuna SIRI gani inayozungumziwa hapo? Baraza la Mawaziri wanataka kuwaficha Watanzania kitu gani hapo KAMA SIYO RUSHWA NA KUPINDISHA MAMBO??????!!!!!!!

Hapa bwana kusema kweli hakuna cha SIRI lazima kieleweke. Kama Zitto kama Mwenyekiti anaweza kuingia kwenye vikao nyeti vya Kamati ya Fedha ya Mashirika ya Umma na kuna mambo mengi anayoyafahamu kuhusu Wizara mbalimbali na Maamuzi yana yofikiwa kwenye vikao muhimu vya Mawaziri na Wizara husika kuhusiana pengine na Mashirika yaliyo chini ya Wizara husika. Hivyo hakuna SIRI anayotaka kutuambia Makinda kuwa sisi Watanzania au Zitto hatujui!

Mfano mdogo tu ni pale Zitto na Kamati yake walipobatilisha MAAMUZI YA Waziri Maige kwa TANAPA kupunguza tozo za Watalii kwenye Mbuga za Wanyama, kama sijakosea. Haya yalikuwa maaamuzi ya Waziri lakini Zitto na Kamati yake waliweza kubatilisha kitu hicho na kina hold mpaka sasa. Naamini Zitto hakukurupuka katika hili. Hebu wamwache Zitto atoe ushahidi wake ili Taifa linufaike!

Huyu kigagula Makinda aache kuwadanganya Watanzania na Bunge lake kwa ujumla. Bado mpira anao miguuni pake.

Lazima kieleweke. Hakuna cha Spika kutetea Ufisadi na Uzembe!
 
Back
Top Bottom